Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,632
- 697,796
Upepo unavuma vibaya upande wa ACT wazalendo kupitia kiongozi wake mkuu asiyechaguliwa kwa kura ndugu ZZK.
Amebakiwa na muda mchache muhimu wa kuzicheza karata zake vema la sivyo chama kinaenda kumeguka mapande mawili huku pande kubwa likibaki visiwani na yeye kuachwa na kipande cha bara kisicho na maslahi wala nguvu..!
Je mapito ya CHADEMA yaliyopita na kukiacha chama kiikiwa kimoja na chenye kuimarika zaidi yatawezekana kwa ZZK na ACT yake¿? Kumbuka ZZK ni zao la CHADEMA na alisaidia pakubwa kuiyumbisha pale alipoutaka uenyekiti mwaka 2010/2011?
Mwisho wa mchezo yeye na kundi lake walikimbia CHADEMA na kwenda kuanzisha ACT WAZALENDO ile ya kwanza..Ambayo hata hivyo walihitalifiana na ikazaliwa ACT WZALENDO nyingine chini ya ZZK mwenyewe na washirika wake wengi kutimkia CCM.
Rangi halisi za ZZK zilianza kuonekana kwenye uchaguzi mkuu 2015, akionesha viashiria vingi vya ubinafsi, choyo ,tamaa na usaliti... Baadae ilikuja kuthibitika pasina shaka kwamba huyu ni pandikizi na yuko kww maslahi binafsi zaidi kuliko kazi za kisiasa zenye malengo makubwa kwa manufaa ya wengi.
Kupitia ZZK ACT kikawa chama cha mtu mmoja ama kikundi cha walafi wachache wasioaminiana na wasio wamoja.. Nusura ya ACT ni pale Maalim Seif Hamad Rashidi alipojitoa CUF na kuiiunga na ACT ndio chama kikapata uhai mpya lakini sasa mizizi yake kimamlaka ikahamia visiwani ambako kwa sababu ya Maalim seif chama kikapata viti vya uwakilishi na hatimaye kuunda serikali ya Kitaifa huko Zenji ambapo viongizi wa ACT waliula.
ACT baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 kikawa na sura nyingine tofauti kabisa na hapo kilivyokuwa kabla..ACT ya sasa ni CUF asili ndani ya rangi za zambarau na kwa hakika bila kupepesa wala kupapasa macho nguvu yake iko kisiwani kwenye ruzuku na support ya serikali nzima.
ZZK hana asili na Visiwani na hana ubavu wa kuzi control siasa za CUF..Tangu kuondoka kwa Maalim seif na ile keleb aliyopigwa na mgombea urais jasusi mbobezi, amejaribu kwa kila namna kukidhibiti chama ili kiwe chini ya miliki na mamlaka yake lakini ameshindwa kabisa.
Sasa wanazi wa CUF ndani ya sare ya zambarau wameanza kumchoka na wameshamuanzishia chokochoko za kila aina.. Ana muda mchache wa kuzichanga karata zake vizuri..akiyumba kidogo tu watamtupa nje ya janazi na nje mawimbi ni mengi.
Je wakifanikiwa hili..ni nini future yake kisiasa!? Muda utasema THE SOONEST!
View attachment 2113949