Usanii katika kesi za EPA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usanii katika kesi za EPA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 1, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  Nilisema hapa kwamba hizi kesi zitapigwa kalenda mpaka baada ya uchaguzi wa 2010 halafu watuhumiwa wote wataachiwa huru kwa kukosa ushahidi wa kuwatia hatiani. Hivi ni kweli kesi hii muhimu kwa maslahi ya nchi iliyosababisha wizi wa shilingi 133 bilioni (na si ajabu zaidi maana wizi huu wa 133 bilioni ni mwaka mmoja tu 2005/2006) inakosa hakimu wa kuendesha? Kweli hii awamu ni ya ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya!!! :( :( :(. Nimeshindwa kuifungua kama mnavyojua matatizo ya IPPMEDIA Online

  EPA case adjourned for lack of magistrates

  Posted Tue, March,31 2009
  Source Guardian

  The Kisutu Resident Magistrate`s Court yesterday adjourned the hearing of a theft case of 2,897,265,499/63 from the Bank of Tanzania (BoT) External Payment Arrears account (EPA) because the the High Court had not assigned the magistrates to preside over the case
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu BAK, usilalamike hilo tu, kuna watu kibao wana kesi na wako rumande kwa sababu kama hiyo. Mtuhumiwa ni haki yake kesi kusikilizwa mapema ili kama ana makosa afungwe na kama hana awe huru. Utasikia upelelezi haujakamilika miaka 3, kweli hii ni haki. Tena hiyo miaka yote mtu yuko rumande, kashindwa masharti ya dhamana. Suala lina baki pale pale wale waliopewa (TANU-CCM) nchi toka uhuru imewashinda. Na hii inatokana na kuwa na mazoea lolote watakalofanya watarudishwa madarakani, kwa kupenda ama kwa lazima (wizi wa kura).
   
 3. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,265
  Likes Received: 4,237
  Trophy Points: 280
  Mi nasubiri hiyo ya kina Mramba kama itaisha na wataruhusiwa kugombea au CCM wameshandaa mrithi
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  Mfumwa nakubaliana nawe. Mahakama zetu kuna uzembe wa hali ya juu. Kesi hasa zenye uzito mkubwa kwenye maslahi ya nchi zingeweza kabisa kuendeshwa kila siku ili kumaliza viporo chungu nzima vya kesi za miaka mingi iliyopita. Angalia kesi ya yule kijana aliyempiga Kibao Mwinyi imeendeshwa haraka haraka bila kupigwa kalenda na jamaa kishaadhibiwa. Je kesi ya kupigwa kibao Mwinyi ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa Taifa kuliko kesi ya EPA? Najua hapa watu watakuwa na maoni tofauti.

  Pia wapelelezi wangepewa muda maalum wa kukusanya ushahidi, labda mwaka, kama wanashindwa kupata ushahidi wa kutosha basi watuhumiwa waachiwe. Angali mfano wa kesi ya EPA. Ballali alikuwa Marekani miezi chungu nzima kabla ya "kifo" chake (mimi siamini kama kafa) na wapepelezi muda wote huo (labda kwa kutoambiwa nini cha kufanya na wakubwa wa nchi) waliuacha upotee bure kabisa, muda ambao ungesaidia kupata ushahidi muhimu katika kesi hiyo.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,772
  Trophy Points: 280
  Jeetu akwamisha kesi ya EPA

  Tuesday, 12 May 2009 16:29
  Na Grace Michael
  Majira


  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imeutaka upande wa utetezi katika kesi ya wizi wa mabilioni ya fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kuhakikisha mfanyabiashara maarufu Bw. Jeetu Patel anahudhuria kortini siku iliyopangwa.

  Hatua hiyo ilifikiwa jana baada ya mshitakiwa huyo kushindwa kufika wakati kesi ilipokuwa ianze usikilizwaji wa awali.

  Kesi hiyo ipo mbele ya Jopo la Mahakimu watatu; Bi. Grace Mwakipesile, Bw. John Kahyoza na Bw. Ruwaichi Meela ambao waliiahirisha na kuutaka upande huo kuhakikisha mshitakiwa anakuwepo siku ya usikilizwaji.

  Mshitakiwa huyo alikwama kufika kortini hapo kutokana na kuwa na ahadi ya kuonana na daktari wa matatizo ya moyo kama alivyowahi kuiarifu mahakama hiyo.

  Akiwasilisha ombi la kuahirishwa, wakili wa upande wa utetezi Bw. Mpaya Kamala alidai walipata taarifa kutoka kwa mshitakiwa inayoeleza sababu za kutofika mahakamani.

  "Tunaomba kuahirisha kesi kwani tumepata barua ambayo inaeleza kuwa mshitakiwa ana ahadi ya kuonana na daktari wake, hivyo tunaomba ipangwe tarehe nyingine," aliomba Bw. Mpaya.

  Kutokana na maombi hayo pande zote mbili zilikubaliana kusikiliza kesi hiyo Mei 28 mwaka huu ambapo washitakiwa watasomewa maelezo ya awali.

  Awali Bw. Patel aliwasilisha ombi kortini akidai kushauriwa na Hospitali ya Hindu Mandal kwenda India kuonana na mtaalam wa Moyo hatua iliyokataliwa na kutakiwa kuonana na madaktari wa nchini.

  Mshitakiwa huyo na wenzake wanakabiliwa na kesi ya wizi wa sh. bilioni 2.6 kupitia Kampuni ya Bencon International Ltd ya Tanzania na Matsushita Electric Trading Company ya Japan. Wengine katika kesi hiyo ni Bw. Devendra Patel na Bw. Amit Nandy.
   
Loading...