Usambazaji umeme Bomba Mbili bado ni kizungumkuti

pacoma

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
650
414
Wakazi wa Bomba Mbili kata ya Kivule iliyoko Wilaya Ilala jijini DSM. Wanamwomba Waziri anayehusika na umeme aje kujionea jinsi mradi unavyosuasua, Mradi ulikuwa wa miezi 3 na naibu Waziri alienda alitoa order hiyo, lakini cha kushangaza mpaka sasa takribani miezi 6 hata nusu tu eneo la bomba mbili hawajakamilisha.

Baadhi ya wananchi walikwenda kwa mkurugenzi kuuliza kulikoni,majibu waliyopewa ni ya kisiasa. Mara vifaa hakuna sababu ya Corona haviji, Mara mvua imetukwamisha, Mara fungu hakuna. Kwanza wafanyakazi wa mradi huo hawazidi 10.

Kinachoendelea sasa kwa mujibu wa wakazi wa bomba mbili,ili wasambaze wire mtaani kwenu wananchi wa mtaa ule wanachangishana watoe rushwa kwa wafanyakazi wa mradi ili wapelekewe waya.

MAWAZIRI WENYE DHAMANA MPO, MKUU WA MKOA UPO, WILAYA UPO, NK. Msaidieni Rais. Fuatilieni tatizo liko wapi, nendeni kwa wakazi waambieni nini kinachoendelea katika mradi huo, kwanini haukamiliki? Hili swala litampunguzia Rais wetu kura, pamoja na chama chetu.
 
Huo mradi ndio umekuja hadi huku Viwege! Ila viwege wameweka babadhi ya maeneo. Nlichogundua huwa kuna kuwa na upigaji sana kwenye hii miradi. Unakuta mradi unatakiwa ueneee eneo kubwa lakini wao wanaweka kakipande kadogo tu basi!
 
Back
Top Bottom