Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,152
- 137,156
Nimekuwa nikisoma soma humu tokea 2015 kutoka kwa baadhi ya watu kuwa eti aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA na mgombea urais wa chama hicho mwaka 2010, Dkt. Wilbroad Slaa ni msaliti.
Eti ni msaliti kwa sababu aliamua kuachana na siasa baada ya CHADEMA kuamua kubadili gia angani. Pia, baada ya kuachana na siasa akakataa pia kumuunga mkono mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa.
Sioni kabisa usaliti wa Dkt. Slaa hapo. Ninachokiona ni mtu mwenye msimamo na uadilifu na anayeongozwa na kanuni.
Hivi kweli kabisa mtu na akili yako timamu, kati ya Slaa na CHADEMA, unaweza kumwona Slaa ndiye msaliti?
Kama kuna msaliti basi msaliti huyo ni CHADEMA na si Dkt. Slaa.
CHADEMA walisaliti karibu kila kitu walichokipigania wakiongozwa na Dkt. Slaa. Ni CHADEMA ndiyo waliobadilika. CHADEMA ndiyo wasaliti.
Nyie wote mnaodiriki kumuita Dkt. Slaa kuwa ni msaliti ni vifuu tundu msiojielewa kabisa.