Nakubaliana na wewe kwamba katika Biblia, ni jambo moja tu ambalo kwa hilo ndoa imeruhusiwa kuvunjika nalo ni zinaa.
Naomba ieleweke kwamba mmke anaweza kumuacha mume kwa zinaa vilevile.
Na hapo ni kama msamaha utashindikana kwa sababu biblia hiyohiyo inatufundisha kusamehe na kuwa na upendo bila kuhesabu mabaya.
Nafikiri katika makosa yote hili la kusaliti linakua gumu kusamehe lakini haimaanishi haiwezekani kusamehe.
Mwisho kabisa, hakuna jibu linalotosheleza mazingira yote ya nini kitatokea, unweza kusema utaua mtu na usifanye hivyo, unaweza kusema utamwacha mme/mke wako na usifanye hivyo, unaweza kusema utamsamehe na ukampiga na kumwacha juu. Mazingira ya wakati huo yanachangia sana kuamua nini kinafanyika.
Cha msingi tu ni kujua kwamba usaliti wowote ule kwa mme/mmke una madhara makubwa sana kwenye mahusiano.