Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 65
Nina subiri kwanza yule Mkurugenzi wa BoT aliyewekwa kando na tayari ameishahojiwa na vijana wa kazi apelekwe mahakamani. Baada ya hapo nina uhakika hiyo report ya E&Y itatoka tu kwa kuwa huyo jamaa nina uhakika anayo na ni mtu wa visasi lazima ataimwaga ili kuwakomoa, maana ukimwaga mboga mwenzako anamwaga ugali ili wote tukose!
Kama hataitoa huyo basi katika kutajana tajana lazima kuna watu wataimwaga tu ili kukomoana baada ya kuona huu mchezo mchafu unaoendelea. JK sasa hivi amekalia kaa la moto japo hajui, ila kwa kuwa anahisi sisi bado ni wadanganyika, basi mafisadi wenzake watamuumbua tu!
Mjadala mzuri!!!
Angalizo tu!
Hoja ziko mbili, na nashauri zijadiliwe kama hoja mbili tofauti zisichanganywe! maana naona inaelekea wanabodi wanatafuta majibu ya hoja ya 2. kutoka kwenye hoja ya 1.
1. Hoja ya EPA account ndio tunaojadili kwa muda sasa. (Mwanzilishi wa hili ni Serikali yenyewe)
2. Hoja ya Deep Green Finance, Tanggold etc...(Mwanzilishi Dr. Slaa na Kambi ya Upinzani). Hili lakiko kwenye scope ya lile la kwanza, wala hakuna independent investigation, kama inafanyika ni ya vyombo vya dola ambavyo vinaripoti back to the government.
Yup,
So whether kwa bahati mbaya au double coincidence, hii TISS imetumika both ways lakini in the end, money trail inaishia TISS na serikali inafunga kwa kusema kuwa ni suala la usalama wa taifa.
Exactly this is what I am talking about. Unajua watu wamekuwa wanakwepa sana kuzungumzia hili jambo.....Haya mambo ya kusema kuwa usalama wa taifa ulitumika hapa imegonga pande zote na inabidi TISS wa usalama waje clean kuhusu hili ....
Tutaanza na BOT kwa sasa maana ndio tembo mkubwa chumbani kwa sasa kisha hayo ya TRA pia yatafuata kadri siku zinavyoenda.
African Lady;
I love your persistence ! Ama kweli dada yangu king'anaganizi! humwachii mtu apumue ! Huyo ndugu yangu (kama yupo mpe pole) I can just imagine what he is going through🙂 ( with a light touch).
Your point of view accepted and keep up the good fight my girl; We are in this together for a very long haul!
Zalendohalisi,
Usijali kabisa kuhusu ninachofanya nikitoka kazini kwa sababu ndugu yako (kama yupo nitampa pole) anago through very good time in deed.
... Ukimuuliza Slaa na wote anaofanya nao kazi wanahakika kuwa TISS hapa imetumika kucover jamaa wanaodai kutunza usalama wa nchi yetu.
Muda umefika sasa hii issue iibuliwe upya. Kwa sasa ushahidi upo wa kutosha wa jinsi jamaa wa usalama wa taifa wanavyotumiwa kwenye mambo ya kifisadi. Waandishi wa habari wameomba wapewe copy ya report ya E&Y wamenyimwa kwa visingizio vya usalama wa taifa. I am sick and tired na hawa TISS na visingizio vyao rundo visivyo na msingi.
... Hii TISS iliyotumika hapa kwenye issue ya Tangold lazima ifunguliwe ili ijulikane aliyelipwa hapa ni nani.
It is time to come out clean!
Baada ya hapo Tangold Ltd. haikupokea wala kuingiza fedha zozote kwenye akaunti yake hadi tarehe 6 Juni 2006 ilipohamisha shilingi za Tanzania 220,980,370.00 kwenda ‘TISS.' TISS ni kifupi cha Tanzania Intelligence and Security Service ambalo ni jina la Kiingereza la Idara ya Usalama wa Taifa!
Ufisadi wa usalama wa taifa umewafanya kuwa mambumbumbu hata wasijue kuwa TISS inawahusu wao na kuitumia kila sehemu kwa vile walivyozoea. Fisadi mwingine wa ccm ameitafsiri hiyo TISS ambayo wewe unaiita Tanzania Inter-bank Service system kama Tanzania Internal Surveillance system.
Kalamu hiyo TISS ya benki tafsiri yake sahihi ni
TISS - Tanzania Inter-Bank Settlement System na wala sio Services kama huyo mchovu alivyosema hapo juu.
Hapa kunaonekana kuna free masonry strategies; the "Dons" and "Brothers".
Kwa kuzingatia mabandiko hayo hapo juu thread hii ishapoteza maana na pengine tunajadili kitu kisichokuwepo!
Mie nshapoteza kompasi yangu sijui kaskazini wapi pls help....
....
Agreed na kwa hilo namwonea huruma sana JK kwa vile ana nafasi ya kuacha legacy hata zaidi ya JKN kama atatumia mwanya huu kuwatosa hao wenzake ( damu nzito), moreover everyone for themselves and God for all, asafishe uchafu huo na tuanze upya. Akilifnay hilo atakuwa amejiwekea retirement scene yenye amani na sifa kemkem. Lakini kama ulivyosema mara nyingi,sidhani anaelewa wala kuliona hilo.
You can't say it better; huyo aliyepelekewa hizo pesa through TISS ni nani (of course ni CCM money laundering system na majina tunayo, wala siyo siri e.g Lotto Kitita, Amiko etc) kwa vile we have been duped (to quote Meghji). Na Salome Mbatia kafa na mengi tu kifuani, she knew it all.
(BTW I used kin'ganganizi in a positive way meaning insistence on make a point understood )
ur right mamaaaa hapa lazima tujue huyu usalama wa taifa kila hela ya ufisadi kapelekewa yeye ni nani,,na anaishi wapi
Kasheshe,
kiutendaji uko sahihi, kilichofanyika ni ukaguzi wa EPA. Kuna swali hapa liliulizwa na memba wa JF hapa. Kama wizi umefanyika kwenye nyumba yako, ukaamuka kufanya uchunguzi ukagundua kuwa fanicha zimeibwa toka living room, ukaenda chumba cha wageni ukagundua kuwa vitu vimeibwa, je si jukumu lako kwenda vyumba vyote vya watoto na ikiwezekana nyumba yote kujua kilichotokea?
Hapa mchezo wa maneno wanaoucheza na sisi tunaujua. Wanachojaribu hapa ni kuwachanganya wananchi wa kawaida wasijue kinachoendelea. Ona leo Kikwete anasema kuwa pesa zilizoibwa ni za watanzania na sio za wafadhili! what a shame!
Hapa ni kusukuma back kwao, wanataka tukubali tu na hayo majina waliyotoa huku wakiacha mapapa malafi na walinzi wao wa usalama wa taifa wakipeta tu na mashangingi ndani ya dar!
Mwafrika wa Kike:
I am absolutely flabbagasted by this male chauvenist ZalendoHalisi.
Kwa nini wewe MwK you have time with such a sick mind? Huoni anatafuta njia za kukusitisha kwa kukupaka matope?
Anaacha kuongelea mambo yanayohusika, yeye anaongelea MwK!
Usikatishwe tamaa na watu kama hawa, kwani unagusa maslahi yao hawa.
MWK,
Ushauri wangu kwa upinzani na kwa wanaharakati wote! twende step by step! Let reduce speed a little bit.
1. Tuache serikali ikamilishe hili la EPA ambalo si dogo! Wakishamaliza yaani miezi 5.5 ijayo tuwapongeze kama wakifanya vizuri au tuwahukumu wakiboranga.
2. Bila kujali kwamba wamefanya vizuri au Lah! wakati huo ukifika tuanze na hili la upande wa pili ...deep... deep.... Green ... Green...Tanga... Tengo.. mwana... Gold Gold ...etc.
Kwa nini nasema hivi, vyama vya upinzani vikiyalundika haya pamoja wananchi wataona kwamba Upinzani unalalamika tu wakati wanaona matendo ya serikali yako +ve
- Rais amemsimamisha Gavana!
- Rais ameunda task force
- Rais amesimamisha/freeze EPA account mpaka taratibu zingine zitungwe.
- Gavana Mpya anabadilisha uongozi wa Ndani wa Central Bank.
- Waziri ameteua au kubadili board members
- Task force iko kazini etc
- etc
3. Wananchi wetu hawana uwezo wa kupokea na kuchambua mambo mengi kwa pamoja, hapa JF wenyewe watu wanachanganyikiwa, je vijijini itakuwa je? Opposition wanaweza kukosa maximum gain wasipokuwa makini!
Wana JF na especially my sister the African Lady.
Let us take a deep breath and read between the lines. Ukweli ni kwamba hizo transactions ni fishy yes, and in this case TISS ni Tanzania Inter-Bank Settlement System, na ni system(and I know how it works), currently being used to facilitate inter-bank transactions within local banks in Tanzania. Kinachotokea ni kama hutaki ku-expose who is the actual recipient was hizo pesa na kama ni transansaction within the realm of the local banking system, then kwenye transaction logs zako unaweza kuweka TISS. Ila nivigumu kuiweka hivyo kama transaction ina involve foreign banks (meaning outside your local banking realm) manake sheria za money laundering zitakubana, lakini napo pia kuna mbinu zingine zinazoweza kutumika.
Nadhani issue ya TISS (Idara) kuhusiana na hilo transaction log siyo and we could be barking at the wrong tree! Nadhani kilichotokea ni kuwa pesa hizo zilikombwa mara ya mwisho na wenye akaunti wakatoa order ziwekwe kwenye local account kwenye benki nyingine through TISS (inter-bank settlement) badala ya kuandika cheques etc.
Lingine ni kwamba Tanzania Intelligence Community lina watu very well versed with their profession and most of them are very articulate professionals, na hilo I stand by my comment and I don't have to prove it, ila pia kuna wachache wanaojidai wamo kumbe hawamo na ndio hao tunakumbana nao mitaani mbwembwe nyiingi. Kwa mfano kwa issue ya BOT niliandika majuzi kuwa walimwabia Balali mara nyingi tu kuwa analizwa lakini hakusikia, kumbuka huyu jamaa BWM alimpa kichwa saana.Hata ile document ya kwanza kuhusu BOT scam alionyeshwa na TISS yeye akapuuzia, na hii ni kala ya circulation yake over the internet! Sasa la ajabu ni kwamba, yeye badala ya kusikiliza ushauri wa TISS akatumia bango la TISS (according to Meghji)kuwa malipo ya Kagoda ni kwa shughuli za usalama wa taifa, ambalo pia nina uhakika Mama Meghji amelizua tu. Yeye aliboronga na hata hiyo barua ya ku-retract naamini kaiandika juzi tu! Mbona mwanzoni alikuwa anamtetea Balali. Mama akubali tu kazi imemshinda; alichoweza ni kuziagiza suti za JK for inauguration ceremony hapo alifanya kazi nzuri!
La mwisho ni kwamba tusiliangalie hili la BOT kuwa ni kubwa mno; makubwa yapo ambapo serikali inapoteza over $2 million kila siku na mahali hapo ni TRA. Kama kuna penye ufisadi kikomo ni TRA, kuanzia system yenyewe ya taxation, structure ya shirika lenyewe na viongozi wake ndo basi tena, wakiongozwa na Yona, Mramba, Meghji! Kama kuna wa kuwavalia njuga ni TRA, kwa vile hakuna nchi inayoweza kuendelea kama haina taxation system inayoeleweka. Yetu ni kumliza mchapa kazi!