mkuu mimi sihusiki ila nilisikia tu baada ya mda fulani kupita, kwa hiyo siwezi jua lolote kuhusu hayo.Wakitangaza tena nushtue au huu mwaka hawatangazi
Poa NYOKA tumekusumoa..naona vijana watachangamkia kipindi kingine..Habari wanajamvi, kumekuwana ulinganishi,ukosoaji na maulizo kwa nini nchi zilizoendelea mashirika yao ya kijasusi hutangaza nafasi za kazi kwa uwazi kabisa kama zinavyotangazwa kazi nyingine kwenye vyombo mbalimbali kama magazetini,mitandaoni n.k. baadhi ya wakosoaji huwa ni watu walio katika nchi hizi zilizoendelea hivyo kwako huona kitu cha kawaida ila kwetu hushangaa na kutoa mifano ya mashirika kama CIA, MI6 n.k wakitangaza nafasi za kazi
Ukweli ni kwamba kazi hizi hutangazwa kama kawaida ila tu hazitangazwi direct kabisa kwa kuambiwa unajiriwa na idara ya ujasusi. Utakuta tangazo linahitaji wapishi, wafagiaji n.k lakini unachoenda kukifanya unafanya ukiwa mwajiriwa wa idara. Hii hutokea kulingana na mahitaji ya wakati huo. ila sisemiwote huajiriwa hivyo hapana,ila ikitokea kwa mfano idara ina uhitaji madereva,inamaana zinaweza kutangazwa tu nafasi za kazi za udereva.
Ngoja nitoe mifano hai, majuma kadhaa nyuma kulitangazwa nafasi kwa ajili ya kuwapata vijana wa kuwapa mafunzo ya upigaji picha ili wazunguke mashuleni nchi nzima kwa ajili ya kupiga picha, lakini tangazo lilionesha ni kazi ya mda mfupi na ukilipwa kwa kila kichwa kiasi fulani tu cha kawaida, lakini kweli ilikuwa ni idara. Je vijana wa ngapi wenye degree unaweza ukawaambia kuwa ukapatiwe mafunzo ya kupiga picha alafu azunguke nchi nzima kwa kila kichwa elfu moja wakakubali? Aliyekubali maana yake yupo tayari kufanya kazi yeyote mahala popote bila kujali kwamba ana elimu gani.
Mfano wa pili kulitangzwa kazi kwa watu wenye Diploma ya IT lakini walikuwa wanaenda kuwa waajiriwa wa idara, imagine usawa huu wa masuala ya IT yaliyopamba moto lakini unasikia wanahitajika wa Diploma kwangu tafsiri yake kwanza matarajio ni kwamba wengi wao watakuwa ni vijana wadogo, kwa hiyo watakuwa ni watiifu kwani wengi wao hawajaanza maisha,wengi wao watakuwa hawajaingia kwenye masuala ya ndoa, wengi wao watakuwa wana njaa na kiu ya mafanikio lakini pia miili yao inaweza kuhimili mikiki mikiki ya mafunzokwa urahisi zaidi.
Ni mawazo yangu binafsi, karibuni kwa michango
Hapana sipo Mkuu wala sihusiki, ila nilipata kusikia tu mitaani.Haya tumekusikia mkuu , kwani wewe ndio upo katika nafasi ya kujua ajira zitatoka lini? utustue mimi nimesomea madini au hakuna dili huko? lakini nataka mkataba wa mwaka mmoja tu
ngumu kujua mkuu, hizi story tunasikia baada ya mambo kupita.Zikitangazwa tujulishane wadau nipo tayari na ndio ndoto yangu kubwa.
yah mkuu nimetoa elimu nilichosikia na mimi, unaweza kuongeza elimu zaidiHahahahahaaaaaaaa,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,duniani kuna mengi sana wapaswa kuyajua ndugu mtoa mada ila umejutahidi kutuelimisha asante sana
ina maana nimesikia uongo Mkuu?Mnajua kudanganyana mngejua
nadhani serikali haina migodi mingi,mingi iko kwa sekta binafsi kwa nn usiombe hukoHaya tumekusikia mkuu , kwani wewe ndio upo katika nafasi ya kujua ajira zitatoka lini? utustue mimi nimesomea madini au hakuna dili huko? lakini nataka mkataba wa mwaka mmoja tu