Usalama wa Taifa hutangaza nafasi za kazi ila sio direct kama watu tuvyofikiria

KalistusM

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
235
232
Habari wanajamvi, kumekuwa na ulinganishi,ukosoaji na maulizo kwa nini nchi zilizoendelea mashirika yao ya kijasusi hutangaza nafasi za kazi kwa uwazi kabisa kama zinavyotangazwa kazi nyingine kwenye vyombo mbalimbali kama magazetini,mitandaoni n.k. lakini ni tofauti kwa nchi zetu. Baadhi ya wakosoaji huwa ni watu walio katika nchi hizi zilizoendelea hivyo kwao huona kitu cha kawaida ila hushangaa kwetu halipo hilo jamabo na kutoa mifano ya mashirika kama CIA, MI6 n.k wakitangaza nafasi za kazi kwa uwazi kabisa

Ukweli ni kwamba kazi hizi hutangazwa kama kawaida ila tu hazitangazwi direct kabisa kwa kuambiwa unajiriwa na idara ya ujasusi. Utakuta tangazo linahitaji wapishi, wafagiaji n.k lakini unachoenda kukifanya unafanya ukiwa mwajiriwa wa idara. Hii hutokea kulingana na mahitaji ya wakati huo. ila sisemi wote huajiriwa hivyo hapana,ila ikitokea kwa mfano idara ina uhitaji wa madereva,ina maana zinaweza kutangazwa tu nafasi za kazi za udereva.

Ngoja nitoe mifano hai, majuma kadhaa nyuma kulitangazwa nafasi kwa ajili ya kuwapata vijana wa kuwapa mafunzo ya upigaji picha ili wazunguke mashuleni nchi nzima kwa ajili ya kupiga picha, lakini tangazo lilionesha ni kazi ya mda mfupi na ukilipwa kwa kila kichwa kiasi fulani tu cha kawaida, lakini kweli ilikuwa ni idara. Je vijana wa ngapi wenye degree unaweza ukawaambia kuwa ukapatiwe mafunzo ya kupiga picha alafu azunguke nchi nzima kwa kila kichwa elfu moja wakakubali? Aliyekubali maana yake yupo tayari kufanya kazi yeyote mahala popote bila kujali kwamba ana elimu gani.

Mfano wa pili kulitangzwa kazi kwa watu wenye Diploma ya IT lakini walikuwa wanaenda kuwa waajiriwa wa idara, imagine usawa huu wa masuala ya IT yaliyovyopamba moto lakini unasikia wanahitajika wa Diploma. Kwangu tafsiri yake kwanza matarajio ni kwamba wengi wao watakuwa ni vijana wadogo, kwa hiyo watakuwa ni watiifu kwani wengi wao hawajaanza maisha,wengi wao watakuwa hawajaingia kwenye masuala ya ndoa, wengi wao watakuwa wana njaa na kiu ya mafanikio lakini pia miili yao inaweza kuhimili mikiki mikiki ya mafunzo kwa urahisi zaidi.

Ni mawazo yangu binafsi, karibuni kwa michango
 
Mbona sasa hujaeleweka Mkuu?

Kazi hizo zinatangazwa chini ya Wizara gani? Au taasisi ipi? Maana upo too general.

Kwa mfano, hizo kazi za upigaji picha pamoja na wataalamu wa IT ilitangazwa na nani? Yaani muajiri aliyetangaza nafasi hizo alikuwa nani?

Shukrani.
 
Habari wanajamvi, kumekuwana ulinganishi,ukosoaji na maulizo kwa nini nchi zilizoendelea mashirika yao ya kijasusi hutangaza nafasi za kazi kwa uwazi kabisa kama zinavyotangazwa kazi nyingine kwenye vyombo mbalimbali kama magazetini,mitandaoni n.k. baadhi ya wakosoaji huwa ni watu walio katika nchi hizi zilizoendelea hivyo kwako huona kitu cha kawaida ila kwetu hushangaa na kutoa mifano ya mashirika kama CIA, MI6 n.k wakitangaza nafasi za kazi

Ukweli ni kwamba kazi hizi hutangazwa kama kawaida ila tu hazitangazwi direct kabisa kwa kuambiwa unajiriwa na idara ya ujasusi. Utakuta tangazo linahitaji wapishi, wafagiaji n.k lakini unachoenda kukifanya unafanya ukiwa mwajiriwa wa idara. Hii hutokea kulingana na mahitaji ya wakati huo. ila sisemiwote huajiriwa hivyo hapana,ila ikitokea kwa mfano idara ina uhitaji madereva,inamaana zinaweza kutangazwa tu nafasi za kazi za udereva.

Ngoja nitoe mifano hai, majuma kadhaa nyuma kulitangazwa nafasi kwa ajili ya kuwapata vijana wa kuwapa mafunzo ya upigaji picha ili wazunguke mashuleni nchi nzima kwa ajili ya kupiga picha, lakini tangazo lilionesha ni kazi ya mda mfupi na ukilipwa kwa kila kichwa kiasi fulani tu cha kawaida, lakini kweli ilikuwa ni idara. Je vijana wa ngapi wenye degree unaweza ukawaambia kuwa ukapatiwe mafunzo ya kupiga picha alafu azunguke nchi nzima kwa kila kichwa elfu moja wakakubali? Aliyekubali maana yake yupo tayari kufanya kazi yeyote mahala popote bila kujali kwamba ana elimu gani.

Mfano wa pili kulitangzwa kazi kwa watu wenye Diploma ya IT lakini walikuwa wanaenda kuwa waajiriwa wa idara, imagine usawa huu wa masuala ya IT yaliyopamba moto lakini unasikia wanahitajika wa Diploma kwangu tafsiri yake kwanza matarajio ni kwamba wengi wao watakuwa ni vijana wadogo, kwa hiyo watakuwa ni watiifu kwani wengi wao hawajaanza maisha,wengi wao watakuwa hawajaingia kwenye masuala ya ndoa, wengi wao watakuwa wana njaa na kiu ya mafanikio lakini pia miili yao inaweza kuhimili mikiki mikiki ya mafunzokwa urahisi zaidi.

Ni mawazo yangu binafsi, karibuni kwa michango
Poa NYOKA tumekusumoa..naona vijana watachangamkia kipindi kingine..
 
Hahahahahaaaaaaaa,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,duniani kuna mengi sana wapaswa kuyajua ndugu mtoa mada ila umejutahidi kutuelimisha asante sana
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom