Usalama wa Taifa hutangaza nafasi za kazi ila sio direct kama watu tuvyofikiria

Nikiwa chuo kuna jamaa(mwajiriwa wa makumbusho-ila mimi sikujua hill) alitaka kuniingiza huko-alikuwa ananidodosa vimaswali flan....kuna siku nilichemka nikamwambia kasiri kangu...ndio ukawa mwisho.
.....nilikuja kutana naye baada ya kumaliza chuo nikiwa mwajiriwa Arusha akiwa mkuu wa kitengo wilaya fulan ya mkoa wa Arusha-tukawa marafiki mpaka sasa.

Ni hayo tu kwa Leo...
 
Kama ndivyo ilivyo basi kuajiriwa usalama ni bahati ya mtu na sio sifa na uwezo stahiki.

Kuna mambo mengi hutokea au hata matangazo mengi ya kazi hutanganzwa, sasa kujua kazi hii ni vipi na mwajiri ni nani ni jambo la msingi sana la kuzingatia la kila muombaji.

Ikitokea matangazo yao ni ya namna hiyo sijui kama huwa wanapata watu sahihi au waliokusudiwa, kwa maana yeyote aliye makini haombi kazi kwa bahati nasibu ni lazima afuatilie kwanza juu ya akiombacho.

NB. Kuna matapeli wengi sana mjini na kujua huyu ni tapeli sio kazi rahisi labda kama anaanza utapeli, hivyo sio rahisi kuomba kazi kama huna taarifa za msingi juu ya kazi yenyewe na wahusika ni wakina nani.
 
Kwanza hiyo sio kazi ya kuikimbilia hasa kama unataka kuwa just kwenye maisha yako.
Hii ni kazi mbaya sana ndiyo maana kuna whistleblowing site nyingi zinazoendeshwa na wataalamu maalumu wanajitolea kusaidia watu walio athirika kisaikolojia na wanataka kutoka lakini wanashindwa.

Wengi hawajui tu kiundani na ni sababu wanatamani kuwa.
 
Habari wanajamvi, kumekuwa na ulinganishi,ukosoaji na maulizo kwa nini nchi zilizoendelea mashirika yao ya kijasusi hutangaza nafasi za kazi kwa uwazi kabisa kama zinavyotangazwa kazi nyingine kwenye vyombo mbalimbali kama magazetini,mitandaoni n.k. lakini ni tofauti kwa nchi zetu. Baadhi ya wakosoaji huwa ni watu walio katika nchi hizi zilizoendelea hivyo kwao huona kitu cha kawaida ila hushangaa kwetu halipo hilo jamabo na kutoa mifano ya mashirika kama CIA, MI6 n.k wakitangaza nafasi za kazi kwa uwazi kabisa

Ukweli ni kwamba kazi hizi hutangazwa kama kawaida ila tu hazitangazwi direct kabisa kwa kuambiwa unajiriwa na idara ya ujasusi. Utakuta tangazo linahitaji wapishi, wafagiaji n.k lakini unachoenda kukifanya unafanya ukiwa mwajiriwa wa idara. Hii hutokea kulingana na mahitaji ya wakati huo. ila sisemi wote huajiriwa hivyo hapana,ila ikitokea kwa mfano idara ina uhitaji wa madereva,ina maana zinaweza kutangazwa tu nafasi za kazi za udereva.

Ngoja nitoe mifano hai, majuma kadhaa nyuma kulitangazwa nafasi kwa ajili ya kuwapata vijana wa kuwapa mafunzo ya upigaji picha ili wazunguke mashuleni nchi nzima kwa ajili ya kupiga picha, lakini tangazo lilionesha ni kazi ya mda mfupi na ukilipwa kwa kila kichwa kiasi fulani tu cha kawaida, lakini kweli ilikuwa ni idara. Je vijana wa ngapi wenye degree unaweza ukawaambia kuwa ukapatiwe mafunzo ya kupiga picha alafu azunguke nchi nzima kwa kila kichwa elfu moja wakakubali? Aliyekubali maana yake yupo tayari kufanya kazi yeyote mahala popote bila kujali kwamba ana elimu gani.

Mfano wa pili kulitangzwa kazi kwa watu wenye Diploma ya IT lakini walikuwa wanaenda kuwa waajiriwa wa idara, imagine usawa huu wa masuala ya IT yaliyovyopamba moto lakini unasikia wanahitajika wa Diploma. Kwangu tafsiri yake kwanza matarajio ni kwamba wengi wao watakuwa ni vijana wadogo, kwa hiyo watakuwa ni watiifu kwani wengi wao hawajaanza maisha,wengi wao watakuwa hawajaingia kwenye masuala ya ndoa, wengi wao watakuwa wana njaa na kiu ya mafanikio lakini pia miili yao inaweza kuhimili mikiki mikiki ya mafunzo kwa urahisi zaidi.

Ni mawazo yangu binafsi, karibuni kwa michango
Kimsingi sasa hivi hawa jamaa wanapita sana vyuoni, hasa vya diploma na certificates. Wakifika wanajifanya tu kama kampuni ya recruitment so mnapeleka vyeti wanakagua then mnaandika sponsors ambao sio blood related(sijui kwanini) then watawaambia tutawapigia simu. Na kweli baada ya mda mtapigiwa simu kwa wenye vigezo japo hawatawaambia kama mnaitwa kitengo. Just in short.
 
Mwaka 2007 nilipomaliza masomo pale DIT FTC mkuu wa idara alitujulisha baadhi YA wanafunzi kunawatu wamekuja kwake wanaitaji wafanyakazi wa IT. Tulirudi tukapigishwa interview yakawaida maswali mengi yalihusu historia YA familia.... Baada YA Wiki mbili tukapelekwa hospitali kupimwa kunabaadhi walitemeshwa walionekana afya sio mzuri. Walitupa go ahead YA kuajiriwa sehemu nyingine na wakasema kama tutapata safari itakayo tuweka mbali na dar zaidi mwezi tutoe taarifa na walitupiga pini YA kuowa/kuzaa kiolela... (lazima umjulishe mkuu akupe ruhusa kwanza) jamaa walitufuatilia zaidi YA miaka 2 mwaka 2010 ndio tulikula mkataba..... Tuliopita katika michujo tulikuwa 9 lakini walioweza kuvumilia hadi wakapata ajira walikuwa 5... Wengine subra ilikuwa ngumu tulikuwa na hamu YA pesa ya faster faster.... Jamaa zangu wapo kijitonyama kama IT specialist na wengine telecominicationEng... Naungana na mtoa mada kazi za kitengo IWA azipo wazi Sana na hadi ulambe ajira lazima usote Sana na wakati wanakufuatilia inachukua zaidi YA mwaka ndio utagundua ni wazee wa kitendo upo nao. Mara nyingi tulikuwa tunakutana nao Pale pale DIT Mara ofisi za chuo cha utumishi......
 
vipi hali wanajamvi...nafwatilia kwa karibu mada husika,ningependa tu kufahamishwa kuhusu nafasi za ajira ya jeshi la polisi,na proces zote husika hadi kuingia rasmi...naombeni msaada...natanguliza shukrani
 
Zikitangazwa tena tutumie PM kuwa ni za TISS. ..


Kwa hiyo hata bashite anaweza kuwa TISS?
 
Back
Top Bottom