Usalama barabarani

code4494

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
798
1,205
Hellow JF,
Mnaendeleaje na pilika za maisha za kujenga taifa letu..nlikuwa naomba msaada wa kujua kama dereva unapokamatwa na traffic kipi kinachoanza baina ya askari kukuambia utoe leseni au dereva kujua ni nini sababu ya traffic kukusimamisha?maana Leo nimepigwa faini baada tu ya kutoa leseni huku kosa nikiwa bado sijalijua,na baada ya kuandikiwa ndipo kosa naambiwa ikiwa aliyefanya ni mwingine,imenihuzunisha mno! Na mbaya zaidi hakuna pa kwenda kujitetea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikimbilie kutoa leseni unaposimamishwa, ata akuombe vipi usitoe leseni. Ukimpa tu anaandika anachojisikia.
 
Askari ukimpa leseni tu anakua mbabe atakubambikia kosa lolote sometime wakikuomba leseni unazuga kama unaitafuta hivi uku unapimpima upepo kama katumwa vyeti au ya kubrush viatu tu manake kuna siku nawaonaga kama vile wamepanga kuandikia magari to asa ukikutana nao siku kama hizo hata utoe maelezo gani husikilizwi unapewa za macho fasta
 
Chakwanza kabisa mtambue askari kwa no zake kisha usijenge hofu kwa askari na kama unaona kuna mazingira ya kuonewa omba mwende mahakamani.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo wengi wanaogopa kuwekwa lockup, .maana itabidi uwekwe lockup wakati utaratibu wa kuchukuliwa maelezo na kukupeleka mahakamani unafanywa,, na ukifika pale mahakamani unafikia pia kwenye selo ya mahakama ,,unakutana na watoto wa mbwa wakutoka segerea wanakusaula viwalo vyako kwanza na dundo zuri kama unalo , ,,iyo naionaga pale mahakama ya wilaya kinondoni na ilala
 
Back
Top Bottom