Usajiri wa wachezaji (soccer) bongo.

Sumu ya nyigu

Member
May 18, 2019
57
110
Wakuu naombeni ufafanuzi kidogo kwa mwenye ufahamu kuhusu mfumo wa usajiri wa wachezaj bongo. Tunaposema mchezaji kasajiriwa kwa dau la 80 million mfano, tafsiri yake ni nini? I mean in terms of monthly payments ikoje, au hyo pesa ya usajiri ni tofauti na mshahara wa Kila mwezi? Mwenye info please!
Nawasilisha.
 
Kibongo bongo mchezaji huru(asie na mkataba) ukisikia kasajiliwa kwa dau la milioni 80, ujue hizo ni za kibindoni, anakunja yeye kama yeye, na bado pesa ya mshahara iko pale pale.
 
Kama mchezaji amemaliza mkataba na timu A ananufaika moja kwa moja na signing fee itakayotolewa na timu B. Kama ana wakala wake naye ananufaika na fedha hizo zitakazotolewa ndio maana wakala anaweza kutaka fedha ndefu za mauzo ya mchezaji wake ili na yeye anufaike. Kwa nchi yetu fedha hii ulipwa kwa installment hata mbili kulingana na urefu wa mkataba.
Mshahara ni makubaliano tofauti kati ya mchezaji na timu anayoingia nayo mkataba.
 
Back
Top Bottom