Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,723
Ni ajabu sana kwa hizi timu zetu za Kitanzania Simba na Yanga kufanya mambo kienyeji kienyeji sana ili kuwafurahisha mashabiki wao na sio kuitengeneza timu.
Kuna tetesi kuwa Simba wamemsajili Miquissone, unachojiuliza uyo Kocha alimuona Miquissone kwenye mechi ipi ya kiushindani mpaka akapendekeza asajiliwe? Na je, Simba ina mapungufu gani kwenye eneo lake la pembeni mpaka sasa?
Wamemsajili Klamo, wanaye Banda, wanaye Onana, wanaye Kibu Denis, wanaocheza hizo nafasi wakati huo huo wamesajili mabeki 3 tu? Yaani wanajaza wachezaji kwenye nafasi moja wanasahau wanatakiwa wabalance na nafasi nyingine? Sidhani kama huu ni usajili wa kocha. Huu ni usajili wa viongozi wanaotaka kuutumia kwa maslai yao kwenye uongozi.
Miquissone mwenyewe kakaa nje ya uwanja karibia msimu mzima hajacheza mechi yoyote ya kiushindani mpaka akatemwa timu ya taifa kutokana na kutokuwa fiti, leo hii watu wanajinasibu kumsajili kwa nderemo na vifijo🤔🤔.
Kweli soka la Tanzania ni kivyetu vyetu, nimekubali!