Usaili wa Tax Officers waahirishwa

Parody

Member
Sep 13, 2020
24
69
Juzi kuna mdau aliandika kuwa mitihani ya usaili wa Tax Officers wa TRA umevuja na walikuwa wanasove pepa wakiwa kwenye magari kuelekea Dodoma kwenye usaili. Sasa sekretariet imesema usaili umeahirishwa bila hata kutoa sababu zinazoeleweka.

Kuna kaharufu ka uozo hapa.

Pia, Soma=> Mtihani wa usaili wa Tax Officer (TRA) wavuja

Screenshot 2021-08-10 at 10.05.01.png
 
Sekretarieti ya ajira kwa mara nyingine tena, hawa huwa wananjinasibu ni chombo huru wanafanya mambo kwa uwazi pasipokupendelea mtu.

Ingekuwa ni vyema kwa wasailiwa wote wanaoingia katika usaili wa mahojiano basi pale pindi wanapotoa majina ya watu waliopangiwa kituo cha kazi basi wahakikishe pia kwa wale ambao hawakufaulu usaili basi waweze kuona alama zao ili waweze kujua kama wapo kwenye kanzi data ama lah.

Kama kuna mchezo mchafu kwenye hii taasisi ya kuajiri watanzania ni hapo kwenye majina ya kanzi data, unakuta anapewa kazi mtu ambaye hakuwahi kufanya usaili ama kuwepo katika kanzi data hizo.

Kwa hiyo kuondoa sintofahamu hii wale wote wanaofanikiwa kuingia katika usaili wa mahojiano waweze kuona maksi zao hii itaondoa mashaka kwa walio wengi.

Naomba kama wako humu ndani wapate kulifanyia kazi hili.
 
Wajitafakari upya wao ndo watahini na wasimamizi wakuu kama uvujaji wa mtihani lawama juu yao, kweli Wana watu wameandaliwa kwa ajili ya hizo kazi ndo sababu ya mtihani kuvuja kwa makusudi wapate hairisha vyote na kuwaweka?
 
Iweke hapa pia
Cheki huo Uzi hapo chini comment ya 315, wameiweka mkuu.

 
Juzi kuna mdau aliandika kuwa mitihani ya usaili wa Tax Officers wa TRA umevuja na walikuwa wanasove pepa wakiwa kwenye magari kuelekea Dodoma kwenye usaili. Sasa sekretariet imesema usaili umeahirishwa bila hata kutoa sababu zinazoeleweka.

Kuna kaharufu ka uozo hapa.

Pia, Soma=> Mtihani wa usaili wa Tax Officer (TRA) wavuja

Ni usaili wote umehairishwa, sio Tax Officers peke yake
Screenshot_20210810-180905.png
 
Back
Top Bottom