Usaili TBS: Nafasi 47 kwa watahiniwa zaidi ya 7,450

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Hivi karibuni Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilitangaza nafasi mbalimbali za kazi kupitia tovuti yake. Tayari watahiniwa wameshachaguliwa kwa ajili ya kufanya mtihani wa kuandika kuanzia leo tarehe 31 Julai 2014 mpaka tarehe 1 Agosti 2014 katika ukumbi wa Yombo (University of Dar Es Salaam). TBS ilitangaza jumla ya nafasi 47. Kwa haraka haraka zaidi ya watu 7,450 wamechaguliwa kufanya mtihani huo wa kuandika. Zifuatatizo ni nafasi zilizotangazwa na idadi ya watahiniwa walioitwa kufanya mtihani.

  1. Assistant Accountant II- nafasi 3. Walioitwa kwenye usaili ni watu 1,360.
  2. Assistant Internal Auditor Control II – nafasi 2. Walioitwa kwenye usaili ni watu 266
  3. Accounts Technicians II – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 305.
  4. Human Resource Officer II – nafasi 2. Walioitwa kwenye usaili ni watu 857.
  5. Standards Officer II - nafasi 3. Walioitwa kwenye usaili ni watu 211.
  6. Quality Assurance Officer II. Nafasi 10. Walioitwa kwenye Usaili ni watu 752
  7. Metrologist II – nafasi 3. Walioitwa kwenye usaili ni watu 117.
  8. Maintenance Engineer II – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 89
  9. Maintenance Technician II – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 88.
  10. Laboratory Assistant II – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 61.
  11. Laboratory Technician II – nafasi 2. Walioitwa kwenye usaili ni watu 141.
  12. Computer System Technician I – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 307.
  13. Personal Secretary II – nafasi 3. Walioitwa kwenye usaili ni watu 247.
  14. Corporate and Public Affair Officer II – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 342.
  15. Driver II – nafasi 6. Walioitwa kwenye usaili ni watu 408
  16. Editor II – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 71
  17. Legal Officer II – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 140
  18. Librarian II – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 80.
  19. Record Management Assistant I – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 203.
  20. Record Management Assistant II – nafasi 2. Walioitwa kwenye usaili ni watu 501.
  21. Senior Marketing Officer II – nafasi 1. Walioitwa kwenye usaili ni watu 167.
  22. Packaging Technology Centre Mananger – Nafasi 1. Hakuna aliyeitwa kwenye usaili.
Shirika la kazi duniani (ILO) linapendekeza usaili wa kazi uwape uhakika wa zaidi ya 50% wanaosailiwa. Hii ina maana kuwa mtu anayefanyiwa usaili wa kazi anapaswa kuwa na uhakika wa angalau 50% wa kupata kazi wakati anapofanyiwa usaili. Asilimia 50% maana yake ni kuwa idadi ya wasailiwa isizidi mara mbili ya nafasi za kazi zilizopo.

Kwa mfano kama nafasi ni 47 unapaswa kufanya usaili kwa watu wasiozidi 94. Ila sijui hili pendekezo la ILO ni binding na linatumika pia katika kufanya mtihani ya kuandika.
 
Hii serekali ya ccm hii inashida mno..kuna vijana wengi mno hawana ajira..ila vijana wa kitanzania tunachekanaga nini sisi tuliokimbilia nchi za watu kutafuta fursa
 
Hili"bomu" limeshatajwa kwa muda mrefu tu, kuna waliobeza.
 
Hii serekali ya ccm hii inashida mno..kuna vijana wengi mno hawana ajira..ila vijana wa kitanzania tunachekanaga nini sisi tuliokimbilia nchi za watu kutafuta fursa

Dah bora walioemda kubeba box majuu hakuna magumashi kama huku bongo tatizo la ajira ni kubwa viwanda vyote enzi ya Nyerere vilivokuwa vinaajiri vimekufa wanapeana ajra na kuwaambia vijama wajiajiri tunakoelekea kubaya sana
 
hili ni BOMU. tumkabidhi nchi bwana mamvi atuondolee tatizo hili.
 
Hiyo standard ya ILO haikubaliki. Tuna sera zetu, na kamwe hatutaki kuingiliwa na hao wakoloni wanaojiita ILO. Sera yetu (ni siri yetu ya ndani) ya ajira kwenye taasisi za umma ni kwamba watoto na ndugu wa senior officers kwenye taasisi lazima wapewe kipaombele. At least 50% of the recruitees should be blood relatives of senior officials in the same office (or another office on an agreed exchange basis) na hiyo asilimia itakayobakia wanagawane hao watahiniwa wengine amabao hawana ndugu zao huko ofisini!
 
Nadhani hawa maafisa utumishi wameamua kuonyesha tu kwa jamii hali halisi ya tatizo la ajira kwa jamii.
Nafasi 47 huwezi kuita watu zaidi ya 7000 kwa interview... nonsense
 
Dah bora walioemda kubeba box majuu hakuna magumashi kama huku bongo tatizo la ajira ni kubwa viwanda vyote enzi ya Nyerere vilivokuwa vinaajiri vimekufa wanapeana ajra na kuwaambia vijama wajiajiri tunakoelekea kubaya sana

Kuna mtu mmoja anaitwa waziri mkuu eti anasema siyo tatizo la TZ tu! Sawa lakini sijui inampa faraja gani yeye kama kiongozi.

Hawa wazembe wa CCM kuanzia Mwinyi, MKapa na sasa msanii wetu wameshindwa kutengeneza ajira. Enzi za Nyerere hali ilikuwa hivi;
1. Mutex - Musoma (partially working)
2. Mwatex -Mwanza (partially working)
3. Sunguratex - Dar (Dead)
4. Urafiki -Dar (partially working)
5. Magunia -Moshi (Dead)
6. Phillips -Arusha (Dead)
7. National Matshusta -Dar (Dead)
8. Mbeya Textile -Mbeya (Dead)
9. TAMCO -KIbaha (Now a Yu Tong shade)
10. Canvas -Morogoro (partially working)
11. Bora -Dar (Dead)
12. Moroshoes -Morogoro (?)
13. Tanganyika Parkers (Dead)
14. UFI -Dar (dead)
15. KIZAKU -Mbeya (Dead)
16. National Milling (taken by politicians now calling themselves Bakhresa group)
17. RTC (dead, was good start of local chain of supermarkets)
18. KAMATA (dead)
19. UDA, MWADECO, MUDECO, Kagera-RETCO, all decos in every district (dead)
20. NAPOCO (dead)
20. BHESCO (where are they?)
21. TANNERIES industries (----)

Kwa ujumla nchi ilikuwa imesukwa kutoa ajila. Viwanda vya nguo vilikuwa na waajiliwa zaidi ya 500 kila kimoja wakifanya kazi kwa shift. Hata kama vilifanya vibaya, ilikuwa ni mwanzo wa kufanya masahihisho na kuvipeleka mbele. Akaja Mzee ruksa, yeye hakujua afanye nini! Akaja bwana kiburi na tamaa, yeye akaamua kuuza ili naye apate cha familia. Amekuja huyu msanii yeye hajui kabisa kilichotokea nyuma na badala yake ni kuleta studio za miziki. Ametoa ahadi ya ajira milioni moja, kumbe akimaanisha wauza bar! Leo hii tungesema tuna tatizo lakini si kiasi hiki!
 
Nadhani hawa maafisa utumishi wameamua kuonyesha tu kwa jamii hali halisi ya tatizo la ajira kwa jamii. Nafasi 47 huwezi kuita watu zaidi ya 7000 kwa interview... nonsense
deezekiels aliomba nafasi tatu za kazi TBC, zote ameitwa na zote usaili ulikuwa leo saa 8:30 - 10:00.

Sasa sijui alifanyaje mitihani mitatu kwa kazi tatu kwa wakati mmoja?

Labda atufahamishe kilichotokea.
 
Last edited by a moderator:
deezekiels aliomba nafasi tatu za kazi TBC, zote ameitwa na zote usaili ulikuwa leo saa 8:30 - 10:00.

Sasa sijui alifanyaje mitihani mitatu kwa kazi tatu kwa wakati mmoja?

Labda atufahamishe kilichotokea.

Hao wanaoratibu hizo ajira nao waliajiriwa kimizengwe may be. Tisishangae wanapokuwa na utendaji wa aina hii...
 
Last edited by a moderator:
Kuna mtu mmoja anaitwa waziri mkuu eti anasema siyo tatizo la TZ tu! Sawa lakini sijui inampa faraja gani yeye kama kiongozi.

Siyo tatizo la Tanzania tuu lakini hatuwezi kuchukuwa matatizo ya nchi nyingine ku-justify matatizo yetu.
 
Siyo tatizo la Tanzania tuu lakini hatuwezi kuchukuwa matatizo ya nchi nyingine ku-justify matatizo yetu.

Je, inawezekana kutengeneza ajira (katika mfumo rasmi) kwa kila raia katika nchi?
Kama jibu ni ndiyo, ni namna gani??? (Nadhani ndio la msingi zaidi kutafakari na kujadili kuliko kulalamika)
Kama haiwezekani, ni nini njia mbadala kukabiliana na tatizo la ajira (Rasmi)??
JF Home of Great Thinkers...

From the Far corner!
 
Dah bora walioemda kubeba box majuu hakuna magumashi kama huku bongo tatizo la ajira ni kubwa viwanda vyote enzi ya Nyerere vilivokuwa vinaajiri vimekufa wanapeana ajra na kuwaambia vijama wajiajiri tunakoelekea kubaya sana
Watu humu jf huwa wanatubeza sana..lkn mm mwenyewe nimesoma hali halisi ya hapo bongo ni shida..atlest nchi za watu unaitiwa kazi mbili mbili unakataa tu mwenyewe japo ni kazi za kawaida lkn maisha yanakwenda na unawezakusaidia ndugu bongo..vijana inabidi wakae wajitafakari..
 
Je, inawezekana kutengeneza ajira (katika mfumo rasmi) kwa kila raia katika nchi?
Kama jibu ni ndiyo, ni namna gani??? (Nadhani ndio la msingi zaidi kutafakari na kujadili kuliko kulalamika)
Kama haiwezekani, ni nini njia mbadala kukabiliana na tatizo la ajira (Rasmi)??
JF Home of Great Thinkers...

Kama waliokuwa entrusted with power hawawezi kutatua matatizo ambayo waliyopromise kuyatatua then mimi kama mpiga kura unataka niwasaidiaje hasa wanapotumia matizo ya nchi nyingine kujustify matatizo waliyopromise kuwa watayatatua?

To step into their shoes? I am not a great thinker wao ndiyo great thinkers.

Mie just mpiga kura on the street.
 
sawa tu. waacheni kila mmoja ajaribu bahati yake. sasa kama hakuna ajira wafanyeje?
 
Back
Top Bottom