Halmashauri ya Jiji la Dar yasitisha ada ya maegesho Mjini

Halmashauri ya Jiji la Dar yasitisha ada ya maegesho Mjini

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,279
Reaction score
7,699
TAARIFA KWA UMMA. (2).jpg
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imebatilisha tangazo lililowataka waendesha bodaboda, bajaji na maguta kulipa ada ya maegesho ya Sh100,000 kwa miezi sita au Sh180,000 kwa mwaka, huku baadhi ya madereva wakilalamikia ukamataji na faini ya Sh70,000 wanazodai kukutana nazo wanapoingia katikati ya jiji.

Katika taarifa yake ya Agosti 14, 2026, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Wakili Faraja Nakua amesema tangazo hilo limebatilishwa kwa kuwa halikutoa ufafanuzi wa kutosha kuhusu walengwa, maeneo yaliyokusudiwa, madhumuni ya ada, utaratibu wa utekelezaji na msingi wake kisheria.

“Tangazo hilo halikutoa ufafanuzi toshelevu kuhusu walengwa wa ada hizo, maeneo mahususi yaliyokusudiwa, madhumuni, utaratibu wa utekelezaji wake pamoja na msingi wake kisheria hivyo kusababisha mkanganyiko,” amesema Nakua.

Amesema halmashauri inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, ikiwamo Kifungu cha 93(1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288, huku ikitaja Sheria Ndogo za Udhibiti wa Vyombo vya Usafiri Mjini, Tangazo la Serikali Na.82 la Februari 7, 2025.

“Hadi wakati huo, utekelezaji wa maelekezo ya tangazo tajwa hapo juu umesitishwa,” amesema.

Pia soma:
~
Maafisa usafirishaji wa mtandao, maarufu kama bodaboda za mtandao, wamefunga barabara katika eneo la Chuo cha Biashara (CBE) Posta - Dar
~ Walinzi wa Halmashauri wanakamata Pikipiki Kariakoo kwa kuita "wrong parking" bila utaratibu
 
Tengeneza tatizo alafu litatue uone shujaa....
 
So basically walikurupuka bila kufanya homework yao? Halmashauri nzima inatoa tangazo bila msingi wa sheria, yaani ni mwendo wa trial and error tu kwenye mifuko ya wananchi.
 
Back
Top Bottom