Ndugu watanzania wote (in the voice of profesa Muhongo)
Tuache Jaziba, tuache kulazimisha mapenzi yetu kutimia,tuwe na subra, tujipe nafasi ya kutafakari na kupima mambo haya, tujiweke katika nafasi ya kuwatendea maadui zetu vile ambavyo sisi tungependa kutendewa.
Na zaidi, tufuate ushauri alioutoa Mheshimwa Lusinde jana jioni bungeni, kwamba, "TUSEME KWELI ILI TUFANYE MAAMUZI YA HAKI"
KUHUSU PESA ZA ESCROW KUWA NI ZA UMA ETI KWA SABABU KULIKUWA NA KODI YA VAT NDANI YAKE
Ndugu watanzania wote.
Huu ni upotoshaji, ni uongo na uzushi ambao tunapaswa kuukataa, jambo lolote linalofanywa kwa uovu mwisho wake huwa sio mwema.
Report iliyowasilishwa na PAC katika bunge letu, japo ilitegemewa kuwa msingi wa kulipatia haki Taifa letu, imekuwa ni chanzo cha aibu kwa Taifa zima, hutuwezi kupigania maslahi ya Taifa letu kwa kusema uongo, kuficha ukweli kwa wingi wa meneno yaliyopindishwa pindishwa na kupambwa kwa lugha za ghirba.
UKWELI NI HUU
Kama ambavyo mahusiano ya IPTL na TANESCO yanajurikana, hawa walikuwa na bado wanaendelea kufanya biashara pamoja, IPTL akiwa muuzaji na TANESCO Mnunuzi.
Bila kuzingatia namna wanavyofikia bei ya bidhaa husika, ni wazi IPTL imekuwa ikiipatia INVOICES Tanesco, Ili Tanesco Iilipe IPTL.
Sheria yetu ya kodi ya VAT ya mwaka 1997, imetoa maelekezo yanayowapa wafanyabishara FURSA ya kukusanya kodi ya VAT kutoka kwa wanunuzi wa bidhaa zao, kwa niaba ya TRA.
Kutokana na vigezo vilivyowekwa katika sheria husika, IPTL nao ni wakara wa TRA katika kukusanya kodi ya VAT kutoka Tanesco.
Kutokana na mahusiano ya kibishara kati ya TANESCO NA IPTL, TANESCO Haina mamlaka mpaka leo ya kuchukua maamuzi ya kutoilipa IPTL VAT eti ipeleke VAT hiyo TRA yenyewe.
Hivyo basi, hata katika PESA zilizokuwa kwenye ACCOUNT YA ESCROW, TANESCO walitekeleza wajibu wao wa kisheria na kibiasha kuziweka hela hizo kwenye account hiyo zote za IPTL pamoja na VAT (Ambazo kimsingi zote ni za IPTL), Na wakati malipo yanafanyika kutoka account hiyo, YALIFANYIKA KWA USAHIHI KABISA Kwa PESA zote KULIPWA kwa IPTL. Kwa sababu ni wajibu wa IPTL kukusanya VAT kutoka Tanesco.
TRA walipaswa kuidai IPTL pesa hiyo ndani ya mwezi mmoja baada ya IPTL kuipatia INVOICES Tanesco, bila kujali kama IPTL wanaubishani na Tanesco juu ya usahihi wa INVOICE AMOUNTS au la?.
Huu ndio utaratibu, sio mpya, na wote tunaufahamu, jana nimetoa mfano ambao haukueleweka, ukienda dukani kununua bidhaa, unaambiwa bei ya bidhaa ambayo ndani yake kuna VAT, ukifanya maamuzi ya kununua unamlipa muuzaji pesa zote, NA KUANZIA HAPO ZINAKUWA ZAKE na wewe bidhaa inakuwa yako rasmi.
Swala la wafanyabishara kutopeleka makusanyo ya VAT TRA ni tatizo lingine.
HIVYO BASI
Kama sababu ya msingi ya kudai kwamba zile pesa ni za UMA ni sababu ya VAT COMPONENT KWA ZILE HELA, HUO NI UONGO NI UPOTOSHAJI.
Nawasilisha.