Naomba watanzania tusiwe na jazba.
Tanesco ni mfanyabiashara kama wengine tu
Tanesco ni wafanyabiashara ya kutuuzia umeme. Katika kuuza huo umeme wameweka VAT, ambayo wao wanawajibu wa moja kwa moja kuipeleka TRA. Kama Tanesco hawakupeleka VAT, TRA waibane Tanesco sio IPTL
Ili Tanesco wafanye hiyo biashara ya kutuuzia umeme, lazima wagharamie gharama za uzalishaji ikiwemo kuilipa IPTL (achilia mbali mkinzano wa viwango, ambalo hili ni u-pumbavu wa Tanesco).
Kama ilivyo kwa mlaji yeyote, yeye hulipa gharama ya bidhaa na VAT. Suala la muuzaji kuipeleka hiyo VAT TRA ni la huyo muuzaji sio mnunuzi. IPTL ni muuzaji na Tanesco ni mnunuzi. Hivyo wajibu wa kulipa VAT ya capacity charge TRA ni wa IPTL sio Tanesco.
ESCROW ACCOUNT
Kutokana na mzozo wa rates za capacity charge, ilifunguliwa ili kuhifadhi fedha kwa muda hadi hapo watakapo ridhiana kama Tanesco haibiwi, IPTL wachukue pesa zao, na kama wanaibiwa, basi kiasi walichoibiwa wakipunguze kutoka kwenye hii account na kinachobaki IPTL walipwe.
Suala la kulipa VAT kwa pesa hii lilikuwa na linabaki kuwa la IPTL. Nashangaa kwa nini TRA wameshindwa kuitekeleza sheria ya VAT. Naamini Tanesco walikuwa wanatenga hii pesa baada ya kupokea Tax invoices toka IPTL. IPTL kwa kutoa tax invoice, walitakiwa kulipa VAT (baada ya kujaza VAT return) bila kujali kama wamelipwa na Tanesco au la. Hapa TRA wanatakiwa wajibu, sio kukurupuka na kusema ndani ya fedha za Escrow kuna kodi ya serikali NO.
Kama IPTL hawakulipa VAT hadi leo, TRA wanatakiwa kuwajibika.
KULIPWA PESA HIZO IPTL
Kama Tanesco (mdaiwa wa capacity charge) aliridhika kuwa hakuibiwa ????? basi hakuna tatizo lolote kulipa IPTL pesa yote bila kupunguza kodi yeyote, laba ka TRA waliiagiza Tanesco kuwa wakara wa kuikusanyia kodi zote za IPTL, vinginevyo hakuna kosa.
UTARATIBU WA KUTOA PESA
Kila mkataba una utaratibu wake. Naamini hata wakati wa kufungua hii account, kulikuwa na utaratibu wa namna ya kuja kuifunga. Uangaliwe huo kama ulifuatwa au la. Kama haukufuatwa watu wawajibike kwa hilo na hapa wa kuwajibika ni GAVANA WA BENKI KUU.
MIGAWO
Pamoja na maelezo mazuri mengi ya kujitetea namna pesa ilivokuwa inatoka, hapa kuna tatizo kubwa. Sioni shida mtu kuamua kugawa pesa yake kwa anayemtaka, ila katika hili kuna shida, figure zinarandana???????
1. Inaonesha kuwa muda wa kuamua kulipa IPTL au kurudisha fedha Tanesco ulikuwa bado (na hili ndilo halisia), ila wajanja walitumia mwanya huu kujinufaisha au
2. Mtoaji alikuwa anatakatisha pesa chafu aliyonayo, sio ya IPTL tu bali ni Zaidi hizi. Money Laundering au
3. Wapokeaji ndio vinara wa kusuka mipango ya uchotaji huu, na inaonyesha wako wengi Zaidi ya walitajwa
CAPITAL GAINS
Hili sio suala la pesa hii, TRA, IPTL na wote kwenye mnyororo wa kubadilisha hati fungani (shares) wamechemka na wawajibike.
USHAURI
Tusipoteze uelekeo kwa kungangania kuwa ni za serikali au la.
a) Tujikite kuhoji , je kutoka kwake kulikuwa sahihi kwa maana ya wakati, maana bado kesi ya capacity haijaisha hivyo haikuwa sahihi kutoa hizo pesa, maana iliwekwa BOT kusubiri suluhu.
b) Gavana wa BOT ajibu kama terms of reference za kufungua hii account na namna zilivyotoka ni sahihi? Vinginevyo awajibike na waliomtuma au kumshinikiza
c) Mwanasheria Mkuu, alikuwa sahihi kusema pesa hii haina kodi ya serikali, lakini, kabla ya kutoa hayo maagizo, akiwa mtetezi wa haki za serikali, alitakiwa kujua je VAT ya hiyo fedha, IPTL walilipa kwa wakati TRA? Kama walilipa, ruksa kutoa (kama muda ulikuwa sahihi) kama walikuwa hawajalipa, hakuatakiwa kuruhusu kutoka wakati akijua fika kuwa IPTL iko ICU. Awajibike kwa kutokuwa makini
d) TRA: TRA wanakimbizana na vidagaa Kariakoo, wanaacha kukusanya mabilioni ya VAT (kama IPTL hawakulipa kila mwezi walipotoa invoice za kuidai Tanesco) toka IPTL. Watendaji (Kamishna wakuu na makamishan wa VAT) waliokuwepo toka Escrow account inafunguliwa hadi leo wajibu na kuchukuliwa hatua
e) Kamati ya Zitto, inatakiwa itende haki sio kutumia jazba na chuki binafsi. Wasituaminishe uongo, hasa kusema kulikuwa na pesa za serikali. Wao wangesema, kwa kuwa Tanesco ni shirika la umma, kama wakishinda kesi, itakuwa kazi sana kupata pesa yao toka IPTL. Waache haya maneno ya inaweza kuwemo
..
Nawasilisha