Usahihi Kuhusu DVR kwa Members Wote:

Usahihi Kuhusu DVR kwa Members Wote:

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Posts
4,694
Reaction score
793
DVR- Ni kifaa cha kutunzia picha za video ambazo zimepigwa na Camera Kwa matumizi ya baadaye mara nyingi zinatumika kwenye ulinzi kwa kuunganisha na Closed Circuit TV - CCTV. DVR yenyewe haipigi picha...

Kwa kifupi... mfumo wenyewe uko hivi....

1. Unahitaji Camera {moja au zaidi, nyingi na zilizowekwa kwenye pembe mbalimbali ndizo zina-guarantee fully coverage ya tukio}

2. Unahitaji kifaa cha kutunzia hizo picha zinazotoka kwenye camera nyingi... ambacho mara nyingi kinaitwa DVR-- hii ni computer zenye Hard Disk yenye uwezo wa kuweka kumbukumbu nyingi. Na ina software malaaumu kwa ajili ya ku-play live tukio lolote ambalo unataka ku-rewind la Camera yoyote... Walinzi wa makampuni ya Ulinzi wanatumia sana. Au Wapiga Picha za Harusi wanatumia sana ku-rewind live kwenye tukio ambalo wamelipenda including kuweka slow motion. Mara nyingi kama unapenda ku-rewind matukio live lazima basi uweke Monitor/TV ya kuonyesha hayo matukio. Lakini kama huhitaji huna haja ya kuwa na monitor na kama unaamini mitambo yako kweli ina-record/tunza maana bila monitor huwezi kuverify kweli kama utunzaji unafanyika.

3.Kwa kuwa una Camera nyingi, unahitaji kuziunganisha kwenye hiyo DVR yako au kifaa cha kutunzia na ku-rewind picha kwa ajili ya ku-view... hapa unahitaji mfumo wa kuunganisha hizo camera zako zote kwenda kwenye DVR - Kwa maana nyingine unakuwa na Closed Circuit TV - CCTV kwa ajili hiyo.

.

Mtu makini anaweza kukuambia ame-cover tukio kwa kusema idadi ya Camera alizotumia na Angle zilizowekwa. Kwa sababu hata bila DVR au CCTV ukiwa na Camera zako nyingi zenye DVD [Kifaa again cha kutunza] za kutosha na kama sio lazima kuona footage hapo kwenye tukio lenyewe huhitaji DVR au CCTV.

Kwa maana nyingi kitendo cha kwamba mnaongea kwa wiki sasa hamuongelei Camera za kuchukua matukio zilikuwa ngapi mnadanganyana tu.

Mfano mzuri. Kuwa na Latest DVR au na CCTV kwenye Harusi yako alafu usiwe na Camera... tuone kama utaambulia kitu...

Au uwe na Camera moja kwenye harusi yako... imeunganishwa kwenye latest worldclass DVR through CCTV alafu mpiga picha wako mwenye hiyo camera awe anapiga picha ndani ya hall/ukumbi alafu siku ya siku akuonyeshe picha za nje ya ukumbi wakati yeye muda wote alikuwa ndani ya ukumbi. Ati kwa sababu ya world class DVR au CCTV cabling.

Nilidhani niweke- Ukweli sawa.

"Mambo ya eti kutumia Satellite etc... Hauna maana yoyote..."

NB: Ukiwa na Latest DVR ku-review image footage za tukio ni suala la ku-click tu... muda gani? camera ipi? then you get everything huhitaji masaa, siku au ma-wiki.

Wapenzi wa Football au Wengine; Stadium zina CCTV system inayounganisha camera nyingi au zote zilizoko kwenye pembe mbalimbali za uwanja... kwenda kwenye DVR ku-record matukio yote... na mengine hata huyaoni kwenye TV yako, lakini ukitaka waweza onyeshwa almost kila kitu... Kwa sababu idadi ya picha zinazorikodiwa ziko sawa sawa na idadi ya Camera zilizoko uwanjani. Hivyo Stadiumu zina Cameras, CCTV na DVR pamoja ndizo zinakuletea football live... Wengine Mlishawahi kusikia kwamba kuna mtangazaji akitamka kuna camera 200 au x... kwenye stadium Q, meaning accuracy ya matukio yote inasababishwa na Idadi ya kubwa ya Camera zilizosimikwa kila kona ya Uwanja mpaka nje ya Uwanja... sio DVR. DVR ni kwa jili ukubwa wa kutunza matukio tu.

Meaning of DVR from Wikipedia.
A digital video recorder (DVR), sometimes referred to by the merchandising term personal video recorder (PVR), is a consumer electronics device or application software that records video in a digital format to a disk drive, USB flash drive, SD memory card or other local or networked mass storage device

Wateja wa DSTv wale wanaoweza ku-record program fulani na kucheki baadaye wanazo PVR.... recording events ambazo already zinaletwa na DSTv na kuangalia baadaye.

So DVR is something simple and not complicated like the way watu wanatoka mapovu navyo... na ukiwa na latest techonology DVR unaonyesha matukio instantly.

Mfano wa DVR ambazo wengine mnazo majumbani mwenu especially wateja wa DSTv.
dvr-system.jpg

Note: Thread hii ni ya kuelimisha tu, haiko kupinga au ku-support chochote kinachoendelea kwenye Thread Zingine. Huenda kwa elimu hii ndogo mwaweza kujadili kwa hakika mambo yenu yanayoendelea.

Nawatakia siku njema na Mukamwombe Mungu.
 
Sasa kulikua na kuna ulazima gn wa wewe kuanzisha thredi?
 
kuna mtu mmoja aliwahi kusema.....TUNAKAMATA MAJAMBAZI KWA KUTUMIA LAPTOP.......hamna tofauti sana na kelele za DVR
 
Kinacho nishangaza ni kuwa aliyetoa ushuhuda mpaka sasa ni mmoja tu, ushahidi kupitia hizo DVR. Sasa mleta uzi unaweza kutusaidia kujibu je kama unatumia DVR kurekodi, je watu wengine hawawezi kuona kwa macho ya kawaida tukio linalo rekodiwa? Kwa maana watu walikua ni wengi na bado sijasikia ushuhuda mwingine isipokua DVR tu.
 
kuna mtu mmoja aliwahi kusema.....TUNAKAMATA MAJAMBAZI KWA KUTUMIA LAPTOP.......hamna tofauti sana na kelele za DVR

In fact with proper software you can change/make any computer being desktop au laptop to be a DVR- Kivaa cha kutunzia picha zilizopigwa au zinazopigwa.... Swali zinapigwa na nini? So far till I write this bandiko picha zinapigwa na Camera sio na DVR.
 
Kinacho nishangaza ni kuwa aliyetoa ushuhuda mpaka sasa ni mmoja tu, ushahidi kupitia hizo DVR. Sasa mleta uzi unaweza kutusaidia kujibu je kama unatumia DVR kurekodi, je watu wengine hawawezi kuona kwa macho ya kawaida tukio linalo rekodiwa? Kwa maana watu walikua ni wengi na bado sijasikia ushuhuda mwingine isipokua DVR tu.
wanasema kinachosikia na kuona ni ubongo wako na sio masikio au macho.kama ume-tune ubongo wako kutokusikia na kuona kamwe huwezi kusikia waka kuona.
Jumapili njema.....!
 
WaTanzania tuna tabia ya Kudharauliana sana; Yaani kuonana mazoba... ati kwa sababu babu yangu kule kijijini hajui kitu fulani unaamua kumdanganya tu.... live....

Anyway; najibu maswali ya huo mfumo tu... Ya siasa ngoja niwaachie wanaoweza kudanganya wenzao live.
 
blah blah zoooote fanyeni ila mlipua bomu anajulikana nukta
 
kwa hio issue sio DVR ila kulikuwa na camera ngapi na wapiga picha wangapi
 
kwa hio issue sio DVR ila kulikuwa na camera ngapi na wapiga picha wangapi

Exactly this is the question I expected kutoka kwenye watu wenye akili zao... na sio tu Camera Ngapi bali zilizowekwa pia kwenye angle/corner ngapi za sehemu ya tukio...

Maana wapiga picha kumi wote wakielekeza camera zao kwa Bibi Harusi kwenye jukwaa pale Ukumbini! Huwezi kuniambia wakati huo hou utaona matukio ya kwenye chakula! Yet kwenye chakula hakuna Camera imeelekeza huko.

Angalizo: Ila kama mpiga Camera alikuwa standby ku-rekodi tukio fulani linalo/litakalotokea muda fulani... of course lazima alipate tena vizuri. Kama Wapiga picha wamejiandaa kupiga tukio la kukata keki definetely muda huo wote watakuwa tayari... Lakini again kinacholeta tukio ni Camera na Mpiga Picha... Sio Kompyuta (DVR) inayosubiri kutumiwa na Camera tukio lolote kutoka camera yoyote.
 
Cha msingi happo ni picha ziko wapi na sio zilitumika kamera ngapi
 
Kamera moja au kumi, DRV au D4, kinachotakiwa ni ushahidi bila chenga. Kwa mujibu wa makamanda, huo ushahidi upo. Ni suala la muda tu kila kitu kitajulikana.
 
DVR- Ni kifaa cha kutunzia picha za video ambazo zimepigwa na Camera Kwa matumizi ya baadaye mara nyingi zinatumika kwenye ulinzi kwa kuunganisha na Closed Circuit TV - CCTV. DVR yenyewe haipigi picha...

Kwa kifupi... mfumo wenyewe uko hivi....

1. Unahitaji Camera {moja au zaidi, nyingi na zilizowekwa kwenye pembe mbalimbali ndizo zina-guarantee fully coverage ya tukio}

sio lazima kuwa na camera kwenye angle mbali mbali, unakuwa na camera kwenye angle mbalimbali kulingana na camera unayotumia. mfano ni mkoa wa mwanza kuna camera moja imewekwa barabarani pale karibu na mwanza hotel lakini coverage yake ni kubwa na inachukua picha kama vile mtu yuko kwenye send off au harusi.

Mleta mada nenda mwanza na ukweli utaupata.

[h=1]Security CCTV Camera/Vehicle IR PTZ Camera/Waterproof Pan Tilt (J-VP-5106-L/R)[/h]

Product Description
High-intensity aluminum alloy, anti-impact, and anti-cauterization IP66 powerful spring and rubber system, suitable for the mobile environment multiple installations: Magnetic catch, bolt installation built-in temperature control circuit, all-weather environment design double window, camera match IR light, camera match thermal, or two camera proximate and teleradiography double lights, maximum optical range is 100m IR light can linkage camera and light, can be close by manual match with s3 series camera have 5 to 15Hz machine power anti-shake and auto-follow function.

Recommended: Police wagon, fire engine, and armor cash carrier special industry

Technical Specification:

Voltage: 12V DC
Power: ≤ 20W
Pan turn speed: 0.1 to 55° /second
Tilt turn speed: 0.1 to 40° /second
Pan turn scale: 360° Continuously
Tilt turn scale: -10 to 90°
Communication format: RS-485
Communication protocol: Pelco p or d
Band rate: 1, 200, 2, 400, 4, 800, and 9, 600
Address scale: 0 to 63
Suitable temperature: -30 to 55° C
IR wavelength: 850nm
IR half-power beam width: 30° (10, 25, 45, and 60° )
IR output power: 5, 000mw
IR useful life: 10, 000 hours
Shinning distance: More than 100m
Weight: 9.5kg
 
Kinacho nishangaza ni kuwa aliyetoa ushuhuda mpaka sasa ni mmoja tu, ushahidi kupitia hizo DVR. Sasa mleta uzi unaweza kutusaidia kujibu je kama unatumia DVR kurekodi, je watu wengine hawawezi kuona kwa macho ya kawaida tukio linalo rekodiwa? Kwa maana watu walikua ni wengi na bado sijasikia ushuhuda mwingine isipokua DVR tu.

are you alive or . . . .!
 
Security CCTV Camera/Vehicle IR PTZ Camera/Waterproof Pan Tilt (J-VP-5106-L/R)

Nataka watu kama ninyi muwasaidie WaTanzania wenzetu... maana lugha hizi zinatumika kuficha certain message.

1. Kwanza tuna/mekubaliana kwamba Lazima kuwe na Camera ili upate matukio... DVR yenyewe bila Camera ni hakuna kitu. So hoja ingekuwa Camera au image feeder kwenda kwenye DVR.

2. Ni kweli Camera zina record angle tofauti, kwa mfano hiyo ya kwako haiwezi kupata matukio ya 360 deg...at a time... in short hauwezi kupata kitu nyuma ya hiyo Camera. Ingawa unaweza tilt deferent angle by 360degree... yaani kuzungusha ingalie pande mbalia mbali., lakini wakati unatilk kwenda kusini... una miss kaskazini au Mashariki una miss Kusini.... Lazima ufanye tilt horizontally and vertically. Hivyo Camera moja... yaweza kupata tukio ambalo liko-upande ambayo iko-optimized. lakini sio matukio yote...at a time.
Kuhakikisha coverage makampuni ya Ulinzi ya combination ya Cameras... kuhakikisha wana-cover each angle wanayotaka ku-cover.

3. Na kuweza kupata coverage kubwa lazima hiyo Camera iwe eneo ambalo unaona kila kitu! Lakini kama hapo 2.... huwezi ku-cover everything with one camera.

Matumizi ya PTZ camera uliyoweka hapo juu ni kufuatilia mtu au tukio ambalo linaonekana au lishaonekana baadaa ya kugundulika kwenye camera zingine... hivyo security guards wanatumia PTZ kwa ajili ya kufualia kwa detail in short wanaweza ku-zoom,, kutilt horizontally na vertically kufuatilia hilo tukio haramu....... position ya PTZ camera ni muhimu sana kupata sehemu mbalimbali.

Mfano hiyo Camera ukiwa umeweka mbele ya Nyumba yako... haiwezi kuona Nyuma ya Nyumba yako. Labda uiweke juu zaidi hewani ndio itaona nyuma na mbele lakini pia haiwezi kuonyesha ndani ya nyumba.

In short mijadala mingi ingekuwa ya kuzungumzia Camera zaidi kuliko Kuzungumzia computer ya Kuhifadhi picha!

Finally... Technologia ya Kuchukua Picha iko Guided na "Theory za Light"; Ambako mpaka leo... Light inasafiri kwenye mstari ulionyooka. Light ikizuitwa na Mti, Mtu, Gari...Nyumba ndio imetoka hivyo.
 
Hebu tusubiri

Back
Top Bottom