Boniphace Bembele Ng'wita
JF-Expert Member
- Dec 25, 2013
- 3,446
- 1,812
Ni kwa nini UDA pekee wanaruhusiwa kupeleka abiria Posta kwa yale magari yanayotokea Temeke kuishia mnazi mmoja
Ndugu zangu najua hata nikisema hakitabadilika kitu lakini bora niseme ili nitoe lililopo moyoni mwangu. Hapa ninapoongea niko Mnazi mmoja naenda Feri lakini cha kusikitisha, hawa UDA wenye dhamana ya kutupeleka Feri wanaamua wao wanavyotaka.
Kilichonikera zaidi wanaamua kuishia posta alafu wakifika posta wanashusha na kupakia tena abiria wa ferry.
Maanake ni kwamba abiria kama unaenda Feri basi unalazimika kulipa nauli mara mbili ili ufike Feri. Wahusika mlioamua kutoa kazi hii kwa UDA basi ninaomba mlifuatilie hili ili kuondoa kero hii kwa maana wananchi mnatutwisha mzigo sana.
Fikiria mm naishi kitunda, nilizoea kupanda gari mbili + kivuko mpaka nafika kigamboni (kitunda- banana- kivuko) lakini sasa napanda magari manne (kitunda-banana-mnazi mmoja-posta-kivukoni-kivuko).
Kweli sisi masikini tutajikwamua?
Daladala kurejea Posta, Kivukoni
MAMLAKA ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imetangaza kurejesha safari za daladala kwenda Kivukoni mwishoni mwa mwezi huu. Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam juzi, Ofisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki, Conrad Shio, alisema daladala zote ambazo zilikuwa zimesitishwa kutoa huduma za usafiri zitaanza kufanya hivyo kutokana na ujenzi wa barabara kumalizika.
Shio alisema wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake ambao muda mrefu walikuwa wakipata adha ya usafiri, hususani waliokuwa wakienda Kigamboni, watakuwa wameepukana na adha hiyo.
Mamlaka hiyo ilisitisha daladala kutoa huduma za usafirishaji abiria wanaokwenda Posta na Kivukoni Septemba 30, mwaka jana, kabla ya kuja kuliruhusu Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) kutoa huduma maeneo hayo, hali iliyosababisha malalamiko kutoka kwa wamiliki wa daladala, wakidai shirika hilo linapendelewa na mamlaka hiyo.
CHANZO: TANZANIA DAIMA (13/07/2014)