Usafiri wa Makonda kwa walimu ni balaa tupu

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,906
2,885
Kama ilivyotarajiwa na wengi hali ilikua si hali hapo jana wakati waalimu wakianza wiki yao ya kusafiri bure kwenye daladala katika mkoa wa Dar ambapo wengi wao walijikuta wakitukanwa na wengine kulazimika kushushwa kwenye daladala huku wakitupiwa maneno ya kashfa kama vile " mnadhani tunaweka mate kwenye gari!?"

Huku wengine wakisema inabidi muonyeshe vitambulisho kabla ya kupanda ili tuwachukue wachache jambo lililopelekea wengine kuficha vitambulisho vyao na kulipa nauli kama kawaida.

Hata hivyo kuna waliosafiri bila usumbufu wowote na kumshukuru sana Makonda kwa wazo lake,huku wengine wakishndwa kuitumia fursa hiyo kwa kucheleweshewa vitambulisho vyao na wakuu wao wa kazi.

Chanzo: Uhuru fm
 
ii n dharau sana ata ao waalimu waliopokea ivo vitambulisho hawajielewi, haya sasa wanasema waoneshe vitambulisho ili wawachukue wachache
 
Hivi kweli ikitokea nusu gari walimu itakuaje? Bora wanajeshi uniform zinasaidia wanajuana na kupanda wachache
 
kama ilivyotarajiwa na wengi hali ilikua si hali hapo jana wakati waalimu wakianza wiki yao ya kusafiri bure kwenye daladala ktk mkoa wa dar ambapo wengi wao walijikuta wakitukanwa na wengine kulazimika kushushwa kwenye daladala huku wakitupiwa maneno ya kashfa kama vile " mnadhani tunaweka mate kwenye gari!?".

Weka haraka namba za magari yaliyowatendea hivyo walimu hapa na yanaenda njia ipi .Ili washughulikiwe haraka iwezekanavyo tafadhali.
 
kwa hiyo staili hili swala litakuwa gumu sana, wataishia kudhalilishwa tu,Ingekuwa vizuri wakapewa transport allowance na mwajiri wao then wenyewe watajipanga
Hii lin ni figisu ya kipuuzi mno ya kisiasa ndio maana hawawezi kupewa allowance kwakuwa wakipewa wa dar wa mikoani nao watataka
 
kwa hiyo staili hili swala litakuwa gumu sana, wataishia kudhalilishwa tu,Ingekuwa vizuri wakapewa transport allowance na mwajiri wao then wenyewe watajipanga


Wengi wanaodai posho za usafiri kwa utafiti wangui wanakaa karibu na maeneo ya shule wanataka pesa ya dezo au wana magari na usafiri wao.

Serikali na wamiliki wa daladala wameamua kuwasaidia wale wanaokaa mbali na shule.Kama unaona wanafaidi kupanda basi bure na wewe hamia mbali upande hayo mabasi bure.

Ninachokiomba hili jukwaa lisiwe kama la walevi mtu lete ushahidi wa kuanzia basi namba nk AMBALO LINANYANYASA watu.Chama cha makondakta na madereva wa daladala pia wametoa wito kuwa mwalimu yeyote atakaye nyanyaswa taarifa zifikishwe kwao pia chama cha wamiliki wa daladala nao wametoa wito huo huo wapelekewe taarifa za dreva au kondakta yeyote atakaye nyanyasa walimu.

Humu kuna watu wanaandika tu kwa ulevi tu wa siasa za kipinzani kuwa chochote kinachofanywa na serikali ni cha kupinga tu.
 
Hii lin ni figisu ya kipuuzi mno ya kisiasa ndio maana hawawezi kupewa allowance kwakuwa wakipewa wa dar wa mikoani nao watataka
Na Dar siyo wote ni Wilaya ya Kinondoni,sasa shule ipo Wilaya ya Temeke unakaa Kinondoni inakuwaje???Kazi hii wangu wangejadili kwenye halmashauri ili wajue namna ya kuwasaidia hao Walimu kwa Nauli hii ya vitambulisho mhhhhhhhhhhhhh!
 
Weka haraka namba za magari yaliyowatendea hivyo walimu hapa na yanaenda njia ipi .Ili washughulikiwe haraka iwezekanavyo tafadhali.

Washughulikiwe na nani wewe??...huu ni msaada wametoa kwa hiyo ni hiyari yao kuwapandisha au kutowapandisha,alichofanya Makonda ni kuwaombea lift Walimu kwa wamiliki wa daladala lakini hakuna sheria inayowalazimisha wawapandishe bure.
 
Back
Top Bottom