Usafiri Dar - Bagamoyo sasa kwa boti ya kasi

Usafiri Dar - Bagamoyo sasa kwa boti ya kasi

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
"itaanza kazi baada ya kuzinduliwa na JK".
kivuko+px.jpg

Kivuko kilichopewa jina la MV Dar es Salaam, kimeletwa nchini jana kutoka Bangladesh kikiwa cha kwanza kwa mwendokasi kuliko vingine vyote nchini. Kina uwezo wa kubeba watu 300 waliokaa pamoja na mizigo.


Dar es Salaam.Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam sasa wataanza kusafiri kwa kutumia kivuko cha kisasa kutoka katikati ya jiji hadi Bagamoyo na mikoa mingine badala ya kutumia usafiri wa barabara.
Kivuko hicho kilichopewa jina la MV Dar es Salaam, kimeletwa nchini jana kutoka Bangladesh kikiwa cha kwanza kwa mwendokasi kuliko vingine vyote nchini. Kina uwezo wa kubeba watu 300 waliokaa pamoja na mizigo.
Akizungumza katika hafla ya kupokea kivuko hicho kwenye Bandari ya Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuri alisema ujio wa kivuko hicho chenye thamani ya Sh7.9 bilioni ni mwanzo wa utatuzi wa kero ya foleni katika jiji hili.
Dk magufuli alisema kumekuwa na utegemezi mkubwa wa usafirishaji kwa njia ya barabara, jambo ambalo linasababisha foleni bila sababu ya msingi.
“Asilimia 99 ya mizigo husafirishwa kwa njia ya barabara, wakati asilimia moja tu ikisafirishwa kwa ndege, treni na meli. Hakuna haja ya kusafirisha makontena kwa njia ya barabara, tunahitaji usafiri wa treni kusafirisha makontena kutoka bandarini kwenda nje ya mji ili malori yakapakie huko,” alisema.
Alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza adha ya foleni, ambayo mara nyingi husababishwa na malori yanayobeba mizigo kutoka au kwenda bandarini, hasa katika Barabara za Mandela na Kilwa.
Waziri huyo alibainisha miradi mingine ya kupunguza foleni itakayotekelezwa jijini ni ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara eneo la Ubungo na Tazara. Pia, ujenzi wa Daraja la Kigamboni litakalokamilika Juni, mwakani na kugharimu Sh214 bilioni.
Alisema mradi mwingine wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT) utagharimu Sh288 bilioni na unatarajiwa kukamilika Machi, mwakani. Alibainisha kuwa bado ujenzi wa barabara za mzunguko unaendelea na kumtaka mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kudhibiti wafanyabiashara ndogondogo wanaoingilia hifadhi ya barabara na kusababisha foleni.
“Dar es Salaam inahitaji vivuko vingine vingi zaidi, tuna Sh3.7 bilioni kwa ajili ya kivuko kingine cha Dar es Salaam,” alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa), Mhandisi Marcellin Magesa alisema mradi wa ujenzi wa kivuko cha Dar es Salaam – Bagamoyo ulianzishwa na Serikali kupitia bajeti yake ya mwaka 2013/14.


Chanzo: Mwananchi.
 
Wamechelewa wangeleta wkt barabara mbovu

Tusiwahi kuwasifia, hawakawii kutuliza. Isije ikawa na Second Hand Kivukoni baada ya siku 2 hakifanyi kazi. Kama wamekula hela za ESCROW watazionea aibu hela zilizonunua kivuko? Kama kiko imara tunawapongeza
 
Na sasa Magufuli anataka kujenga Daraja toka Aga Khan Hospital mpaka mita ya Kona ya Masaki karibi na stanbic Bank pale hahahahahah kweli CHADEMA tumeshinda hii miradi ilikuwa ndoto tuu sasa wanahaha
 
Yani waziri huyu huyuanaleta kivuko,waziri huyu huyu tena anakuja na mradi wa kipande cha barabara kitachoishia coco. Najiuliza hivi hawa maawaziri hawakaagi chini pamoja yani hawana communication katika utendaji wao,waziri wa afya au wa elimu walikuwa wapi kumpinga huyu waziri mmoja ambaye kipaumbele kwa watz kilikuwa kivuko wangesema inatosha hiyo hela ya kipande cha barabara cha juu ya bahari wakakipinga na hiyo hela akapewa huyo waziri wa afya au elimu .
Kama tukipata usafiri wa kuwabeba watu hadi bagamoyo hatuhitaji barabara hiyo watu wa masaki hamkai kwenye foleni mda mrefu kama tunavyokaa watu tunaoenda msasani,morocco,kijitonyama,makumbusho,mwenge,mbezi beach,kawe,boko,bunju,tegeta.
mawaziri mjipange na miradi mnayoichagua kuipa vipaumbele
 
Katika karne hii kivuko kinakuwa na fan badala ya air condition. Hovyo kabisa!
 
watanzania wengi huwa tuna amin vitu katika picha .Basi tupia ka picha tafadhali
 
Kuna umuhimu gani kianzie bagamoyo na si sehemu yeyote ile?
 
Hasara tupu... kisa kummfurahisha profesa kuju
 
Mimi jamani haya ma VIVUKO na mimi ni tofauti kabisa, leo hii wanakisifia sana lakini ikitokea kimepata majanga ndo utaanza kusikia habari za kwamba kule kilipokuwa tayari kilishafungiwa kutoa huduma ya kubeba abiria kwa sababu ya uchakavu(ref,mv spice).
 
Tusiwahi kuwasifia, hawakawii kutuliza. Isije ikawa na Second Hand Kivukoni baada ya siku 2 hakifanyi kazi. Kama wamekula hela za ESCROW watazionea aibu hela zilizonunua kivuko? Kama kiko imara tunawapongeza

Magumash tu kama radar
 
Back
Top Bottom