whitehorse
JF-Expert Member
- Aug 29, 2009
- 2,570
- 4,455
Wana JF leo nimeshuhudia usafi kabambe unafanyika pale jengo la NHC Mtaa wa Samora. Jengo zuri maridhawa kabisa lakini limejengwa kwa vioo na kuna floor za vioo zinatazama barabarani.
Kwanza maji yanayomwagwa yanamiminikia barabarani na wapita njia na wenye magari yanamwagika hovyo usipogundua kama unapita kwa mguu unalowa na maji machafu na pia wale wafanya usafi sasa hawana vifaa vya kujizuia na hatari yoyote wafanyapo usafi. Wanapiga usafi kwenye floor imejengwa kwa kioo wanamwaga maji ya sabuni na hawana cha kujizuia wanapoanguka hivi NHC wanapotoa hizi tender za usafi wanazingatia viwango vya ubora au ndio dharau kwa wahudumu wa usafi?
OSHA mko wapi mnalala usingizi wa pono wakati haya yanatokea kwenye jiji kubwa kama hili ? Hivi huwa mnapita kwenye haya majengo na kuchungulia haya?
Mwisho wa siku wanaodondoka na kufariki ni wahudumu wasio na sauti wala pesa.
Kazi kwenu NHC na OSHA laleni na likitokea la hatari mtanyoosha maelezo kwenye makaratasi yenu ya maelezo kuwa hamkuwa na taarifa