leipzig
JF-Expert Member
- Jan 9, 2013
- 2,766
- 1,716
Mimi na mke wangu tumekuwa na mtazamo tofauti sana kuhusu usafi wa chumbani kwetu. Naona usafi wa chumba unaofanywa na mke wangu hauridhishi na hivyo nilimshauri mmoja wa wasichana wetu wa kazi afanye pia usafi wa chumbani.
Kwa bahati mbaya sana yeye hakubaliani kabisa na wazo hilo, anasema heshima yake kwa wasichana wa kazi itapungua. Nikumuuliza heshima yake itapungua kwa vipi anadai hataki binti wa kazi aone nguo zetu za ndani kitu ambacho mimi naona ni sababu ndogo sana.
Sasa nimeshindwa kusubiri nimeona nije hapa jukwaani nisikize ushauri wenu, malezi yangu kwa baba na mama yangu yalikuwa binti wa kazi anafanya usafi pia chumbani kwa mama na baba.
Nawasilisha!