USA yaendelea kuichimba Tanzania

USA yaendelea kuichimba Tanzania

Mi nilivoelewa ni kuwa america wanataka kutuingizia vikundi vya kigaidi ili kuidhoofisha serekali iliyopo!!kwa nongwa ya kunyimwa fursa za uwekezaji nchini!!!
 
''Msiwe na shaka, tutavuka salama vikundi vya kigaidi havina nafasi hapa''- Mjomba Fujo 9-2-2020.

Watakao kuwa hai baada ya miaka 5-10 mtarejea hii comment yangu kama hakikisho la usalama kwa Watanzania bila kujali dini zao.
 
Mungu atatunusuru na hili. Mimi nahisi tatizo lao kubwa hawa jamaa juu ya hii issue mi kutaka sisi tutowe majeshi yaende Somalia. Kenya na allies wengine naona washachoka kupokea masanduku ya maiti. Hawa vichaa Alshabab na Alqaeeda tuwaachie kama walivyo. Lakini kwa dalili hizi nahisi kama hawa jamaa wanataka kutuletea zengwe kiaina!

Mimi siamini kama Waislam Tanzania kuwa wako institutionally radicalised. Wako tu individuals ambao wataendelea kuexist duniani kote kutoka kila dini. Suala la Bakwata ni kuwa kuna wasema kweli kina Shehe Ponda ambaye yuko vocalist rather than radicalised na naamini anayo right ya kujieleza.
Umeandika ninachowaza.

Hawa watu roho zinawauma saana kuona majirani zetu wanasumbuliwa na vikundi vya kigaidi lakini sisi tupo ahueni kama sio salama.

Walitaka tushiriki kusaidia. Na tusijindanganye tukawaamini hawa jirani zetu wayasemayo wakutanapo na wakubwa hatuyajui. Juzi Fox wanasema Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kuwa na vijana wengi kuliko nchi yoyote Al-shaabab, hadi unajiuliza inamaana tumewapita hata wasomali?

Trump raia wao waliuliwa juzi na Al-shaabab..hawezi kupenda hili hata siku moja. Ni sawa na jirani mwenye misukosuko na aliye na amani..utatafutiwa visababu tu
 
Watu wanaowekeza kwenye elimu ndani ya jamii zao sio wapuuzi it’s part of national security pia. Kwa sababu wanajua madhara ya ignorance haswa kwenye urahisi wa kuchota akili za raia mbumbumbu.

Mtu kiazi kama Musiba iwapo ni sehemu ya usalama wa taifa anahitaji an intelligent handler mwenye kujua chombo chake kitarusha nini sio kila habari ya kuipa publicity; vitu vingine kutoka nje wacha serikari ikabiliane navyo au independent media kama wakizipata hila sio vyombo rafiki vya serikari kuvileta haswa habari zenye elements za ‘sensationalism’ kwa kufanya ivyo sana sana unamsaidia huyo mwenye lengo ya kuichafua nchi maana wewe ndio unamsaidia kufikisha ujumbe wake.

Halafu hiyo report ni ya kimataifa aija ripotiwa na western media tu bali vyombo vya kimataifa hata TV ya China imeripoti.

Na wala central to it sio Tanzania per se bali wapiganaji wa Al-Shabab ambapo if anything Tanzania inaonywa kuna terrorism recruiting cells ndani ya mipaka yake wanaosaidia icho kikundi na vijana wengi wamejiunga.

Hila sasa ukisoma michango ya wasomi wa JF khaa, it is as hao watu wanashambulia Tanzania.




Habari hiyo hapo hata vyombo vya China vimeripoti, sio kila kitu anachopewa Musiba ni kuisaidia Tanzania bali vingine ni kuwapa wahusika publicity wanayoitaka through sensationalism ya utoaji wake wa habari.

Watu wakisema ‘intelligence services’ ujue they mean as the definition implies ni mchezo wa vipanga sio kuokota watu ovyo ovyo mtu ajiulizi ata lengo ya source zake.
 
Kudeal na mabeberu hasa huyu beberu mkuu kunataka akili ya zaidi sana..

Ukisoma vizuri na ukawa unayajua matendo ya USA basi utagundua tayari ameshaunda kundi lingine la kigaidi Tanzania. Anachofanya sasa ni kutuandaa kisaikolojia ili kazi iendelee, tayari ana namna mbili za kuidestabilize Tanzania kupitia dini na siasa na target yake ni mikoa ya kusini na soon utasikia wakusini wanataka Taifa lao..
Na anaenda kufanikiwa kwenye hili...angalia hapa JF...tumeisahau Marekani tunamtetea kwa kila jambo kana kwamba yeye ni malaika.
 
samurai,
Ila hapa wanatuonea sisi wananchi wa chini.

Kwa nini wasimdungue jiwe moja kwa moja na sisi wananchi tutashangilia sana
Lengo unadhani ni kutusaidia sisi wananchi wa chini?

Jiulize kama walitaka kuwasaidia wananchi wa chini wanakandamiza uhuru wa habari huwa wanacheza lottery yao? Kufungwa kwa Green Lottery kutamuathiri vipi aliyekandamiza uhuru...!

Zimbabwe kuwekewa vikwazo nani leo anataabika? Mugabe familia yake inakula na kuishi vizuri wanakufa kwa njaa wazimbabwe tena wale wa chini.
 
Marekani sio watu wazuri.
I mean administration sio wamarekani Kama raia
 
Well said.

Marekani hana rafiki au adui wa kudumu. Wao wanachojali ni maslahi yao tu.

"You are either with us or you're against us".

Umri umenifundisha kuelewa, ili USA asikuzonge zonge inabidi umpe chochote akitakacho kwa masharti yake.

Lazima umpe vipaumbele katika miradi yako mikubwa na usimzuie na usimbadilishie masharti anayoyataka yeye anapotaka kuwekeza miradi yake mikubwa nchini kwako.

Major export ya USA ni Vita na machafuko Kwa faida yake.

Kubali tu akule, hapo utakuwa salama milele na atakulinda, kinyume na hayo, umeenda na maji!
Acha uwoga.
hatuwezi kuishi kwa kuogopa marekani wala taifa lolote lile.
 
Hii habari imenifanya nifikirie sana, hawa USA wanataka kuanzisha au wameshaanzisha chokochoko za kutuchafua Tanzania?

Ukiitazama hii habari, ukiitazama habari ya aliyechana Qur'an, ukija kusoma nyuzi za anaejiita Mcqueenen hapa JF. Ukifikiri ya Makonda kunyimwa visa, ukifikiri ya Watanzania kuondolewa kwenye bahati nasibu ya green card, ukifikiri ya World Bank, ukifikiri ya msaada wa silaha kutoka USA, ukifikiri ya Tanzania kutangazwa siyo salama sana kwa utalii.

Kwa yote hayo unaweza kuunganisha dots na kukuta tayari limeshapikwa na linangoja kupakuliwa tu.

Allah tulinde na wenye kutia wasiwasi kwenye nyoyo za watu. Allah tuepushe na shari na hassad zote, tunazoziona na tusizoziona.

Haya si madogo kwa kiwango chochote kile, inabidi serikali, wasio na dini na wenye dini, tuwe macho na kuwa na subira na tusifanye pupa kwa hizi fitna zinazoendelea.

Tusikubali kuchonganishwa.
Kama sisi wenyewe hatutendeani haki hakuna namna ambayo tunaweza kushinda, tuwe na muafaka wa kitaifa kwanza ili adui akose pa kupenya,tazama Zamzibar wanataka kutunga sheria kandamizi kabla ya uchaguzi unategemea watakusikiliza jamaa wakiingia?
 
Jamestown wametoa. tahadhari ni jukumu letu kufanyia kazi, kws ss tunaoishi mazingira ya uswahilini, mtoni kwa Aziz Ali, tandika, mtoni mtongani, mbagala, mapipa, manzese nk maneno mfumo Kristo, na lugha za kukata tamaa ya maisha miongoni mwetu sio mageni, kwamba kuna watz wameshakamtwa na kushtakiwa akahukumiwa kifungo yupo, ss tusiwalaumu whistleblowers, ila tusiache kujiuliza nia ya hii tanzanite TV in nn? .......ni kumsafisha bw Mkubwa tu! kwa kutangaza uzalendo feki! na kutafuta kuonewa huruma. Ukiangalia vizuri bw mkubwa ameleta mgawanyiko mkubwa kwa siasa zake za kibaguzi, ss hivi juna wao wenyenchi na ss wakubambikiwa kesi za ugsidi, uhujumu uchumi na utakasishaji pesa, nionavyo kama waamerica wakija kutupiga mabomu wapo watakao ungana nao na wala hao sio wasaliti watakua wapigania uhuru!
 
Lengo unadhani ni kutusaidia sisi wananchi wa chini?

Jiulize kama walitaka kuwasaidia wananchi wa chini wanakandamiza uhuru wa habari huwa wanacheza lottery yao? Kufungwa kwa Green Lottery kutamuathiri vipi aliyekandamiza uhuru...!

Zimbabwe kuwekewa vikwazo nani leo anataabika? Mugabe familia yake inakula na kuishi vizuri wanakufa kwa njaa wazimbabwe tena wale wa chini.
Wamefunga lottery kwa sababu Serikali. Inaficha data hasa za magonjwa ya mlipuko.

Kwa hio Marekani anachokiogopa na ni sera yake, hawezi kuwapa watu visa wanaotoka kwenye nchi yenye ebola lakini taarifa zake zinafichwa
 
Wakijilipua kwenye mikutano ya ccm Ni poa tu. Maana ndio tunaosikia kuwa mikutano yao inaruhusiwa na jeshi la police.

Vyama vingine hawaruhusiwi. Mm naona wakianza kujilipua ili wajilipuaji wafanikiwe Ni kwenda kwenye mikutano hiyo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu inaonekana kana kwamba wana chuki na ccm hao tayari.
 
Back
Top Bottom