USA kuishambulia Iran karibuni

USA kuishambulia Iran karibuni

Hakutegemea kama Iran wangethubutu kufanya waliyofanya!!!!!!
Wafuatiliaji wa mjadala huu nawakumbusha kuwa 'hiyo' drone iliyodunguliwa ni ya anga za juu (high altitude drone), haionekani kirahisi (stealth), pia nyongeza ya hapo ni kwa drone hiyo ilizima transponders zake ili isishutukiwe kunyata kwake. Kwa maneno mengine ilikuwa na 'three levels of protection'. Muiran kupitia ulinzi wake wa Anga amevunja levels zote tatu na 'kuishusha' drone ya US.
Narudia ninawakumbusha tu wana jukwaa.
 
Mi ndo nakwambia, hakuna cha vita. Watu wameshaona Marekani anaogopa vita. Wakisema waingie vitani Iran itaangamia sana. Iran anataka kujifanya kama Korea kaskazini tu.
Kwanini sasa Marekani inaogopa vita?,hahah
 
Kamulize Natanyahau drone yake iluangushwa au haikuangushwa alipo enda anga la Iran, au Natanyahu kasahau.

Hebu tazama aibu hi sijui Trump ataificha wapi.


Siri ya Trump kuzia leo mashambuli ni sababu Pilot aliye kuwa kiongozi wa zile fleet za F16 kuona Raddar Jamming system inamuonyesha kuwa Radar ya Iran hajawezia kuijam ni power full na yeye option zake ni ndogo aingie kichwa kichwa au vipi. Ndio hapa control room wakabidi wawaulize pentagoni,wa go fwd au wasubiri kwanza. Trump akaona bora asisogeze pua.
Teh teh teh kweli mnajua kujitekenya na kucheka wenyewe.
 
Najilipia mwenyewe kwa jasho langu.
Ohoo kumbe hujui mkuu hiyo unayolipa wewe ni kwa nafasi yako tu sehemu kubwa washalipa serikali na donors wakubwa. Muulize mtu alie nchi zilizoendelea amabako hakuna donors jinsi medical services zilivo ghali.
 
Kwa taarifa yako Marekani huwa hapigi mahali ambapo jamaa wana uwezo wa kurudishia!!!!!! Ndege yao ya kijeshi isiyo na ruban " US Navy MQ-4C Triton drone" waliyoituma kufanya ujasusi juu ya Iran "haikurudi"!!!!! Na hii ni vresion mpya kabisa yenye dhana za kujificha isionekane na dhana za kijilinda isidunguliwe lakini saa hii imebaki majivu!!!!! Mtasubiri sana Marekani kujitutumua kwa Iran!!!!! Aendelee kumwonea Mchina kwa kukatisha kwenye bahari ya china na mimeli yake!!!! Wairan hawajui kubeep!!!! wao ni kupiga tu ukujichanganya kwenye anga zao!!!!! Tukio hili limemwogopesha sana Marekani!!!!! Hakutegemea kama Iran wangethubutu kufanya waliyofanya!!!!!!
Kuna wakati utapotea kabisa humu yaani utaingia kabisa mitini. It's only a matter of time.
 
Teh teh teh kweli mnajua kujitekenya na kucheka wenyewe.
Wakati drone hiyo inashambuliwa, kulikuwa na ndege nyingine ya kiuchunguzi ilikuwa ikiifuatilia drone hiyo, ndege hiyo ilikuwa na askari kama 35 wa US. Iran ingeweza kuitungua ndege hiyo...ila kiubinadamu ikaona iwape onyo wa US kwa kudondosha drone yao. Iran wanajua wanachokifanya.

 
Hahaha Saudia mbona wanajitafutia balaa hawaoni kuwa --USA atasababisha ardhi yao igeuzwe kuwa tanuri la moto
Mheshimiwa maarufu, "Mujtahid," katika Twitter yake vyanzo vya kunukuu vilivyoelezewa na Wizara ya Ulinzi ya Saudi, alisema kuwa Marekani sasa imewaomba Saud Arabia kuandaa maeneo ya kijeshi ya Saudi kutumikia Amerika katika mapambano ya karibu.

Inasemekana USA atashambulia Iran kama sehemu tatu hivi sababu Trump anaruhusiwa kutokana na sheria afanye mashambulizi kiasi kama hakuruhusiwa na congess kwenda vitani, na Iran akijibu hapo ndio itabidi congress wampe Trump green light aingie katika vita kamili na hicho ndio Trump, Natanyahu, MBZ na MBS wanakitaka.

Vita vinakuja katika hizi siku au hii week, kutokana na huyo Mheshimiwa maarufu Mujitahidi, na mara nyingi habari zake huwa za kweli haswa katika habari za Royal family za Saudia na inasemekana ni one of Saudi Royal Family.
 
Marekani sidhani kama ataingia kwenye vita na Iran hizo zitakua mbwembwe tu ila anajua uwezo wa kijeshi wa Iran kwamba sio wa kubezwa. Nadhani pia atafikiria kuhusu kuyumba kiuchumi akiwa vitani wakati huo mshindani wake kiuchumi China atakua anazidi kupepea wakati yeye anapigana vita.
Yaani mimi nasubiri apigane vita. .mchina azidi kupaa kiuchumi ''Russia nao hawato kuwa nyuma kuuza siraha kwa muajemi. ..hili picha Kali sana
 
Hahaha eti bahati mbaya. ..Aliye paswa kusema bahati mbaya ni aliye pigwa au mpigaji. ..!? Hii kali ha haa
Wale wa Persian wana akili kama mchwa. Tena kwenye Sayansi ya Nuclear na atoms usiwachezee kabisa. Trump mwenyewe kasanda alitanganza kwa mbwembwe kuwa watakiona cha moto. Mbona sasa kabadili uamuzi kuwa hatafanya chochote kuwa ilikuwa bahati mbaya. Iran wamemjibu haikuwa bahati mbaya. Iran is not Iraq,not Afghanistan.
 
Venezuela tu kataifa kadogo. .kamemtoa kamasi ndio atawaweza waajemi. ... wale Persian sio watu wa mchezo mchezo. .kama anaweza kweli atie maguu tuone
Unatarajia USA atampapasapapasa na vibom vya kuteleza?! Atamtandika mpaka dunia imuombee poh!
Shock and owe! Ndicho kinafuata.
 
Una zungumzia habari za Jana nilikula Makange. Sisi tunaongelea wakati huu uliopo. ...atie maguu Iran tuone
Japan alivyoonyesha ukichwa ngumu kwenye vita wamarekani walimtandika Atomic Bom.
Iran iko kwenye level ya utafiti wa ma Nuke, USA anayamiliki bila kudhibitiwa na yeyote halafu uhatarishe usalama wa NEW YORK wakuangalie!!? Kwani minyuklia yao wameitengeneza ya maonyesho!!?

WAIRAN wanadhani wanajitambua.
 
Hahaha Saudia mbona wanajitafutia balaa hawaoni kuwa --USA atasababisha ardhi yao igeuzwe kuwa tanuri la moto
Yule Crown Prince wa Saudia ni mdogo kisiasa bado, angekuwa na akili asinge washambulia wa Yemen nchi masikini.

Trump kaja wakati mzuri baba yake yule crown prince ana ugonjwa wa zahamier yani mfalme ba mwanae hawajui chochote zaidi ya kununua silaha hata kuzitumia hawajui.
 
Marekani sidhani kama ataingia kwenye vita na Iran hizo zitakua mbwembwe tu ila anajua uwezo wa kijeshi wa Iran kwamba sio wa kubezwa. Nadhani pia atafikiria kuhusu kuyumba kiuchumi akiwa vitani wakati huo mshindani wake kiuchumi China atakua anazidi kupepea wakati yeye anapigana vita.
Hakuna shughuli ya kiuchumi yenye faida kubwa kuliko vita, litambue hilo kwa leo.
 
Back
Top Bottom