Wewe jamaa unanichekeshaga sana aisee.
Siku zote unapozungumzia Demokrasia na mambo kama Haki za Binadamu inabidi wazo kubwa kuja kichwani kwako ni Ulinzi wa Haki za Raia dhidi ya Dola (Protection of Human Rights and Values from Arbitrary State Action). Halafu pili Ulinzi wa Haki za Raia dhidi ya Raia Mwingine: Lugha ya kisheria inasema Horizontal and Vertical Protection of Human Rights and Human Value. Hivyo ili kuangalia kama Demokrasia ipo au haipo kwenye nchi fulani lazima uangalie hivyo vitu viwili.Haya sasa kwenye ishu ya Kanye West hebu tujaribu kutumia haya majaribio mawili:
1. Vertical Protection of Human Rights (Protection of Human Rights against Arbitrary State Action)
Kanye West kasema kofia yake inasema Make America Great Again na kawaponda watu weusi kwa tabia yao ya kujifanya wao ndiyo Wahanga wakubwa wa Ubaguzi na hawataki kubadilika. Hajafanya kosa lolote lile na wala hajavunja Sheria za nchi, hapa Dola lina jukumu la Kumlinda. Haya katika hili la kwanza Kanye West hajagombana na Serikali na hakuna wakala yoyote wa Serikali anayemshambulia kwa kusema kile anachokiamini.
2. Horizontal Protection of Human Rights (Protection of one citizen against illegal interference by another citizen)
Hapa mtu moja analindwa kutoka kwa mtu mwingine, ili haki zake za msingi ziheshimiwe. Hivyo basi asitukanwe, asishambuliwe, asiibiwe na wala kufanywa chochote kile kibaya. Umetoa mfano kwamba watu wanamshambulia Kanye West kwa kukaa karibu na Rais Donald Trump lakini umesahau kwamba wanachokifanya siyo kinyume cha sheria "Freedom of Expression", Kukataa kununua Muziki wake nalo siyo kosa kisheria kwasababu hawana wajibu huo na siyo lazima ninunue Muziki wa Kanye West "Freedom of Choice). Hivyo kwenye demokrasia ndiyo inafanya kazi hivi, pale unapoengea tegemea kupingwa tu: Democracy is a like a Pendulum Bob it goes back and forth ad infinitum .
NB: Hivyo ndugu Barbarosa unaposema nchi haina demokrasia ni lazima uyaangalie haya mambo mawili kwanza halafu ndiyo uje kulia-lia hapa. Kitu kikubwa katika kupima uwepo wa Demokrasia ni SHERIA au LEGALITY OF SUBJECT MATTER hivyo kama sheria hazijavunja haki za Raia wewe unatoa wapi nguvu ya kusema Marekani hakuna Demokrasia ???