US $ vs TSh.

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
Leo jambo hili nalirudia hapa kwa mara ya pili. Hapa Golden Plaza "joint venture " wa NHC anatufanyia maajabu. anatutoza Huduma za umeme wa TANESCO, maji ya kisima chumvi tupu na walinzi wasio hata na redio kwa fedha za kimarekani. Tufanyeje ili sheria ichukue mkondo kwani si haki kutoza huduma hizi kwa $. Mbaya sana kasahinisha watu mkataba unaoonyesha kuwa huduma zi ktk $ japo kisheria kumbe ni mtanzania mwenzetu! TUSAIDIENI fisadi huyu tumtie hatiani. Kwani kodi ya NHC tunailipa kwa Tshs.
 
Ndio utumwa huo katika nchi yako mwenyewe. Ukiwaambia wenye madaraka ya kuchukua hatua hawatafanya chochote halafu na sisi tunajidai ati tuna serikali, serikali gani hii kama sio Majambazi na wezi?
 
Kwani si serikali ilishaagiza ndani ya jamhuri malipo yawe kwa tsh? Au ilibatilisha?
 
Kwa kweli mimi nakereheka nchi yetu tuafanya biashara kwa kutumia fedha za kigeni! Serikali inafanya nini? Kwa mtindo huu fedha yetu itakuwa na thamani kweli? Kwa kweli inasikitisha.neda hapo kenya na vidola vyako kama watakuelewa!
 
huu umekua wimbo lakini cha kushangaza serikali imetulia tuli....Nyumba, Gari, Kodi, hoteli, huduma, mpaka wafanya kazi za ndani watalipwa kwa $$$.. Tutavumilia mpaka lini jamani??:A S 13:
 
Back
Top Bottom