Mkuu DotWorld samahani nilikuwa offline kidogo, mkuu nikweleze kitu: majibu ya baadhi ya members yanaonyesha wazi wazi uelewa wao katika nyanja za Geopolitics ni borderline kabisa - hapa watu tunaelemishana na kubadirishana mawazo - wengi wao ukichunguza majibu yao ni kwa ajili ya kubishana na kugeuza ukweli kuwa Uongo, ukijaribu kuwapa facts and figures wanakwambia majibu hayo umeyapata kutoka kwenye search engines in other words huna akili za kuona mbali!!!
Hapa chini ntajaribu kujibu hoja zako ingawa zilikuwa zinaelekezwa kwa member mwingine, lakini nimeona na mimi nichangie kidogo kwa yale ninayo yajua ili members tuwekane sana katika masuala yanayo husu usalama wa Dunia yetu.
Mkuu DotWorld hawajui kwamba mchochezi mkubwa wa vita kati ya Iran na Iraq alikuwa ni Merikani, walifanya hivyo kilipiza kisasi:
kwanza:
Kutokana na Iran kumuondoa madarakani
Shah Reza Palvi ambaye alikuwa puppet mkubwa wa US Govt, si hilo tu makampuni makubwa ya Merikani/Uingereza yalikuwa yamewekeza IRAN hasa hasa sekta ya mafuta na gesi na kuhuzia silaha karibu zote zilizokuwa zinatumiwa na jeshi la IRAN - IRAN iligehuzwa shamba la Bibi na makampuni haya ya magharibi!
Wairan na Ayattola Khomeni aliyekuwa huamishoni huko Ufaransa wakaona they've had enough za jamaa hawa, wakafanya mpango kabambe wakafanikiwa kuwazidi kete American Govt na Anglo-Amerikani Companies , Shah akajikuta anatimkia uhamishoni na ndio ukuwa mwisho wake na makampuni aliyokuwa ameyakaribisha kuwekeza IRAN.
Pili:
Kutekwa nyara Wanadiplomasia wakiwemo wafanyakazi ndani ya jumba la Ubalozi wa Merikani huko Iran, walishikiliwa mateka ndani ya Balozi karibu kwa kipindi cha mwaka mzima, Rais Carter aliwahi kujaribu ku-rescue mateka hao under Operation Eagle Claw lakini jaribio hilo lilishindwa baada ya main rotor ya Helicopter kugonga Verticle Stabilizer ya ndege ya kijeshi ya mizigo iliyo sheheni mafuta wakati walipo kuwa wametua jangwani kijipanga jinsi ya kuvamia Ubalozi, katika ajali hiyo wanajeshi wanane walipoteza uhai wao hivyo Operation nzima ikawa aborted - mateka walikuja kuwa-freed wakati wa utawala wa Reagan na inasemekana wakati wa kampeini Reagan alimuomba Ruhollah Khomeini hasiwachilie mateka ili Reagan apate kete ya kumshinda Cartert kirahisi kwa kumshindiria kwa raia kwamba rais Carter ni mwoga ndio maana alishindwa kuwaokoa mateka huko IRAN, Reagan alifanikiwa sana kumdhoofisha mwenzake na kushinda Urais kiulaani -ndio michezo ya siasa ilivyo.
Who created Saddam Hussein:
Hapa namaanisha wanadamu sio
his MAKER, Saddam alikuwa rafiki mkubwa wa Administration ya US Govt especially Ramsfield wakati wa enzi za Reagan vile vile Ramsfield ndiye alim-recruit Chenny akiwa kijana mdogo tu na kumfundisha mambo ya ukatili na kiburi kapewa kazi kwenye ofisi ya Ramsfield wakati wa utawala wa Reagan au Bush Sr sikumbuki vizuri - je katika utawala wa Bush Jr Dunia ilishuhudia nini kwenye mixed grill ya Ramsfield, Chenny, Conddi Rice na Bush Jr? Si walikuwa ma Monsters tu hawa - imagine familia ya Bush na ma-bedfellows wake bila aibu wanaleta vita mara ya pili mashariki ya kati eti anataka kumuondoa Saddam Hussein kwa kuwa alijaribu kumuua Baba yake huko Kuwait - visingizio tu! Nilimsikia kwa masikio yangu akisema "Saddam Husein wanted to kill my father" ndio maana alihamuru wamunyonge kwa kamba kulipiza kisasi, anafanya u-barbalism huku akijifanya ni Mkristo kwa kwenda kanisani kila J2.
Tukirudi kwenye mada kuhusu Saladin a.k.a Saddam Hussein - Ramsfield ndiye alifundisha wataalamu wa Iraq kutengeneza Chemical/Biological bombs ili wahangamize Wairan, Wamerikani ndio walikuwa wanatumia Satellite zao ku-monitor mwenendo wa majeshi ya IRAN alafu wanampa taarifa hizo Saddam na jeshi lake ili makombora na ndege za kijeshi zilenge sehemu ambazo jeshi la Iran limejichimbia, si hilo tu Wamerikani walikwenda mbali zaidi kwa kushauri jeshi la Iraq liwashe majenerator ya umeme waweke live wires kwenye Marshes ili wanajeshi wa IRAN wawe electrocuted kwa wingi!!
Kibaya zaidi kinahusu mbinu chafu za jamaa hawa kumlaghai Saddam Hussein avamie Kuwait, archtect/Engineer wa njama hizo alikuwa ni Margret Thatcher kwa kibali cha Merikani - ni hivi: Wamerikani na Waingereza pamoja na Israel waliogopa sana influence/ushawishi wa Saddam katika nchi za Kiarabu vile vile waliona anajimarisha sana kijeshi pamoja na masuala ya utafiti wa kisayansi na kupendekeza kwake kwamba dhahabu ziwe zinatumuka badala ya dollars nk - nchi za magharibi zikamuona Hussein amehanza kuwa tishio kwa maslahi yao, sasa nini kilicho fatia - Thatcher siku moja kampigia simu Saddam na kumkumbusha kwamba actually IRAQ ilikuwa ni nchi moja hapakuwepo Taifa linalojulikania kama Kuwait sisi Waingereza ndio tuli-buni Taifa la kuwait wakati wa Ukoloni kwa lengo maalumu hatukutaka utajiri wa mafuta ubaki ndini ya IRAQ peke yake, sasa kwa kuwa hivi sasa una mgogoro na Kuwait wanaonekana wanawaibia mafuta kwa kuchimba chini kwa chini wanavuka mipaka na kuawibia mafuta - Bwana Saddam unaonaje ukirudisha Kanchi ka Kuwait kwenye greater Iraq kama ilivyo kuwa zamani, we fanya hima u-annex Kuwait sisi na Merikani tutakuhunga mkono!! Saddam ndivyo alivyo ingizwa mkenge - baada ya Hussein kutekeleza ushauri wa Thatcher Uingereza ndio ikawa Taifa la kwanza kumlahumu Saddam Hussein, kumbe Margret na Merikani walikuwa wanamtega Hussein ili wapate sababu ya aidha kumuondoa madarakani au kudhoofisha jeshi lake na influence aliyo kuwa nayo Mashariki ya kati.
Well said mkuu lengo lao ndilo hilo hasa! It is saddening indeed!
Splendid indeed DotWorld, vitu hivi havifundishwi shuleni - cha muhimu hapa ni kuwa endowed na a-mega smart analytical mind na kuwa mkweli bila ya ku-entertain ushabiki husio na tija, taifa lolote linalo leta wasi wasi karibu Dunia nzima litajwe na kukemewa bila ya kuogopa ushawishi wao wa kifedha na ujuma zao za kudumaza mataifa mengine kwa maslahi yao yasio na utu.