Urusi yaendelea kuchukua udhibiti wa maeneo ya Ukraine

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Vikosi vya Urusi vimechukua udhibiti wa kijiji cha kwanza mashariki mwa Ukraine katika mkoa wa Dnipropetrovsk.
Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi pamoja na wanablogu wanaofuatilia vita hivyo.

Hata hivyo taarifa hiyo haijathibitishwa na vyanzo kutoka Ukraine wala Wizara ya Ulinzi ya Urusi. Mara kadhaa Urusi imekuwa ikitaja kuwa tayari kusaini mkataba wa amani lakini ikiitaka Ukraine kujiondoa kikamilifu katika mikoa minne ambayo Urusi iliinyakua kinyume cha sheria.

Hayo yanajiri wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul amewasili hivi leo mjini Kyiv katika ziara ambayo haijatangazwa na yenye lengo la kudhihirisha kuwa Ujerumani inaendelea kuunga mkono mapambano ya Ukraine.

Wadephul anatarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha.
 
Hali mbaya sana Kwa Ukraine,

Na jinsi anavochelewa kusurrender

Ndo Anazid kukiuka makubaliano yake ya madini na trump,

Maana walishakubaliana na trump, deni la vita litalipwa Kwa madini yote ya Ukraine,

Na Kama mjuavyo, mashariki ndo Kuna zaid ya 70% ya madini yote Ukraine,

Sasa mashariki yenyewe ndo hiyo, Putin keshachukua mikoa 4, sahivi anafukuzia kufikisha 6.

Na Putin keshasema kabisa, ahusiki na makubaliano yake na trump, Hata vita iliisha leo, mikoa aliyochukua hairudishi, Nae ataitumia kujilipa gharama zake za vita.

Sasa sidhan kama trump atakubali kulipwa makinikia badala ya madini ya kule magharibi.

Naiona Tena Ukraine ikienda kusainishwa dili jingine Washington, sioni trump akimshuritisha Putin aachie mikoa 6 anayoishilia Kwa Sasa, kisa mikataba wake na Zelensky.

Yetu macho
 
Kosa kubwa wa Ukrane ni kuchagua uyo Zalensky toka lini mtu akapigana kwa Silaha za misaada !!

tena kichekesho unapambana na Russia !!!

tumeona na Netanyahu kataka kupigana na Iran sawa lkn mwisho mwenye Silaha zake kaamua yeye kumaliza Vita !!!

Ukinibishia sawa lkn Utapigana na mawe na ma Boom. Ya petrol mi sikupi silaha zangu..
 
Hali mbaya sana Kwa Ukraine,

Na jinsi anavochelewa kusurrender

Ndo Anazid kukiuka makubaliano yake ya madini na trump,

Maana walishakubaliana na trump, deni la vita litalipwa Kwa madini yote ya Ukraine,

Na Kama mjuavyo, mashariki ndo Kuna zaid ya 70% ya madini yote Ukraine,

Sasa mashariki yenyewe ndo hiyo, Putin keshachukua mikoa 4, sahivi anafukuzia kufikisha 6.

Na Putin keshasema kabisa, ahusiki na makubaliano yake na trump, Hata vita iliisha leo, mikoa aliyochukua hairudishi, Nae ataitumia kujilipa gharama zake za vita.

Sasa sidhan kama trump atakubali kulipwa makinikia badala ya madini ya kule magharibi.

Naiona Tena Ukraine ikienda kusainishwa dili jingine Washington, sioni trump akimshuritisha Putin aachie mikoa 6 anayoishilia Kwa Sasa, kisa mikataba wake na Zelensky.

Yetu macho
Duh,yaani madini yote yafidie deni lote,hata kama mimi nisingekubali hadi tone la mwisho aisee,maana yake hapa itabidi baada ya hapo tuwe wachuuzi tu huku mali zetu zikiwaneemesha Urusi na marekani
 
Hali mbaya sana Kwa Ukraine,

Na jinsi anavochelewa kusurrender

Ndo Anazid kukiuka makubaliano yake ya madini na trump,

Maana walishakubaliana na trump, deni la vita litalipwa Kwa madini yote ya Ukraine,

Na Kama mjuavyo, mashariki ndo Kuna zaid ya 70% ya madini yote Ukraine,

Sasa mashariki yenyewe ndo hiyo, Putin keshachukua mikoa 4, sahivi anafukuzia kufikisha 6.

Na Putin keshasema kabisa, ahusiki na makubaliano yake na trump, Hata vita iliisha leo, mikoa aliyochukua hairudishi, Nae ataitumia kujilipa gharama zake za vita.

Sasa sidhan kama trump atakubali kulipwa makinikia badala ya madini ya kule magharibi.

Naiona Tena Ukraine ikienda kusainishwa dili jingine Washington, sioni trump akimshuritisha Putin aachie mikoa 6 anayoishilia Kwa Sasa, kisa mikataba wake na Zelensky.

Yetu macho
Urusi anapigana Vita hii kimkakati sana naona akienda kubeba Maeneo mengi huko ukraine
 
Vikosi vya Urusi vimechukua udhibiti wa kijiji cha kwanza mashariki mwa Ukraine katika mkoa wa Dnipropetrovsk.
Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi pamoja na wanablogu wanaofuatilia vita hivyo.

Hata hivyo taarifa hiyo haijathibitishwa na vyanzo kutoka Ukraine wala Wizara ya Ulinzi ya Urusi. Mara kadhaa Urusi imekuwa ikitaja kuwa tayari kusaini mkataba wa amani lakini ikiitaka Ukraine kujiondoa kikamilifu katika mikoa minne ambayo Urusi iliinyakua kinyume cha sheria.

Hayo yanajiri wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul amewasili hivi leo mjini Kyiv katika ziara ambayo haijatangazwa na yenye lengo la kudhihirisha kuwa Ujerumani inaendelea kuunga mkono mapambano ya Ukraine.

Wadephul anatarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha.
Putins days are numbered. Huu mwaka hauishi
 
Siku URUSI ikiichukuwa Odesa,Moldova atafute njia ya baharini
1000059060.jpg
 
Vikosi vya Urusi vimechukua udhibiti wa kijiji cha kwanza mashariki mwa Ukraine katika mkoa wa Dnipropetrovsk.
Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi pamoja na wanablogu wanaofuatilia vita hivyo.

Hata hivyo taarifa hiyo haijathibitishwa na vyanzo kutoka Ukraine wala Wizara ya Ulinzi ya Urusi. Mara kadhaa Urusi imekuwa ikitaja kuwa tayari kusaini mkataba wa amani lakini ikiitaka Ukraine kujiondoa kikamilifu katika mikoa minne ambayo Urusi iliinyakua kinyume cha sheria.

Hayo yanajiri wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul amewasili hivi leo mjini Kyiv katika ziara ambayo haijatangazwa na yenye lengo la kudhihirisha kuwa Ujerumani inaendelea kuunga mkono mapambano ya Ukraine.

Wadephul anatarajiwa kukutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha.
Huu mkoa upo DPR au LPR?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom