Kuna design za processor za aina mbili duniani ambazo ni kubwa
-arm
-x86
Arm ndio hutumika kwenye simu ukiskia snapdragon za qualcomm, A series za apple, mediatek au tegra za nvidia zote hozi ni arm.
Arm hazina nguvu sana na pia hazili umeme sana ndio maana zinatumika kwenye simu.
Aina ya pili ya design za processor ni x86 ambazo hutumia umeme mwingi lakini pia zina nguvu sana. Hizi ndio zipo kwenye laptop, deaktop, server kubwa na super computer.
Hizi x86 zina watengenezaji wawili tu tena wote toka marekani ambao ni intel na amd. Inamaana serikali zote duniani na makampuni makubwa kama bank, atm nk wanategemea hawa jamaa.
Kipindi cha karibuni kuna jamaa anaitwa snowden akatoa siri kuwa marekani anaspy dunia nzima kupitia technology na computer even maraisi wa nchi kubwa kama ujerumani.
So nchi nyingi zikalalamika ila baadhi kama urusi wakaanza kudesign tech zao, na moja ya mafanikio makubwa ndio hizi cpu. Japo zipo slow ila ni zao