Urusi wazindua processor zao za x86

Urusi wazindua processor zao za x86

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,263
Reaction score
44,391
Toka snowden atoe siri za nsa marekani nchi nyingi zinafanya majaribio ya kujitegemea zenyewe kiteknolojia na kupunguza utegemezi wa kampuni za magharibi.

Urusi baada ya kumwaga mabilioni ya dola za kimarekani kwenye kutengeneza processor zao wenyewe, sasa hivi wanavuna matunda waliyoyapanda baada ya kuzindua processor zao za x86.

Ikumbukwe kwamba processor za x86 kwa sasa zinatengenezwa na kampuni mbili tu za amd na intel hivyo kuja kwa hizi za urusi kutasaidia sana wale wanaojali security kwenye computer zao hasa serikali na makampuni makubwa.

Processor hizi zinaitwa elbrus na nguvu yake wamesema ni sawa na processor za i3/i5 za mwaka 2010.

Processor hizi design yake ni 65nm wakati dunia sasa hivi ipo kwenye 14nm hivyo urusi wana safari ndefu.

Hope jamaa wanafanikiwa na kuleta competition kwa intel
 
Mkuu kuna vitu vya ki-IT umeniacha hapo kama nm, naomba ufafanuzi and I hope utasaida wengi wadadisi kama mie...
Natanguliza shukurani
 
These processors are designed to run Elbrus code, x86 instruction set and features are only emulated. Great progress but they still have a long way to go.
 
Mkuu kuna vitu vya ki-IT umeniacha hapo kama nm, naomba ufafanuzi and I hope utasaida wengi wadadisi kama mie...
Natanguliza shukurani

Kuna design za processor za aina mbili duniani ambazo ni kubwa
-arm
-x86

Arm ndio hutumika kwenye simu ukiskia snapdragon za qualcomm, A series za apple, mediatek au tegra za nvidia zote hozi ni arm.

Arm hazina nguvu sana na pia hazili umeme sana ndio maana zinatumika kwenye simu.

Aina ya pili ya design za processor ni x86 ambazo hutumia umeme mwingi lakini pia zina nguvu sana. Hizi ndio zipo kwenye laptop, deaktop, server kubwa na super computer.

Hizi x86 zina watengenezaji wawili tu tena wote toka marekani ambao ni intel na amd. Inamaana serikali zote duniani na makampuni makubwa kama bank, atm nk wanategemea hawa jamaa.

Kipindi cha karibuni kuna jamaa anaitwa snowden akatoa siri kuwa marekani anaspy dunia nzima kupitia technology na computer even maraisi wa nchi kubwa kama ujerumani.

So nchi nyingi zikalalamika ila baadhi kama urusi wakaanza kudesign tech zao, na moja ya mafanikio makubwa ndio hizi cpu. Japo zipo slow ila ni zao
 
Ninavyojua NM ni nanometer, yaani ndio unene wa ile processor, sijafanya uchunguzi zaidi ila naamini ndio hivyo.
 
Duh upo sahihi sikusoma vizuri post yake

Ni manufacturing process jinsi inavyokuwa ndogo ndio jinsi ambavyo processor inakuwa energy efficient
 
Mbona kama hawaja advance, kama ni processor ya mwaka 2010 sasa kwanini wasingetulia na kuchakaza akili walete bora kuliko hii ya sasa?
USA bado anakimbiza kwenye IT sector itachukua miaka mingi sana mtu kufukuzana nae
 
Duh upo sahihi sikusoma vizuri post yake

Ni manufacturing process jinsi inavyokuwa ndogo ndio jinsi ambavyo processor inakuwa energy efficient

Ila sijajua kama wanapima unene wa chip kwa nje au wanapima zile core peke yake
 
Kinachopimwa huwa ni ile core ya processor sio unene wa full chip
 
Nm ni si unit tu
Kilomita-mita-sentimita-milimita-mikromita-nanomita

Ni kidistance kidogo sanaaaa, ikiwa nanomita ndogo inamaana transistor zinakuwa nyingi kwenye cpu.

Ukubwa wa core mnaouzungumzia nyie unaitwa die. Jinsi nm inavyokuwa ndogo ndio jinsi transistor zinavyokuwa nyingi kwenye die.

Nina video moja hapa inaonesha cpu zinavyotengenezwa sema ni kubwa sana nkipata time ntaielezea kwa maneno hapo chini
 
kama all that effort bado wanatumia 65nm safari ni ndefu kinoma, wanaweza kugive up kabla ya kufikia ligi za intel na amd, intel kutoka 22nm hadi 14nm peke yake ilikua mziki wa miaka hadi mwaka huu walivoachia baytrail kimyakimya... Huyu aliye 65nm labda kama ataleap moja kwa moja... Dunia inakimbia kwa speed sana sasa hivi computer zinahitaji massive speed, hawa jamaa watengeneze tu calculator.
 
Hatimae intel na amd wamepata mpinzani japokuwa mpinzani mwenyewe anasuasua
 
Kuna design za processor za aina mbili duniani ambazo ni kubwa
-arm
-x86

Arm ndio hutumika kwenye simu ukiskia snapdragon za qualcomm, A series za apple, mediatek au tegra za nvidia zote hozi ni arm.

Arm hazina nguvu sana na pia hazili umeme sana ndio maana zinatumika kwenye simu.

Aina ya pili ya design za processor ni x86 ambazo hutumia umeme mwingi lakini pia zina nguvu sana. Hizi ndio zipo kwenye laptop, deaktop, server kubwa na super computer.

Hizi x86 zina watengenezaji wawili tu tena wote toka marekani ambao ni intel na amd. Inamaana serikali zote duniani na makampuni makubwa kama bank, atm nk wanategemea hawa jamaa.

Kipindi cha karibuni kuna jamaa anaitwa snowden akatoa siri kuwa marekani anaspy dunia nzima kupitia technology na computer even maraisi wa nchi kubwa kama ujerumani.

So nchi nyingi zikalalamika ila baadhi kama urusi wakaanza kudesign tech zao, na moja ya mafanikio makubwa ndio hizi cpu. Japo zipo slow ila ni zao

Mkuu Chief Mwawa asante kwa hii elimu. Mie nina swali moja. Kwanza kwa uelewa wangu Processor ni core component ya simu au computer, hivyo bila kuwa na kitu hicho huwezi kusema umetengeneza simu au computer, sasa swali langu ni hili, haya makampuni kama Sumsung, sijui Tecno, Huawei nk kama hayatengenezi hizo processor, yanatengeneza nini?
Yaani wao wanatengeneza ile shape ya nje tu? Naomba unisaidie nijue hasa wao wana kitu hasa wanachotengeneza kama the core component of the device si yakwao!
 
Inategemea na kampuni.

Samsung ana processor zake za arm zinaitwa exynos, na apple ana zake na huawei ana zake zinaitwa kirin. Tofauti na hawa sidhani kama kuna mwengine mwenye processor zake. Ila processor za simu zote ni za arm hivyo samsung/apple/huawei hawafanyi kazi kubwa sababu tayari arm ameshadesign wao wanalipia licence na kuziredesign wanavyotaka wao.

Samsung pia ni mtengenezaji mkubwa wa memory kama internal storage na ram.

Sony yeye anatengeneza sana sensor za camera pamoja na toshiba

Sharp na lg wanatengeneza sana display.

Nokia na erricson wao ni wakali wa network.

Kampuni inapotengeneza simu inanunua technology toka makampuni mengine na kutengeneza simu.
 
mkuu nina swali kuhusiana na makampuni kama TECNO, ITEL and the like. hawa jamaa wanatengeneza CPU zao wao wenyewe? na kwann hawapo GSMarena?
 
Back
Top Bottom