Urusi: Marekani inashirikiana na Ukraine katika kutengeneza silaha za kibiolojia

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Urusi:
Marekani inashrikiana na Ukraine katika kutengeneza silaha za kibiolojia

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa Marekani imekuwa ikidhamini fedha kwa ajili ya mradi wa kuzalisha silaha za kibiolojia nchini Ukraine, na kwamba Moscow ina ushahidi unaothibitisha suala hilo kutoka kwenye maabara za Ukraine.

Mjadala kuhusu ushirikiano wa Marekani na Ukraine katika kuzalisha silaha za kibiolojia ulianza baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Victoria Nuland kutangaza hivi karibuni kwamba, kuna vituo vya utafiti wa kibiolojia nchini Ukraine ambavyo Kyiv na Washington zinafanya jitihada za kuhakikisha kwamba mada zinazorundikana huko hazianguki mikononi mwa majeshi ya Russia.

Shirika la BBC limemnukuu msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia, Igor Konashenkov akisema: "Madhumuni ya utafiti huo wa kibiolojia uliofanywa kwa bajeti ya Pentagon nchini Ukraine lilikuwa kupanga utaratibu wa kueneza kwa siri vimelea vya maradhi."

Konashenkov ameongeza kuwa: "Mafashsti wa Ukraine wanapanga njama za kufanya uchochezi kwa kutumia mada za sumu ili kufungua njia ya kuituhumu Russia kwamba imetumizi ya silaha za kemikali."

Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa, Anatoly Antonov, Jumatano iliyopita aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba: "Matamshi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kuhusu maabara za kibiolojia nchini Ukraine yanaonyesha kuwa, Washington ina wasiwasi kwamba vimelea vya magonjwa vilivyohifadhiwa kwenye kituo hicho vitanaswa na wataalamu wa Russia."

[https://media]Anatoly Antonov

Balozi Antonov amesema, iwapo vimelea hivyo vya maradhi vya silaha za kibiolojia vitaangukia mikononi mwa Russia, nchi za Ukraine na Marekani lazima zikiri kwamba zimekiuka Mkataba wa Marufuku ya Silaha za Kibiolojia na za Sumu.

4bvge1b253a9f31s43t_800C450.jpg
 
Kuna pro-Russia mmoja siku za nyuma alisema Marekani Haina Uwezo wa Kutengeneza Biological and Chemical weapons. Eti Urusi ndio anahiyo teknolojia TU. Pro-Russia walimsapoti balaa Sasa Leo baba yenu analia kisa Chemical na Biological Waepons za Marekani.
 
Marekan anapiga marufuku hizo silaha kinafiki. Sasa lengo la kutengeneza na ukraine ni nini?

Basi Russia ana sababu 100% za kuivamia ukraine
 
Back
Top Bottom