Urusi kuangushwa na Uturuki katika Mgogoro wa Azerbaijan na Armenia. Je, huu ndio mwisho wa Urusi?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Amani iwe nanyi wadau

Tanzania ikiwa inaendelea na uchaguzi mataifa wawili yalikuwa vitani(Armenia na Azerbaijan). Armenia ikiungwa mkono na Urusi kwa kuwa na watu wengi wanaozungumza kirusi (Christian Orthodox) na Azerbaijan ikiungwa mkono na uturuki kwa kuwa majority ya population yao ni Shia Moslems.

Mgogoro huu umeisha Juma lililopota kwa Armenia kuomba vita iishe na kukubaliana kuachia sehemu ya jimbo la Nagorno -Karabakh kwa Azerbaijan ambao walishaanza kutangaza ushindi mnono kwenye vita hii!

Kwa wachambuzi wa siasa Hii ni ishara ya kuanguka kabisa kwa urusi katika siasa za dunia na kuibuka kwa Uturuki Kama New World Power.

Uturuki pia ana mgogoro na China kwa sababu ya China kukandamiza haki za Waislamu wachache wa jamii ya Uyghurs.

Swali sasa ni Je, Kwa hali inavyoenda duniani huku Ccm wakiwa wanawategemea China na Urusi, CCM itaendelea kuwa hai katika miaka michache ijayo?

Naomba ukichangia mada hii usisahau kuwa Mabalozi wa nchi zinazoongoza kuipa fedha na misaada Tanzania (Marekani, Uingereza, Ujerumani, Korea Kusini, Japan, Sweden, Norway, Canada na Umoja wa Ulaya) hawajaudhuria shughuli ya leo ya Magufuli kufungua bunge.

Yajayo yanafurahisha!!
 
Angalia sbb zifuatazo:

Jumuiya ya kimataifa including Russia haikuwah kuikubalia Armenia kumiliki hili eneo lililo kwenye mgogoro, hivyo Russia haikuona umuhimu wa kuizuia Az. isifanye yake

Turkey iliyo upande wa Az. imekuwa rafiki wa Russia hivi karibuni, na Putin ameona aendeleze urafiki; kumbuka Uturuki ni nchi ya pili kwa ukubwa wa jeshi NATO ikitanguliwa na US. Mrussi anakiri siku zote NATO ndio adui yake namba 1; kujipendekeza kwa uturuki ni kumong'onyoa umoja wa adui yake: jambo ambalo amefanikiwa. Sasa Edrogan yuko karibu na putin kuliko Western leaders.

Sababu ya tatu ni kwamba kiongozi wa Armenia alionesha kuegemea upande wa nchi za ulaya(Pro western) na hivyo Russia kaona ni mda muafaka wa kum'punish. US haijaingilia moja kwa moja probably sababu ya uchaguzi.

Sasa kwenye makala yako kuhusisha kuanguka kwa Russia na China kwa nguvu ya Western countries naona hujaitendea haki kalamu ya uandishi.
 
Urusi ni super Power,ni taifa tajiri wa kiuchumi na kiteknologia..

Uturuki haiwezi kumfikia Urusi kwa chochote kile

Uturuki ni mwanachama wa NATO,Mrusi akiipiga Turkey ameipiga USA na Washirika wake

Mrusi hajashindwa vita,amepotezea tu
Basi angemgusa kumbe nae anaangalia kumbuka ktk vitabu vya dini Turkey ndio wagalatia
 
Japo sidharau uwezo wa Uturuki kijeshi unao chipukia kwa kasi,ila suala la kuilinganisha Uturuki na Urusi kijeshi una kosea sana.
Zipo sababu nyingi tu zilizo ifanya Urusi kutotumia nguvu nyingi kwenye huu mgogoro nazo ni kulinda masilahi yake.

Kwanza tambua ya kwamba licha ya Urusi kuwa mshirika wa Armenia kijeshi, lakini wakati huo huo ana ushirika mkubwa wa kibiashara na Azabeijan, maslahi ya kiuchumi anayo yapata kwa Azabeijan ni zaidi ya mara tano ya yale anayo yapata kukoka Armenia kwa sababu uchumi wa Armenia ni mdogo mdogo sana ,kwa hiyo mataifa yote mawili ni muhimu sana kwake.

Sababu ya pili ni Urusi ina masilahi makubwa kwa Uturuki kuanzia kibiashara , kijeshi na kimkakati na pia anatumia Uturuki kuiyumbisha NATO kutokana na akili za Erdogan. Kwa hiyo asinge penda kuikwaza Uturuki.

Hivi ujiulizi ni kwa nini Syria imeacha kuishambulia vikosi vya Uturuki kama mwanzo? Ni kwa sababu Urusi umenikataza kufanya hivyo.
Lakini kumbuka Uturuki ilijiingiza moja kwa moja kwenye hii vita kwa kutuma wana jeshi wake na drone,sasa jaribu kufikiria nini kingetokea iwapo na Urusi na yenyewe ingeamuwa kujiingiza moja kwa moja kwenye hii vita siingekuwa balaa?

Hivi umejiuliza nn kingetokea iwapo ndege za kivita za Urusi zinge vishambulia vikosi vya Uturuki? Kilicho hapa ni Putin katumia busara ya hali ya juu sana kwa sababu mataifa yote yanayo shiriki kwenye hii vita yote ana masilahi nayo.

Lakini kuhusu suala la uwezo wa kisheji Uturuki ina hitaji miaka mingi kuufikia uwezo wa Urusi kijeshi.
 
Japo sidharau uwezo wa Uturuki kijeshi unao chipukia kwa kasi,ila suala la kuilinganisha Uturuki na Urusi kijeshi una kosea sana.
Zipo sababu nyingi tu zilizo ifanya Urusi kutotumia nguvu nyingi kwenye huu mgogoro nazo ni kulinda masilahi yake....
Taarifa za ndani zinasema Urusi hana hiyo nguvu anayojitangaza anayo. Urusi hata kiuchumi ameanguka vibaya sana hivi.

Kuna taarifa pia hali ya Putin kiafya sio nzuri sana kwa sababu umri umemtupa sana mkono na hapo ndo urusi inaonekana haiwezi tena kuwa stable kwa sababu siku zote imekuwa ikitegemea watu strong kuliko taasisi imara kama ilivyo Marekani.

Uturuki kwa sasa ni moja ya nchi inayozalisha silaha za kisasa na kuziuza nchi mbalimbali duniani na ni moja ya nchi iliyowekeza sana kwenye tafiti za kiteknolojia.

Kuna uwezekano kwa uimara wa NATO, Magharibi wakaruhusu Uturuki iwe among super powers ili kudhibiti na kuimaliza kabisa Urusi
 
Aliyeshinda vita ni Azerbaijan wala sio Turkey. Azeri wana bajeti ya jeshi mara 5 ya Armenia, wana population karibia mara tatu, wana wanajeshi zaidi ya mara mbili wana uchumi karibia mara tatu. Sasa Armenia ingeanzaje kuwashinda.

Kiteknolojia Azerbaijan wako mbali sana na Armenia. Wana silaha za gharama kutoka Israel, Turkey na Russia. Armenia wanapewa silaha chache kutoka Russia na nyingine wanakopeshwa kiurafiki tu.

Hakuna mwanajeshi yeyote wa Urusi aliyeshiriki kwenye vita hii. Walikufa marubani wawili tu kwenye ile Mi-24 iliyodunguliwa wiki hii kimakosa na Azerbaijan, ambayo iliomba msamaha mara moja. Helicopter ilikuwa na mission zake wala haikuhusika na vita hii.

Turkey kapeleka silaha kibao kusaidia Azerbaijan ila uchumi wake haumruhusu kufanya proxy war, ndio maana Erdogan alikuwa mbio mbio kumtaka Putin asimamishe vita. Kama walikuwa wanaelekea kushinda kwa nini atake vita iishe si angesubiri watwae eneo zima.
Hizi vita zina gharama sana imagine drone zake 9 za Bairaktar TBT zimedunguliwa na Armenia. What if Russia angepeleka air defence systems na anti-drone systems kingetokea nini.

Huyo Turkey si level za Russia kwenye vita. Speed yake kijeshi ni kubwa lakini bado sana ni mdogo. Tatizo unasikia hotuba na kelele za kujimwambafai wanazotamka Waturuki, wao wenyewe wanajua kabisa nchi iliyowauzia S-400 air defense system sio level zao. Nchi inayowekeana mikwara na Egypt na kupigiana mazoezi kutishana ndio ije ishindane na Russia?

Mwisho, Russia hakuwa na sababu za kuizuia Azerbaijan isichukue eneo lake kama yeye alivyoichukua Crimea yake. Kwanza huyo Nikol Pashinyan alishajikuta pro-Western na nina wasiwasi hamalizi mwaka huu madarakani. Ya nini kumpigania mtu aliyebase upande wa US.
Rejea Ukraine ilivyokuwa na Viktor Yanukovich na ilivopata waliofatia jinsi msimamo wa Russia ulivyobadirika kinyume.
 
Back
Top Bottom