Ifahamu Bosphorous straits: eneo la kimkakati kibiashara lililopo Uturuki na uwezekano wa kutokea mzozo mpya na Urusi

SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
7,079
7,976
Lango la Bosphorus, maarufu kama Istanbul Strait, ni njia nyembamba na asili ya maji iliyoko katika jiji maarufu Istanbul nchini Uturuki.

Uchochoro au mkondo huo unaunganisha bahari Nyeusi (the Black sea) na Bahari ya Marmara; yaani kwa kifupi ni kiunganishi kati ya Ulaya (kwa upande wa Magharibi) na Asia ( kwa upande wa Mashariki.

Mkondo huu una urefu wa kilometa zipatazo 31 (sawasawa na maili 19) na upana wa kilometa 3.7 (sawasawa na maili 2.3).

(Faida za kiuchumi)
Mkondo huu una umuhimu katika usafiri wa kimataifa, kwani meli za baharini kati ya Bahari ya Mediterania na Bahari Nyeusi zinapitia njia hii. Taifa la Urusi ni moja nchi ambazo hutegemea sana lango hili la Bosphorous katika kusafirisha shehena zake.

(Hatari ya mzozo wa kivita)
Katika hali isiyotarajiwa ya hivi karibuni ya undumi la kuwili wa bwana Erdoğan kuruhusu Sweden kujiunga na jumuiya ya NATO, kuna kila dalili za kuibuka mzozo mpya baina ya Uturuki na Urusi, (NARUDIA TENA, UTURUKI NA URUSI), hali inayoweza kupelekea Uturuki kumuwekea vikwazo Urusi kutumia lango la Bosphorous.

Sijui hali itakuwaje mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu 2023, lakini kwa jinsi muendendo wa mambo navyouona, kuna kila dalili ya nchi nyingine kuingia mazima katika mzozo huu wa Ukraine and Russia.
IMG_20230712_201243.jpeg
 
Kwani Mkataba unasemaje kuhusu hilo Lango la Bosphorusa kimataifa?
Wanachoweza kufanya ni kuwekeana vikwazo tu lakini hawawezi kuingia vitani hata siku moja! Sema kinachofanyika Uturuki imebanwa mno na US na washirika wake,nadhani wanailazimisha kuvunja uhusiano na Russia kwa faida ya muungano wa NATO!
 
Back
Top Bottom