Sun Zu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2022
- 758
- 2,106
Mkuu wa baraza la ulinzi la Urusi Dmitry Medvedev amesema Urusi haitishwi na kauli ya raisi wa Marekani Donald Trump kuhusu vikwazo zaidi kwa nchi hiyo endapo itagoma kusaini mkataba wa kusitisha vita huko Ukraine ndani ya siku 50 (49 sasa š) zijazo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Medvedev amesema Urusi kamwe haitishwi na vitisho vya Donald Trump kwa kuwawekea vikwazo vya kiuchumi wale wote wanaonunua gesi, mafuta pamoja na uranium kutoka nchini humo.
Medvedev aliongeza kuwa ulimwengu lazima utegemee kutetemeka huku baadhi ya nchi za ulaya zimechukizwa na kauli ya Donald Trump kwa sababu nishati kutoka nchini Urusi ndiyo nishati nafuu zaidi kwao. Hata hivyo Urusi haitishiki kwa vitisho vya Trump.
Kauli hii ya Dmitry Medvedev inakuja mara baada ya raisi wa Marekani Donald Trump kutangaza kupeleka silaha zaidi nchini Ukraine ili kuifanya Urusi irejee kwenye mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro uliopo ulaya mashariki baina ya Urusi na Ukraine.
NB: Niliwahi kusema humu kuwa hakuna mtu yeyote kutoka nje ya Urusi ambaye anaweza kuamua hatima yao kwenye huu mgogoro uliopo ulaya mashariki baina ya Urusi na Ukraine isipokuwa ni warusi wenyewe. Licha ya vitisho na kauli nyingi za Donald Trump kuhusu Urusi, wanaume wamemjibu kwa kauli moja tu kuwa hawatishiki na kauli zake.
Halafu Urusi angekuwa anaziogopa nchi za magharibi ungeona yeye ndiye anahangaika kutafuta suluhu ya huu mgogoro. Lakini cha ajabu licha ya kulundikiwa vikwazo lukuki vya kiuchumi ndio kwanza anazidi kupigana na wala hajaonekana kwenda kuwapigia magoti watu wa magharibi ili warudi kwenye meza ya mazungumzo. Sasa uoga wa Urusi uko wapi?