Uroho wa madaraka unavyomgharimu Kafulila

Hivi unajua sura za wajumbe wakati wanakushawishi
JamiiForums-861156505.jpg
 
Huyu kazi yake kubwa ilikua ni Kasubili zitto atoe data halafu yeye anakuja kinyume chake kwa kujipendekeza kwa mkuru
 
Ujue mimi nimejiuliza mpaka nashindwa kuelewa hawa wateule wa Rais huwa wanafikiria nini. Hivi kweli mtu inaacha u RAS unaenda kupata kura 64? Serious kabisa unaenda kuwa mshindi wa nne, RAS...


yani hata kufanya tathmini ndogo umeshindwa? Yupo aliyeacha u DC kaenda kupata kura 12
nani huyo mwenye kura 12? DC wa wapi Moshi?
 
Habari wana JF,
Kwa awamu nyingi Kigoma imekuwa miongoni mwa Mikoa michache inayozalisha wabunge wengi vijana wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na hatimaye kujipatia umaarufu mkubwa nchi nzima.

Baadhi yao huanza kuwa na kiburi Mara wanapojihisi wamefanikiwa zaidi kisiasa na kuanza kuwakejeli waliowafanya wafike hapo walipofika.

Uroho wa madaraka pia imekuwa kikwazo kwa viongozi wengi Vijana, Hutamani kufanikiwa zaidi kisiasa kuliko kufanya kazi walizoagizwa na wananchi Bungeni,Kafulila ni mmoja kati ya vijana walioingia Bungeni (2010-2015) kwa kasi na kupata umaarufu wa haraka kwa umahiri wake wa kufichua maovu mbali mbali katika Serikali hadi kufikia hatua ya kuitwa "tumbili".

Aliwahi kumkashifu ZZK aliyemshika mkono na kufanikiwa kuwa Mbunge wa JMT.

Licha ya kuwa mwanasiasa mzuri Amekuwa kijana mwenye Kiburi kwa viongozi wake na mwenye uroho wa madaraka vilivyompelekea kutimuliwa na Chama chake Cha Awali Cha CHADEMA na kutimkia NCCR-MAGEUZI ambako alipewa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika ngazi ya ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini na Kushinda, Alihudumu kwa Kipindi Kimoja na hatimaye katika Uchaguzi wa mwaka 2015 akashindwa na Mwana-mama Hasna Mwilima. Alikimbilia mahakani na kushindwa Mara kadhaa.

Akahamia CCM, Mheshimiwa Rais akamteua kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe kutokana na utendaji Kazi wake wa Awali... 2020 akajivua cheo Cha U-RAS na kutia Nia ya kuteuliwa na Chama chake kugombea nafasi ya Ubunge na Akapigwa kipigo Cha mbwa Koko.

MH. Rais aliwaonya wateuliwa wake na kuwakumbusha kuhusu Kisa Cha Mwananzila aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora ambaye alipotea Kisiasa kutokana na uroho wa madaraka. Kafulila amepotea tayari, Kafulila tumsahau Kabisa,Kapewa nafasi na mheshimiwa Rais kaona haifai asitarajie miujiza yoyote ya kupata nafasi ya Kuteuliwa na Mh. Rais.
Bado hajakomaa kisiasa wanasiasa uchwara hununuliwa kirahisi na kuuzwa(bendera fuata upepo) 'cheap politicians are easily bought and sold'
 
Sitaki kuamini kama Kafulila alishindwa uchaguzi wa 2015 kwenye box la kura,
Walimchakachua tena kibabe hata alipokwenda mahakamani fomu za matokeo ya vituo zilikataliwa kupokelewa kama vielelezo kama walivyo muibia Wenje Nyamagana pia, kilichonishangaza akaenda kuungana nao waliomuibia.
 
Kafulila ni Mnafiki, Hana Aibu tena Macho Makavuu.

Hana aibu.

Usishangae akahamia tena ACT Wazalendo na kugombea Ubunge mwaka huu.
 
Akili za wanasiasa ni ngumu sana kuzielewa.

Inakuwaje unaacha kazi ya "utawala" wa mkoa, kwenda "kutafuta" nafasi ya kuwa mwakilishi wa "kaeneo" ndani ya mkoa?
 
Back
Top Bottom