Urithi unaenda kwa nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urithi unaenda kwa nani?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Donn, Oct 26, 2012.

 1. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Endapo baba akifariki akaacha watoto wawili wakike (18+) na wakiume (18+), lakini hajaacha wosia uridhi wa ardhi ya marehemu itaridhiwa na mtoto yupi? Au watoto wote?

  Je endapo marehemu akiacha wosia wa kumuachia mali yote mtoto mmoja tu wakiume, mahakama inaweza vunja wosia endapo watoto wengine wa marehemu wakifungua kesi ya madai?
   
 2. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  sasa hapo sijui ngoja 2ngoje wa wa law udsm na school of law waje
   
 3. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Subiri wanasheria watakuja sasa hivi kutujuza.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Familia iliyofiwa itagawana mirathi kulingana na aidha itikadi/imani ya dini yao, au watatumia mahakama kuhamua jinsi ya kugawana mali, wakati mwingine sheria za kimila utumika katika kugawana urithi. Kumbuka kwamba urithi ni haki ya kila mtoto aliye hai.

  Kwa swali lako unabidi ufafanue, mirathi hiyo inatakiwa kugawanywa kwa utaratibu upi?
   
 5. M

  MMOJA JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 218
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ni vizuri hii mada ungeipost JF jukwaa la sheria,nadhani ungepata ushauri,kwani kule ndio mahala pake.
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  inategemeana na aina ya sheria itakayotumika kugawa mirathi hiyo. kuna aina tatu zinazotumika, kwa kifupi, kuna mirathi inayogawanya kwa dini ya kiislam, mirathi kugawanywa kimila na ile kiserikali. yaani either kutumia sheria ya kiislam, kutumia sheria za kimila na kutumia sheria ya kiserikali yaani Indian succession Act ya mwaka 1885. kama watawaganya kwa kutumia sheria ya kiselikali, basi wasichana na wavulana watagawanywa kihalali bila kubaguana kwenye gender.hii ndo sheria isiyo na matatizo. kama ni kiislam itagawanywa kwa quran, kama ni kimilia, kwa kifupi ni kwamba, wanawake huwa hawamiliki ardhi/nyumba ila wanaweza kuruhusiwa kuishi ndani hadi pale watakapoolewa. sheria ya kimila ina matatizo sana. kuchagua sheria huwa kuna kipimo kupima kama marehemu alikuwa anaishi maisha ya aina gani. watu wengi wa vijijini huwa wanadhaniwa kuwa waliishi kwa kimila labda utoe ushahidi mpya kubatilisha hilo, wale walioishi miijini muda mrefu na hawakuwa wanafuata mila na desturi katika maisha yao huchukuliwa kama waliishi maisha ya kisasa hivyo sheria ya kiserikali itatumika, wale waliokuwa wanaishi maisha ya kiislam sheria ya kiislam itatumika. mjane anapata 1/8 na iliyobaki wanagawana warithi wengine kama watoto na ndugu wa karibu. sheria ya kiserikali inaweza isigawe mali kwa ndugu wakati mwignine, mali zikaenda kwa watoto.
   
 7. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Opps... Naona nimeipost hapa kwa bahati mbaya .... Msaada mod kunihamishia jukwaa :sorry:
  but ninaongelea endapo sheria za mahakama zitatumika
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mahakama inaamuwa? mahakama haiamui mahakama inahukumu. Mjiamulie nyie mnataka sheria ipi itumike, mkishindwa kujiamulia, mahakama itaamuwa kutokana na sheria ya Dola. Mahakama kama mahakama haina sheria.
   
 9. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,491
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  kuna dalili za kuchakachua wosia hapa
   
 10. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hapo nimeongelea kesi mbili tofauti, endapo wosia haupo. Na endapo wosia ukiwepo.. mpalu
  but napenda kufahamu endapo mahakama ndo itahusika na utoaji wa maamuzi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Wewe acha kupotosha mahakama inafanya maamuzi kwenye makosa ya madai na inahukumu kwenye makosa ya jinai......na kuna maamuzi yanayofanywa na mahakama ni sheria(PRECEDENT) kuna mazingira flani mahakama inatoa mwongozo unaofanana na kutunga sheria...ZOMBA kama hujakaa darasani kusoma sheria usijaribu kupotosha watu umu sheria is a noble proffessional don dare to put your politics.
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wewe ndio katika wale waliojazwa Ubaguzi wa Ujinga. Mahakama inahukumu haiundi wala kutunga sheria, maamuzi ya mahakama ni hukumu, mahakama inaweza kuweka kanuni lakini si sheria au sharia. Usitake kupoteza watu.
   
 13. ram

  ram JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,210
  Likes Received: 909
  Trophy Points: 280
  Eeeh! Kwani hili ni jukwaa la nini?

   
 14. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Wewe ni mbumbumbu wa sheria siwezi bishana na mimi nimekaa darasani wewe ni BUSH LAWYER.
   
 15. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,491
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  ndugu kama kingereza kinapanda na si mvivu wa kjisomea unaweza kupitia hapa chini
   

  Attached Files:

 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ulikuwa unajazwa Ubaguzi wa Ujinga kwenye kuta nne, mwenyewe unajiona ndio umesoma. Ungekuwa unajuwa maana tu ya neno "mahakama" kuwa ni panapotolewa hukumu, usingeyasema yote hayo. Labda Kenya ndio mnatunga sheria mahakamani, nyang'au wahed wee!
   
 17. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Huu ndio ushauri wa kisheria kwa jinsi nnavoifahamu mimi sheria.
  Isipokuwa tu hiyo India Succession Act ni ya mwaka 1865.
  Ila mengine yote umepatia. Humu ndani naona Zomba na mwenzake wanabishana tu vitu visivo na msingi na kutukanana bila kujibu swali la msingi.
  I‘m on mobile otherwise i would‘ve given you a ‘like‘ my fellow learned bro.
   
 18. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  ahsante, nitalipitia lote night, thnx
   
 19. Donn

  Donn JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,450
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  dah... Ahsante sana kwa hii info bro
   
 20. M

  MMOJA JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 218
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mwanzo hii mada ilikua jukwaa la nafasi za kazi na tenda,naona sasa wamefanikiwa kuihamisha,nashukuru ushauri wangu umefuatwa
   
Loading...