Zinduna
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 2,377
- 3,394
Urembo wa Ndonya ni mojawapo ya hadithi zinazopatikana katika kitabu cha zamani kilichokuwa na mkusanyiko wa hadithi mbalimbali za kufurahisha na zenye kufundisha. Kitabu hicho kilikuwa kinaitwa Ujinga wa Muafrika.
Nimebahatika kukisoma kitabu hicho kutoka katika maktaba ya baba yangu. Katika mojawapo ya mkusanyiko wa hadithi hizo kulikuwa na hadithi moja inayoitwa Urembo wa Ndonya. Huyu Ndonya alikuwa ni binti ambaye alikuwa akipenda sana urembo na katika kujiremba kwake kulikuwa na ule mtindo wa kuchoma nywele na shanuo la chuma baada ya kuwa zimepakwa mafuta ya nazi mengi ili zionekane kama za kizungu hivi. Sasa siku moja katika kuchoma kwake nywele kwa bahati mbaya moto ukalipuka kurukia kichwani ambapo aliungua nywele zote na kubaki Kipara. Nyani Ngabu atanisaidia kama kumbukumbu zangu hazitokuwa sahihi maana nilikisoma zamani kidogo na nimejaribu kukitafuta lakini wajukuu wa huyu Mzee weshakichanachana na kukitupilia mbali.
Naam nimekumbuka hadithi hii ya urembo wa Ndonya baada ya kusoma habari moja ya urembo unaofanywa na mabinti huko Afrika Magharibi hususan nchini Senegal na Gambia.
Ni kwamba kumezuka urembo maarufu kwa mabinti kubadili fizi za meno yao na kuwa nyeusi kwa mfano wa tattoo. Kinachofanywa na mabinti hawa ni kuchomachoma fizi kwa sindano na kuweka mchanganyiko wa unga unga utokanao na mafuta yaliyounguzwa na kuchanganywa na samli ambapo mtu akichomwachomwa na sindano na kuwekewa huo unga kama wafanyavyo wachora tattoo fizi zao huwa nyeusi tii na kuacha meno maupe yakionekana dhahiri.
Urembo huo ambao mabinti hao hukiri kwamba ni wa mateso na unaowaacha na maumivu makubwa lakini wamekuwa wakiufanya ili kuwavutia wanaume. Wenyewe wanadai kwamba wanaume nchini mwao hupenda tabasamu la mwanamke mwenye meno meupe na fizi nyeusi na ndio maana wako tayari kupata maumivu ili wapate kuwavutia wanaume.
Balaa gani hili yarabila ala mina kujichoma misindano ili mijanadume initake, kwani wanaume wanapenda fizi nyeusi au ‘papuchi' kajisemea Raiza.
Kwa kweli ukiangalia kwenye picha jinsi wanavyokuwa tortured utadhani wako Guantanamo lakini kumbe ni maumivu ya kujitakia.
Wanawake wenzangu tuige yote lakini nawaomba aina hii ya urembo tusiige maana licha ya madhara ya Kiafya lakini ni hatari kwa maambukizi ya Ukimwi.
Na nyie wanaume msije anza kuwasifia wanawake wenye fizi nyeusi na kuwakimbilia maana mtasababisha watu tuanza kuzisaka fizi nyeusi kwa gharama yoyote.