Uranium Mining Projects In Tanzania: Progress...

Eddy, hawa wanataka kuchimba na siyo kuwekeza kwenye kinu etc. Hii uranium watakayoichimba ni kama dhahabu na mineral nyingine wanazozichimba na sisi tunabakiwa na mashimo tuu! Hakuna mtaji hapa!

FM:

Sasa unalalamika nini? Tukisema tujifunze tuanze wenyewe unaleta longolongo. Tukiwapa WAPWEKEZAJI unasema watatuachia mashimo tu. Je unapendekeza nini? Maana mpaka sasa unakatoa hoja kwa kuonyesha uzembe kwa vile tulivyoshindwa au tunavyoshindwa.

Mimi nataka NYUKI na kama nina matatizo naomba uniambie nianze kujibadilisha na kujenga misingi ya technologia hiyo. Na hata kama itachukua miaka ishirini au hamsini weka estimation zako.

Tanzania imeshindwa kutengeneza viatu, imeshindwa kupambana na malaria. Na kwa ujumla imeshindwa kufanya vitu vingi ambavyo viko ndani ya uwezo wake.

Pamoja na kushindwa kwetu kuna uwezekano mkubwa sana kuwa kizazi kinalichozaliwa baada ya Azimio la Arusha kinaweza kuleta mabadiliko iwapo mambo fulani yatatimizwa au kutafutiwa ufumbuzi.

Unasema Tanzania inapenda miradi mikubwa kwa sifa. Hayo makosa yalifanyika na yametuingiza katika madeni mabaya. Katika miradi ya nguvu za umeme Tanzania haijafanya kwa sifa na miradi hiyo inatumikia taifa ukiondoa IPTL na Richmond ambayo haikufuata taratibu za kibiashara na ufundi.
 
Tatizo sio sisi tunaong'ang'ania vya zamani. Hii teknoloji mnayoibebea bango si ya leo. Imeanza kutumiwa toka fifties. Nyinyi wenzetu ndio mnakuwa single tracked. Mnakataa kabisa kuangalia alternatives ambazo zinajitokeza na kuanza kupewa umbele katika nchi za wenzetu mkikazania hii ambayo mnaona itatuweka kwenye chati. Hizi tunazozingumzia ndiyo wenzetu wanawekeza ilikuondoka kuwa tegemezi kwenye nyanja hii. Teknoloji hiyo ya nyuklia itatuweka kuwa tegemezi tukitegemea good-will ya wakubwa ili tuweze kuendelea nayo. Mimi sioni huo uhuru mnaodai utapatikana vipi kwa kutegemea chanzo ambayo ili tuianzishe itatubidi kukopa kwa wenye nazo, kukubali annual inspections n.k. Cutting edge resarch ni kwenye alternative energy sources na sio kama mnavyodhani kwenye hiyo nyuklia. Tusiwe kama North Korea, wana mabomu ya nyuklia lakini wanashindwa kuwalisha watu wao.

Hata computer zilianza zamani lakini upatikanaji wake ulitegemea maendeleo yake ambayo yalifanya bei kuwa chini. Vilevile kuanzia miaka ya 50 na 60 kulikuwa na wimbi la mabadiliko ya maendeleo ya kijamii na nchi nyingi kupata uhuru. Wimbi hili na uhuru lilisababisha nchi nyingi kufungua vyuo vikuu ambavyo vilifanya technologia kuanza kuenea duniani.

Hiyo alternative energy unayopigia kelele ni muhimu lakini Tanzania ina idadi inayokaribia 40Milioni.
 
Sasa unalalamika nini? Tukisema tujifunze tuanze wenyewe unaleta longolongo. Tukiwapa WAPWEKEZAJI unasema watatuachia mashimo tu. Je unapendekeza nini? Maana mpaka sasa unakatoa hoja kwa kuonyesha uzembe kwa vile tulivyoshindwa au tunavyoshindwa

Naomba tukubaliane kutofautiana. Kama mwenzangu hauoni tofauti kati ya mwekezaji kwenye KUCHIMBA na mwekezaji kwenye uzaishaji wa nishati naona tuna tatizo kubwa la mtizamo. Au mwenzangu unadhani hizo 3 au 5% za madini haya ndiyo zitatupa utajiri wa kuinvest kwenye nyuklia? Mwenzangu unaupenda ubepari kwa kuangalia Manhattan, mimi nauchukia kwa kuangalia South Bronx! Wewe unaona maghorofa ya city centre Dar na vijishopping CENTRE vya shoprite mimi naangalia mbavu za mbwa zilizotapakaa ndani na nje ya Dar! Hatutaweza kukubaliana hata iwe vipi.
 
Nisamehe kutumia jina lako vibaya. Ni usingizi na kukosea kidogo.
1./ Wangetucheka, wangetuzuia na kutupa sanctions. Vitu hivi hutangazi. unafanya kisiri, unashitukiza ukikaribia kumaliza. Au dili na warusi au wachina. Au wape madini wamarekani moja kwa moja, waambie wajenge hiyo Nuclear Plant.

2./ Priority yao sio wakufundishe technology. Priority ya wazungu ni kukufanya wewe uwategemee (soma Economic Hitman labda itakusaidia kuelewa). Ndio maana waChina na waHindi wanawasumbua vichwa, maana hawahitaji msaada wao. Pia, wanafunzi wetu wanapata scholarship za 'arts' nyingi....lakini engineering chache. Kuna watu wanasomea kilimo nje ya nchi, lakini bado tuko nyuma katika kilimo. Mzungu hakusaidii, jisaidie mwenyewe (read UKRAINE).

3./ Hapana, siwezi kuwa hivyo, siko involved na nyuki, ila kama naona opportunity hiyo ipo TZ, then najipachika sehemu huku for atleast 5 yrs (hii ni field iliyo na siri, na lazima upigwe checks kibao. wakati nasoma degree, pass yangu ya bongo wali-kataa kunichukua kama intern kwenye plant ya Nuclear, ila kuna washikaji waingereza waliingia kiulaini, maana they needed people). Ila naamini kuna waTanzania wengine lazima wako katika field hiyo, pia tuna Physicist wazuri tu around the world. Kuna mwalimu wa kibongo alinifundisha Physics, yuko Australia, mtu kama huyo si kawaida. Kama tuna mbongo NASA, basi sehemu zingine wapo tu, better equipped.

Ila ukija katika fani zingine za non/renewable sources, hizo naweza contribute moja kwa moja (na nina imani zaidi na hizi kwa Tanzania, taking into account our competence as peoples). Mimi nimespecialise katika sector moja, ila kutokana na foundation, ni rahisi kuingia sector yoyote (then give a year to feel specialised in that sector).

(Ukitaka kujua zaidi ni-PM).

Nzokanhyilu:

Point ulizoweka hapa ndizo zilipo kichwani mwangu. Kwa maoni yangu binafsi idadi ya watanzania waliosoma inatoasha kuanzisha wa maendeleo. Lakini priority zetu hazina mwelekeo.

Na kwa sasa hata vijana wanaofanya vizuri masomo ya sayansi, wengine hawataki kabisa kuchukua digrii za sayansi na engineering.

Na trend tuliyonayo hata masuala ya alternative energy itabidi tusahau.

Anyway wengine tuna mipango ya kurudisha passport.
 
Anyway wengine tuna mipango ya kurudisha passport.

AFANA-LEIK Bin Maryam mswalie mtume mwanakwetu, si tunasikia Membe anatakapitisha uraiakuwili, vuta subra kidogo tu mambo yatenda sawa, au unataka kurudi kwa visa na kulipishwa midola lukuki Ngorongoro?
 
Naomba tukubaliane kutofautiana. Kama mwenzangu hauoni tofauti kati ya mwekezaji kwenye KUCHIMBA na mwekezaji kwenye uzaishaji wa nishati naona tuna tatizo kubwa la mtizamo. Au mwenzangu unadhani hizo 3 au 5% za madini haya ndiyo zitatupa utajiri wa kuinvest kwenye nyuklia? Mwenzangu unaupenda ubepari kwa kuangalia Manhattan, mimi nauchukia kwa kuangalia South Bronx! Wewe unaona maghorofa ya city centre Dar na vijishopping CENTRE vya shoprite mimi naangalia mbavu za mbwa zilizotapakaa ndani na nje ya Dar! Hatutaweza kukubaliana hata iwe vipi.

HII SASA PURE SIASA.

Kidumu chama cha mapinduzi.
 
BM, kuna watu wameenda shule vizuri tu! uwezo wao kuchambua mambo ni mpana sana, ukizingatia wako nchi zilizoendelea. wasiwasi wangu mambo yao hayaendi vizuri huko, unajua kubeba mabox kuna muda wake na hakuna altenative job. mawazo yao ccm iko nyuma ya misoto yao! sasa hata uwape mawazo mazuri vipi so long yako tz hawataelewa, karoho ka korosho kamewajaa.

Mawazo ya Fundi ni mazuri, kufikia 2010 umeme wa ethanol utakuwa unazalishwa na katani ltd pale tanga, waholanzi watakuwa wanazalisha umeme wa wind farm pale kilwa, wizara ya afya itaweka solar power zahanati zote nchini. songas wataanza kuzalisha gas za kutumia kwenye magari, TPDC wameshaanza kuandaa dispensing stations, magari ya gas yapo karimjee motors (toyota). Kiwira coal mine itakuwa inazalisha 450mw. plan iliyopo umeme wa nuclear utatumika kwenye iron smelter pale liganga na ziada itaingia grid ya taifa.

2009 Dar hapatakuwa na vipanya tena zitakuwa coaches tu kupitia mradi wa DART.

watanizangu waliomtimua mama kabaka kwenye harambee ya ujenzi wa shule hatutakuwa na namna ya kuwasaidia watoto wao, tumewaanzishia mashamba ya chai kwa kuwa wapiga debe hawatakuwepo tena stand za mabasi. Mkuu pasaka nitakuwa sopa lodge kwa mapumziko karibu sana tubadilishane mawazo.
 
plan iliyopo umeme wa nuclear utatumika kwenye iron smelter pale liganga na ziada itaingia grid ya taifa.

Asemavyo Eddy!

NDC Mtwara spatial development initiative coordinator Pascal Malesa says that the total capital investment for the Mchuchuma coal-to-electricity project is expected to be more than $600-million. The Liganga iron-ore project is valued at more than $1-billion and is expected to be privately financed.

Malesa explains that the power station will be integrated with the iron-ore project at Liganga, which is about 80 km away. The Mchuchuma coal project will supply coal for iron and steel manufacturing, create a power and industrial centre in the region, and thereby catalyse industrialisation in the country.

Asemavyo Malesa! Hicho kinu kiko wapi?Nani anaspin?

Matatizo vijana wa siku hizi mnaangalia bling za wakina 50 na mnasahau kuwa kuna upande mwingine wa habari! Sisi tulikulia nyimbo za wakina Robert Nesta Marley, Linston Kwei Johnson,Billie Holiday mashairi ya wakina Langston Hughes na maandishi ya wakina Frantz Fanon, James Baldwin n.k. kutoka huko! Hatuwezi kuelewana.

Naam kubeba maboksi kuna mwisho wake na wengi wangependa warudi kwenye nchi ambayo wanaweza kujivunia. Si hiyo mnayoitaka nyinyi. Ya summer bash mwezi wa sita (Tanzania ikiwa south of the equator) huko coco beach na kwingineko,kujibaragua kwa vishopping centre (si mall kama mnavyodhani) mchwara vya shoprite n.k. Tutataka tuendelee kuvuta hewa safi ambayo mwenyezi mungu ametujalia, kula mboga na matunda yaliyoota kiasili, kula nyama kutoka ng'ombe na mbuzi waliokuzwa kwa kula majani, kuogelea katika mito na bahari isiyojaa sumu na kuwaangalia wajukuu wetu wakijivunia kilicho chao na si kubabatikia wanavyoviona kwenye luninga. Ingawa hujanialika, sitaweza kufika huko Sopa Lodge wanakomwaga kinyesi kwenye ngorongoro. Kubeba maboksi hakulipi kiasi hicho.
 
FM swali zuri umeangalia life of mine ya liganga na mchuchuma? kuna mtu kanikonyeza eti wapigadebe watakula wapi mradi wa DART ukianza, kuna mradi wa biodiesel mkuranga na kisarawe, umeanza na ekari 9,000 za majario (pilot project) lengo ni kuwa na ekari 75,000 wataenda kung'olea ndago huko. wamiliki wa daladala tutawashauri wakanunue share pale dar stock exchange, watakuwa wamemiliki DART kwa namna moja.
 
BM, kuna watu wameenda shule vizuri tu! uwezo wao kuchambua mambo ni mpana sana, ukizingatia wako nchi zilizoendelea. wasiwasi wangu mambo yao hayaendi vizuri huko, unajua kubeba mabox kuna muda wake na hakuna altenative job. mawazo yao ccm iko nyuma ya misoto yao! sasa hata uwape mawazo mazuri vipi so long yako tz hawataelewa, karoho ka korosho kamewajaa.

Mawazo ya Fundi ni mazuri, kufikia 2010 umeme wa ethanol utakuwa unazalishwa na katani ltd pale tanga, waholanzi watakuwa wanazalisha umeme wa wind farm pale kilwa, wizara ya afya itaweka solar power zahanati zote nchini. songas wataanza kuzalisha gas za kutumia kwenye magari, TPDC wameshaanza kuandaa dispensing stations, magari ya gas yapo karimjee motors (toyota). Kiwira coal mine itakuwa inazalisha 450mw. plan iliyopo umeme wa nuclear utatumika kwenye iron smelter pale liganga na ziada itaingia grid ya taifa.

2009 Dar hapatakuwa na vipanya tena zitakuwa coaches tu kupitia mradi wa DART.

watanizangu waliomtimua mama kabaka kwenye harambee ya ujenzi wa shule hatutakuwa na namna ya kuwasaidia watoto wao, tumewaanzishia mashamba ya chai kwa kuwa wapiga debe hawatakuwepo tena stand za mabasi. Mkuu pasaka nitakuwa sopa lodge kwa mapumziko karibu sana tubadilishane mawazo.


Eddy:

Kuna watu wana kazi nzuri na kuna wanaopiga mabox, kama kipato chao ni cha halali hakuna tatizo.

Ukisoma posti nyingi hapa utaona kuna walio-disgruntled na system na viongozi. Hata kama kuna kitu kizuri kinafanyika nyumbani bado emotion zipo.

Pia wako wenye resentment. Kuna upendeleo wa nafasi kazi. Kuna upendeleo wa nafasi za kusoma. Watu wanauliza kwanini mtoto wa fulani yuko BOT.

Na kuna wengine wanachangia kwa kubadilishana mawazo na wanaona kuwa hupo uwezekano wa mtu kufanya vyake pale nafasi inapotokea.

Kwa maoni yangu binafsi. Ukiwa nje ya Tanzania hakuna kitu unachohitaji zaidi kama amani ya mawazo (peace of mind na ukiwa na resentment utapata uchizi wa kujitakia.

Tukirudi kwenye mada naelewa kabisa misimamo wa Nzokanhyilu na Fundi Mchundo. Wakiwa nje ya nchi wanaona vitu vingi vilivyokuwa-implemented kwa kutumia teknologia ambayo mtu yoyote mwenye akili timamu anaweza ku-copy na ku-paste. Na hawaoni sababu kwanini tusianze huko kwanza.
 
AFANA-LEIK Bin Maryam mswalie mtume mwanakwetu, si tunasikia Membe anatakapitisha uraiakuwili, vuta subra kidogo tu mambo yatenda sawa, au unataka kurudi kwa visa na kulipishwa midola lukuki Ngorongoro?

Pundit:

sijuhi ukweli huo lakini nadhani Kenya na Uganda wanakubali DUO. Nadhani nikiomba uraia wa Marekani pia naweza kuomba wa Uganda au Kenya na kuweza kutumia uraia wa Afrika mashariki.

Nikiweza kufanya hivyo kabla ya wao kubadilisha sheria nitatangaza kwenye magazeti kama political statement.
 
Duuh, kwahiyo siku hizi ndio tumebatizwa moja kwa moja kama wabeba maboksi sio? Lakini poa, ili mradi ki-tax tunacholipa kinasaidia kuhamasisha mabadiliko ya maendeleo katika sector mbali mbali. NHS ni bure, maana tax ya maboksi inafanya kazi.
Kubeba maboksi poa tu, ili mradi tukipiga kura, hakuna kuiba, na wazee hawang'ang'anii madarakani. Na hakuna kukatana mapanga ovyo na kukimbiza jirani na marungu na fimbo (halafu sijakata fimbo muda mrefu).
Huku wakiiba wanawekeza kwao, bongo tambarare, viongozi wakiiba wanaenda uswisi na marekani, wengine wanakatazwa kurudi nchini. Mmh bora nibebe maboksi kwakweli.

Asante Eddy kwa kushindwa hoja na kuleta vioja.
 
The Government will announce its controversial decision on whether to give the go-ahead for a new generation of nuclear power stations on Thursday, Downing Street said.

(Advertisement)
Prime Minister Gordon Brown's spokesman said the announcement would come in a statement to MPs from Business Secretary John Hutton.

The Cabinet is expected to discuss the move at its regular weekly meeting on Tuesday - when ministers are expected to agree that new stations should be built to secure Britain's future energy supplies.

Mr Brown's spokesman said: "John Hutton will make a statement to MPs and part of that will be the decision on whether or not to go ahead with the next generation of nuclear power stations."

Mr Brown's spokesman went on: "There has been a consultation under way. That consultation has now concluded and the Government now needs to make a decision in the light of that consultation, and it will be announced what that decision will be on Thursday."

The spokesman also confirmed that firms who build any new nuclear stations - if they are given the go-ahead - will be expected to fully fund the cost of future decommissioning of the stations.

He also said the energy companies would be expected to pay "their full share" of the cost of long-term management of nuclear waste.

The spokesman said: "If the Government does decide that new nuclear should be an option, then owners and operators would have to set aside funds to cover the full cost of decommissioning.

"We have always been clear that the full share of the costs of the long-term management and disposal of waste should fall on the operators.

"We have always been clear that if the Government decides new nuclear should be an option, operators should set aside funds for their full share of the cost of the long-term management of waste and the full cost of decommissioning."

Hii nimeiona leo huko Yahoo. Inaelekea hata huko kwa wenzetu hili suala halichukuliwi kirahisi kama wengine wanavyodhani. Gharama si kujenga na kuoperate tuu. Kuna kudecommission muda wake utakapofika. Na si ajabu decommissioning ikawa agahli sana maana unadeal na contaminated materials. Yote haya tunayaweza? Mnatutakia kweli mema?
 
I think the new strategic term for this has become Energy Independence(Uhuru wa Nishati) Mdahalo wa hivi karibuni wa chama cha demokrasia marekani iliwauliza ajenda zao kuhusu haya na wengi wao walikuwa tu na jibu moja kuu, Nuclear. Wamarekani hawajajenga kinu kipya kwa miaka 30 Uchina sasa hivi wanajenga vinu 40 kwa mkupuo!

Tutakubaliana moja ya sababu za kutojenga vinu hivi ni kutokana na ubwete wa mafuta(uliokwepo nyakati hizo) nguvu ya dola kuchimba,kusambaza na utumiaji. Mafuta haya, yanatokea sehemu mbili au tatu kubwa nako ni mashariki ya kati, Venezuela na(kapuni). Huko kote kunavurugu, cost zimeongezeka, kuna dalili pia mafuta ardhini yanapungua kwa kasi wanaona hakuna njia nyingine ya kujikwamua bali kuongeza matumizi katika sekta ya NYUKI Ingawaje hii itaweza kuchukua miaka kumi LINAFIKIRIWA. Mmoja wa wagombeaji urasi, Romney alionya lisiwe suala la kisiasa kukusanyia kura bali lishugulikiwe(action).

Ili kuwa na Uhuru wa Nishati,marekani wanatumia US$4 billion kwa mwaka katika Uhuru wa Nishati na Ufanisi wa Nishati Tanzania tunatumia kiasi gani?-Uelevu wangu ni kuwa miaka ijayo huu uhuru wa nishati waweza kuleta vurugu,zipo vurugu. Tunaelewa ni jinsi gani mataifa matatu marekani, China ,India yakuwa ndio yanongoza kwa kutumuia mafuta(crude oil/Petroli) kuendesha milipuko ya uzalishaji na ongezeko la nyenzo za kuendesha kuzalisha na kuboresha miundombinu na hatimaye kuboresha maisha ya jamii. Sisi uzalishaji(kwa mapana hapa) ndio huo unakurupuka, nishati tunahitaji, sasa hata kuliongelea hili jambo la NYUKI tusiliongelee?

Vyanzo vya maji vinakadiriwa kupungua baada ya 2025! Wadadisi wa mambo wanaona hii italeta vita kuu ya tatu, kugombania vyanzo vya maji safi, tunaingia kwenye makubaliano na nchi kubwa, matokeo yake hakuna nchi itaweza kusema maji ni ya kwake, maji yatakuwa ya walimwengu kwa hivyo basi ugavi wa umeme kwenye vyanzo hivi vinaweza kuwa kapuni...Kwa nini TUSIFIKIRIE NYUKI

hakuna kitu chechote duniani kisicho na madhara hii decommissioning of the stations baada ya mida yake ndio basi lakufanyiwa utafiti Tanzania na silo la kutia woga miongoni mwa wananchi kwani woga huu upo Ulimwenguni na wamejenga vinu hivyo! Kwa nini TUSIFIKIRIE?

Therefore we have an existing and substantive state of need to foster this strategy, under the conditions presented to us, Tanzania, think Nuclear Power.
 
Nzokanhyilu(kwenye mabano), with all due respect

Nijibu, kwa njia yoyote ile unavyoweza;
Najaribu....
a) Tanzania kuna kiasi gani cha coal/oil/gas? (kumbuka makampuni hayaji Tanzania kubahatisha, wanajua wamefuata nini).
Nikupotezeana muda tu...na mie ngoja nikuulize we vipi Umepewa v linki, una utaaluma kwenye eneo hili, unadai unaweza kufanya hayo mahesabu hakuna aliyebisha na hayo Tumegee vyovyote vile kwa nini tusilifikirie bila ya kutia woga!

b) Kwanini tunashindwa kutibu malaria, ambayo inaua zaidi ya ukimwi (lakini tunataka Nuclear)? Investment yake itakuwa cheap sana in comparison to Nuclear. A healthier nation is a smarter nation.

Sidhani kama tunashindwa na hili.

=Mienendo ya jamii-Imetokana na uchumi, serikali ndio ya kulaumiwa mbu wakitung'ata? Tunafuga na tunaendeleza tabia za kufuga, hebu niambie, Kumwaga maji nje ya dirisha lako nako mpaka serikali ikuambie hayo maji yanaweza kulea mbu? Watanzania wameelimishwa tunajua vyanzo vya gonjwa hili na tunaelewa sasa wapi kulikuwa na makosa, Vijidudu vimejizatiti madawa hayafai na ni kweli bajeti zetu hazikuwa zina dira kwenye Afya kama tunavyotaka au kutegemea...kushindwa kutibu isiwe sababu ya kutofikiri NYUKI. Nimesoma sehemu huko nyuma marekani walianza na haya miaka ya 50 unajua magonjwa mangapi yalikuwa hayatibiki huko kwa wakati huo. Je walisimamisha azma yao ya kuwa na NYUKI?

Ondoa woga!

c) kwanini Tanzania hatuwezi kutumia maji yamezunguka nchi nzima (tumwagilie kama wa-Israel wenye man-made lakes), lakini tunakimbilia Nuclear?

Hapa unazungumzia kilimo! ni kweli hatujaweza kuendeleza kilimo na tukumbuke wakulima wetu wameibiwa sana tu, wamechoka.Maji(safi) haya kama nilivyodokezea huko nyuma- siaajabu haya maji(safi) yasiwe ya soverign state Je una wasiwasi wa huu mjadala?

Kuvuna maji baharini kunahitaji nishati ya nguvu, NYUKI itaweza.

!
d)kwanini Mombasa port more efficient than dar?

Ukiritimba, Vurugu za kisisasa na jamii(mashariki ya kati na maziwa makuu) uzorotaji wa reli ya kati, Ufisadi, Ushuru usioleweka,Janguo!

e)kwanini wasomi wetu wa Ukraine tunawanyanyasa na visa?

Sijui. Kwanini?

Ukiweza kunijibu haya maswali convincingly(sana sana la 'a'), I will spend as long as it takes to prove to you that Nuclear is not yet the way forward. I will even go further, nitakuomba data fulani kuhusu ardhi ya Tanzania (sehemu unayotaka kiwanda/and deposit ya waste ikae), nitaichukua kama personal project, whether it takes 3 months or 6, nitatumia muda wangu wa free nikuandikie report nikitumia technology ya kisasa......hiyo report nitafanya bure (so long you supply the info i need).

Unajikanganya!

Until then, sina muda wa kubishana na watu wanaongea politically (lead by the heart) and not scientifically (lead by the brain) on this issue. Mambo ya kuwa na vision sijui nini......YES, wote tuna ndoto......tatizo ni kuzifikia bila misingi.
Sielewi hayo hapo juu...nieleweshe.

Kama unajua kuhusu Uholanzi kuwa ukanda wa upepo, kwanini hujui 'wind-tunnel' ni nini? google basi....labda nimetoa kwenye vi-link.


Mikwaruzano....Unasema kitu basi kidefaini tu watu wakuelewe, ukisema wind tunnel nani anakuelewa? manaake ulivyosema unadhihirisha taaluma yako nyingine katika midahalo nayo ni confutational, kuleta hisia za woga nakadhalika. Hiyo wind tunnel ina ukubwa gani, inatumia technoloji gani, Unajenga na nini? WEE VIPI?

Hapo juu hujasema chochote.

Angalia vizuri utaona.
Tuendelee.
 
Atanaye, with all due respect. Sikio la kufa halisikii dawa. Huko mnakong'ang'ania ni kubaya. Wasemavyo waswahili, yetu macho!
 
Back
Top Bottom