Uranium Mining Projects In Tanzania: Progress...

Fundi Mchundo,
Mimi naona spidi ya hawa watu wanaong'ang'ania Nuclear, ni kwamba wanatesti zali. Naona wanataka wapige dili ya Richimonduli nyingine, BOT au wasign contract kwenye hoteli huko Irani, halafu waharibu kila kitu, halafu watokee wa kina Zitto wengine wapige ngonjera bungeni kama kina Slaa.....etc etc.

Binti Maryam, unapiga makelele kuhusu fani usiyoijua bali kusoma tu kwenye vi-link, na umeng'ang'ania tu lazima tuwe na vision na kujiamini. Yes, hayo yote tunayo, we have brains for that, lakini we have messed up priorities. Mpaka sasa hujaeleza hiyo funding itatoka wapi, wakati bajeti yetu tunategemea 40% kutoka donors. Wasomi wetu ambao wako nchi kama Ukraine (Chernobyl) hawalipiwi fees etc. Wanafunzi kama hawa ndio wanahitajika kujenga nchi.....sasa sijui kama hatuwezi kuwalipia hawa, hizo pesa utatoa wapi za maabara za kibongo?? Huko huko Ukraine (former USSR)/Urusi wametengeneza helikopta aina ya Mi- (za kivita, ambazo zinaheshimika the world over mpaka leo hii) etc, na wanafunzi wetu wako katika anga za kujifunza lakini hatuwajali.

Nimekuomba uweke resources ya data, au kama kuna mtu ana data za bongo, tupige mahesabu. Hayo mahesabu nitakusaidia.

Ndugu yangu, one of the biggest markets as clean energy technology (I mean Renewable - more importantly) ni Wind Energy. Na katika nchi zinazoogopeka, na zitaogopeka in the future katika fani hii ni China na India. Katika miaka 10 ijayo utakumbuka maneno yangu. Hawa jamaa wanauwezo wa ku-bend rules ili wafike wanakofika ili mradi watatue tatizo lao la umeme. Na hii nina maanisha, watu nchi kubwa, open to the sea, na wako katika spidi kali ya ku-harness wind-energy. Kwa mfano huku UK, hawana uwezo mkubwa katika wind-farming, sababu ya sheria na kwavile nchi ni ndogo ku-harness wind energy. Believe you me, within 10 years, China and India will be exporting wind power. Sisi Pwani yetu kwanini tusiitumie kia-akili? (Wewe mawazo yako na wanaokutetea ni wale wale wanaotaka kuweka kiwanda cha chumvi katikati ya Serengeti sijui.....wakati sehemu hio hiyo ni major attraction ya wanyama na ndege aina ya Flamingo.....Maji yametuzunguka Tanzania, tunatumia vipi tusife njaa? Umeona wa-Israeli wanavyoichonga nchi yao? Feed our people, clean water, and we will think better....)

Nchi ndogo kama uholanzi, wako mbele katika sector ya Wind-energy na wanawekeza hela nyingi katika research hii kila siku (technology ipo, ila research ni kuongeza efficiency). Usipuuzie solar energy pia, wala ethanol. Solar energy hata ulaya inafanya kazi (na has nothing to do with the sun's strength as such), ingawa it has perhaps the poorest return on investment cos of expenses (basi inabidi tufikirie insentives za kushusha bei), the sun will always shine.........lets make it cheaper....

Nimekaa nakusoma unavyopiga soga kuhusu Nuclear energy, ukijua Nuclear energy ndio fyucha peke yake. Sijasikia ukifikiria tutaendesha magari vipi. Will you drive with mini-nuclear reactors in your car?? Haya, umefikiria hydrogen technology magari? Au hata ethanol?

Haya, Tanzania tuko kwenye bonde la ufa, na tuko prone na matetemeko ya ardhi. Jinsi unavyotupa nuclear waste, mara nyingi ni underground. Umeshawahi kusikia kitu inaitwa underground contamination.....especially ikingia kwenye underground channels za maji. Tatizo laweza tokea Tanga, watu wakaathirika Morogoro (theoretically). Binti Maryam, data kama hizi naweza kukupigia mahesabu kutumia technologia. Kumbuka uchafu wa nuclear, mpaka effect zake ziishe inaweza kuwa minimum miaka 10........maji yanasafiri ndugu yangu. Maji ya mlima kilimanjaro yaweza safiri yakatokea sehemu nyingine ya Tanzania usiamini!!!

Na hivi mnaongelea Nyumbu, kuna rafiki zangu wazungu/wadosi walikuwa wananicheka ki-utani......yaani wabongo mnaletewa hadi injini, mnashindwa kutengeneza magari mmh!!
 
Bila kuondoa taadhima, Nzokanhyilu

Kwa wanaong’ang’ania na wasionga’ang’ania is just a matter of Intellectual faculties. Kutesti zali ndio haswa ilikuwa ni azimio langu.

“Naona wanataka wapige dili ya Richimonduli nyingine, BOT au wasign contract kwenye hoteli huko Irani, halafu waharibu kila kitu, halafu watokee wa kina Zitto wengine wapige ngonjera bungeni kama kina Slaa...etc etc.”

Hii ni moja ya hizo faculty zako ambazo ni kutoa mzozo(kutofautiana mawazo ya bin marya na wanga’ang’aniaji) maoni, hukumu, na kupimana-pimana. Hakuna mabaya na haya lakini hakuna haja ya ku-politicize.

Kuhusu maryam kupiga makelele ndio faculty yake kwenye huu mdahalo sijui huko kwingine lakini hapa ameweza kuonyesha mantiki- amechangia, ameonyesha mapungufu pamoja na mlolongo wa mawazo, uchanganuo na hoja.

Unawezekana una undai na haya lakini ukumbuke kutesti zali sio kufanya zali.

Nafikiri ukiangalia hapo juu utaona umeweka data na huko nyuma huyu maryam ameweka vidata au vi link sasa hayo mahesabu umsaidie. Utusaidie na sisi wang’ang’aniaji. Tunaodai uwezekano upo-na kuafiki kwa upeo.

Vilevile naona bado tu umenga’ang’ania nakueleza visivyo. Una maaana serengeti ni sehemu ya attraction peke yake? Nafikiri wewe huyo huyo unataka ujenge hoteli kubwa tuu katikati ya serengeti. Eti watu waje kuona wanyama, basi vinyesi vyote vya kuendesha hoteli vitaishia kwa wanyama.

Kuenda kuvuna chumvi hakuhitaji magari moshi wala nini, au?

Uholanzi iko kwenye tambarare yenye upepo, Iko chini ya bahari. Upepo wa kutoka kaskazini magharibi ni mfano mzuri-hii inamaana wana chanzo kikuu cha kuwezekana kwa hii ‘Wind-energy’ siyo technology au efficiency ambayo inafanya wind energy ni eneo mbadala.
In Tanzania 'a plateau makes up the greater part of the country'. Hiyo Wind-energy itakuwaje basi?
Kwenye 'Nyuki'Tanzania napo tuna chanzo…Uranium, and what not…why not ‘think’ nuclear power?

Yakuendesha magari na nini nafikiri upo uwezekano wa kujadili, upo. Tujadili hili, tulifikirie hili, nalo ni ‘NYUKI’ (Asante bin maryam)

Fuata linki hizo ufungue upeo (visonary glands) jaribu hapa kwanza…www.howstuffworks.com/nuclear-power.htm

“Na hivi mnaongelea Nyumbu, kuna rafiki zangu wazungu/wadosi walikuwa wananicheka ki-utani......yaani wabongo mnaletewa hadi injini, mnashindwa kutengeneza magari mmh!”

Hii ndio mindset inatakikana kubadilika haswa ikija kwenye mijadala ya namna hii. Sasa hao wazungu/wadosi ni wa wapi? Kwani, ni nani hajafanya hivyo?(kupelekewa injini na kushindwa kutengeneza gari) sio ndio nyumbu hizo sasa iwe vipi? Technology advance zimetokana na mengi tu haswa baada ya vita kuu ya pili. Wizi huo (reverse technology) uliwaendeleza nchi nyingi. Nimesema wizi huo na mrejeo wa hao Wazungu/Wadosi. Kwa sisi kuletewa ni vizuri tatizo tumetumia vipi hii advantage kuendeleza (reverse technology) injini hizo?

Next time waambie tuliletewa injini na tumetengeneza nyumbu ‘ki-utani.’ Ungeonyesha uzalendo kidogo.

Cha muhimu katika mjadala huu ni ‘Think nuclear power’ ‘NYUKI’ tu.

Mchango wako una umuhimu, mahususi. asante. Tuendelee

Source zingine:Answers.com
 
Kwanza, kutesti zali in reference to Richmon...is a joke!! Lakini propaganda huwa zinaanza hivi.

Kuhusu figures, nimeomba za potential oil/gas/coal fields Tanzania. Mtu hata hujui nchi yako ina utajiri kiasi gani, umeshaanza kuwaza unataka kwenda teknolojia nyingine. Ndio haya haya, madini yanachimbwa na ndege kuondoka moja kwa moja kutoka machimboni, and you cant account for.

Hiyo Uranium ya bongo akiuziwa mtu, utajua kuna kiasi gani hapo? Ukipata 3% utaridhika eeh?

Ninachosema, Maryam anaongea tu, ila hajatoa figures zozote za resources na costs zake, na jinsi gani Tanzania itapata hizo pesa. Nakupa mfano. Hela iliyopotea BOT plus majengo ya Twin Towers estimate, unajenga kinu kizuri kabisa cha Nuclear. Thats approx $3.0 Billion. JE PRIORITIES ZIKO WAPI MTU AFIKIRIE KITU KAMA HICHO?

Ndugu yangu, kuhusu wind energy, yes ni eneo, lakini efficiency ya blades design na angle zinaleta tofauti i.e aerodynamics za blades (that is efficiency). Mfano, gari mbili za Ferrari zaweza kuwa na ingine sawa, na kila kitu, ila kwa mfano lile dude la mbele liwe-fofauti, yaani angle ya bumper lile la mbele......the smallest degree change, makes a great difference in speed. Hiyo ni efficiency ya aerodynamics. Je Tanzania kuna wind-tunnels ya kupima vitu kama hivi? Kuna softwares za kupima vitu kama hivi?

At no point nimeonyesha kuwa na ujinga wa ku-disturb eco-system ya Serengeti, so sijui wazo la hoteli umetoa wapi. Kama unaweza kuona kuna tatizo kuweka kiwanda cha chumvi.....kwani uone kwamba mimi nafikiria wazo zuri kuweka hotel sehemu hiyo hiyo? Think man. Dont make an argument for the sake of arguing.

Kuhusu energy, be it renewable or non-renewable, sina haja ya kufuata link hiyo. Najua nachoongelea. Hapa kila mwezi kuna lectures/presenations si chini ya 3 za energy proffessionals wana-discuss haya mambo. Not only nimepitia hii area, na nadeal nayo kila siku, ila pia nakutana na proffesionals ambao ni gurus katika area zao. Nina monthly subscription ya haya mambo, kinachonipita ni labda uvivu tu wa kusoma. Na nitatafuta article moja kuna kijana alikuja bongo kufanya thesis or something, na jinsi alivyo-conclude kwenye nchi kama Tanzania. Unajua, sometimes, tusiongee kama tunajua nchi yetu kuliko wengine. Kuna wazungu wanaijua nchi yako kuliko wewe na utajiri wake. Na hizo ndoto za Nuclear ndio kujichora.

Yaani BMaryam ameingiwa na sera za JKN kwa sana, anaweza kuongea na propaganda, kama sifa za waTanzania. Ila when it comes to doing, ndio mambo ya kuchemsha. Tufanye mambo simple, ndo tufikirie makubwa.

As for Nyumbu, sina cha kusifia (yes, nimeongelea Engineering za kuiba, ndizo wamefanya Wachina/Wahindi, sasa sisi tumefanya nini na Nyumbu??). Tunakufa na mbu kila siku, je lab zetu zinafanya nini? We unafikiri wazungu wangekuwa hawajapata solution? Tena ukute solution wanayo, ila sisi tunakufa ovyo miaka nenda rudi....unashindwa kuua mbu unataka Nuclear? Uzalendo naojisifia ni kwamba, Tanzania is a peacefull country, beautiful, we talk a lot with little substance and big smile. I am partially proud of that and embarrased at times!!
 
By the way,
Check makampuni makubwa yanavyojipanga na green-energy.

http://www.everythingsgonegreen.co.uk/category/technology/

Since this a good topic overall, naomba usome hapa na angalia hiyo video, its interesting;

http://www.everythingsgonegreen.co.uk/

au nenda hapa;

http://www.youtube.com/watch?v=bDsIFspVzfI&feature=related

Vitu kama hivi ndio inatakiwa tujiulize tumejipanga vipi? Na kama hatujui tuna oil/gas/coal kiasi gani sasa hivi (na tumebahatika kuwa nayo), tujue huko mbeleni tutalia, na tutajikuta tukiendelea ku-import energy technology........yaani kuna makosa mengine one can see them in the making. Kama madini tumechemsha, basi Energy, nchi zitapigana. Utajiri tunao, we need visionary people, sio waongeaji.
So inabidi watu wajipange kweli. Lakini kujipanga sio ukimbilie Nuclear.
 
Kwanza, kutesti zali in reference to Richmon...is a joke!! Lakini propaganda huwa zinaanza hivi.
I dis-agree to agree.

Kuhusu figures, nimeomba za potential oil/gas/coal fields Tanzania. Mtu hata hujui nchi yako ina utajiri kiasi gani, umeshaanza kuwaza unataka kwenda teknolojia nyingine. Ndio haya haya, madini yanachimbwa na ndege kuondoka moja kwa moja kutoka machimboni, and you cant account for.
Nilishanena huko juu
"Unawezekana una undai na haya lakini ukumbuke kutesti zali sio kufanya zali" na vile vile umeonyesha jinsi gani hauitaji hizo data kwa bin maryam and I quote...
Kuhusu energy, be it renewable or non-renewable, sina haja ya kufuata link hiyo. Najua nachoongelea. Hapa kila mwezi kuna lectures/presenations si chini ya 3 za energy proffessionals wana-discuss haya mambo. Not only nimepitia hii area, na nadeal nayo kila siku, ila pia nakutana na proffesionals ambao ni gurus katika area zao. Nina monthly subscription ya haya mambo, kinachonipita ni labda uvivu tu wa kusoma.

Sasa kwanini usitufanyie hizo mathematics(najua nachoongelea, nadeal nayo kila siku, nakutana na professional) ili kwa sie wanga'ang'anizi wa kufikiria tuelewe kwa nini haya siyo ya kufikiriwa. Mimi nafikiri uwezo upo kama wewe unabobea huko kwanini tusilifikirie?-Tunachojadili ni Strategies je kuna sayansi ya hili? Kama wewe umebobea kwenye dira, basi tuonyeshe hizo data zako

Hiyo Uranium ya bongo akiuziwa mtu, utajua kuna kiasi gani hapo? Ukipata 3% utaridhika eeh?

Nafikiri. lakini sio lazima kuuza tu tunaweza kutumia kwa ajili ya 'NYUKI'. Mchakato uliopo sasa haswa kwa nchi zetu hizi ni kuona kwamba hatuuzi malighafi tu-point taken!

Ninachosema, Maryam anaongea tu, ila hajatoa figures zozote za resources na costs zake, na jinsi gani Tanzania itapata hizo pesa. Nakupa mfano. Hela iliyopotea BOT plus majengo ya Twin Towers estimate, unajenga kinu kizuri kabisa cha Nuclear. Thats approx $3.0 Billion. JE PRIORITIES ZIKO WAPI MTU AFIKIRIE KITU KAMA HICHO?

Sikubaliani na wewe hapa. Hivo vilinki ndio vyanzo vyake, wewe kwa taaluma au ubobeaji wako huko tumegee hizo data za ki-NYUKI na sio scandal za BOT. Tuelewe tu sio Mtanzania aweke kipaumbele hili jambo bali afikirie wakati tunafikiria kuongeza ufanisi katika nyanja za miundombinu basi swala la NYUKI liwepo si vinginevyo unless I am missing a point.

Ndugu yangu, kuhusu wind energy, yes ni eneo, lakini efficiency ya blades design na angle zinaleta tofauti i.e aerodynamics za blades (that is efficiency). Mfano, gari mbili za Ferrari zaweza kuwa na ingine sawa, na kila kitu, ila kwa mfano lile dude la mbele liwe-fofauti, yaani angle ya bumper lile la mbele......the smallest degree change, makes a great difference in speed. Hiyo ni efficiency ya aerodynamics. Je Tanzania kuna wind-tunnels ya kupima vitu kama hivi? Kuna softwares za kupima vitu kama hivi?

I concur! kama sijakosea hii wind-energy umeleta wewe. What is a wind tunnel.
Hii mind set ndio mbaya zaidi, wachana na tunavyo argue. Yaani what does it take to create this wind tunnel? Mlolongo wako wa mawazo unaonyesha na kusambaza mind-set kwamba hatuwezi(kila kitu kikubwa kuliko uwezo wetu). Software? Please nzoka.

At no point nimeonyesha kuwa na ujinga wa ku-disturb eco-system ya Serengeti, so sijui wazo la hoteli umetoa wapi. Kama unaweza kuona kuna tatizo kuweka kiwanda cha chumvi.....kwani uone kwamba mimi nafikiria wazo zuri kuweka hotel sehemu hiyo hiyo? Think man. Dont make an argument for the sake of arguing.

Hapo ndipo tunapo gongana vichwa sasa, namimi naelewa huja sema narejea "Wewe mawazo yako na wanaokutetea ni wale wale wanaotaka kuweka kiwanda cha chumvi katikati ya Serengeti sijui.....wakati sehemu hio hiyo ni major attraction ya wanyama na ndege aina ya Flamingo....." Nilitumia mantiki hiyo na mwazo hayo basi, dah!

Yaani BMaryam ameingiwa na sera za JKN kwa sana, anaweza kuongea na propaganda, kama sifa za waTanzania. Ila when it comes to doing, ndio mambo ya kuchemsha. Tufanye mambo simple, ndo tufikirie makubwa.

Sikujua Bin Maryam mwanasiasa ,angalau ameonyesha ari mpya!

As for Nyumbu, sina cha kusifia (yes, nimeongelea Engineering za kuiba, ndizo wamefanya Wachina/Wahindi, sasa sisi tumefanya nini na Nyumbu??). Tunakufa na mbu kila siku, je lab zetu zinafanya nini? We unafikiri wazungu wangekuwa hawajapata solution? Tena ukute solution wanayo, ila sisi tunakufa ovyo miaka nenda rudi....unashindwa kuua mbu unataka Nuclear? Uzalendo naojisifia ni kwamba, Tanzania is a peacefull country, beautiful, we talk a lot with little substance and big smile. I am partially proud of that and embarrased at times

Tunakubaliana kwenye nyumbu. Tuendelee na uzalendo...
 
Mkuu Atanaye,
Kwanza hii thread imewekwa kwenye Siasa....na huwezi kuongelea maendeleo bila politics, we vipi? Wewe unataka uongelee umeme (power) lakini hutaki kutaja Richmond? We vipi?

I am a member of the Institute of Energy;
Institute of Energy
Sasa, sihitaji kubishana na kuhangaika na data hapa, if you can not answer the simplest of my questions........na soma unahitaji ufanye nini ili uwe member.

Nijibu, kwa njia yoyote ile unavyoweza;

a) Tanzania kuna kiasi gani cha coal/oil/gas? (kumbuka makampuni hayaji Tanzania kubahatisha, wanajua wamefuata nini).
b) Kwanini tunashindwa kutibu malaria, ambayo inaua zaidi ya ukimwi (lakini tunataka Nuclear)? Investment yake itakuwa cheap sana in comparison to Nuclear. A healthier nation is a smarter nation.
c) kwanini Tanzania hatuwezi kutumia maji yamezunguka nchi nzima (tumwagilie kama wa-Israel wenye man-made lakes), lakini tunakimbilia Nuclear?
d)kwanini Mombasa port more efficient than dar?
e)kwanini wasomi wetu wa Ukraine tunawanyanyasa na visa?

Ukiweza kunijibu haya maswali convincingly(sana sana la 'a'), I will spend as long as it takes to prove to you that Nuclear is not yet the way forward. I will even go further, nitakuomba data fulani kuhusu ardhi ya Tanzania (sehemu unayotaka kiwanda/and deposit ya waste ikae), nitaichukua kama personal project, whether it takes 3 months or 6, nitatumia muda wangu wa free nikuandikie report nikitumia technology ya kisasa......hiyo report nitafanya bure (so long you supply the info i need).

Until then, sina muda wa kubishana na watu wanaongea politically (lead by the heart) and not scientifically (lead by the brain) on this issue. Mambo ya kuwa na vision sijui nini......YES, wote tuna ndoto......tatizo ni kuzifikia bila misingi.

Kama unajua kuhusu Uholanzi kuwa ukanda wa upepo, kwanini hujui 'wind-tunnel' ni nini? google basi....labda nimetoa kwenye vi-link.

Hapo juu hujasema chochote.
 
Kwanza, kutesti zali in reference to Richmon...is a joke!! Lakini propaganda huwa zinaanza hivi.

Kuhusu figures, nimeomba za potential oil/gas/coal fields Tanzania. Mtu hata hujui nchi yako ina utajiri kiasi gani, umeshaanza kuwaza unataka kwenda teknolojia nyingine. Ndio haya haya, madini yanachimbwa na ndege kuondoka moja kwa moja kutoka machimboni, and you cant account for.

Hiyo Uranium ya bongo akiuziwa mtu, utajua kuna kiasi gani hapo? Ukipata 3% utaridhika eeh?

Ninachosema, Maryam anaongea tu, ila hajatoa figures zozote za resources na costs zake, na jinsi gani Tanzania itapata hizo pesa. Nakupa mfano. Hela iliyopotea BOT plus majengo ya Twin Towers estimate, unajenga kinu kizuri kabisa cha Nuclear. Thats approx $3.0 Billion. JE PRIORITIES ZIKO WAPI MTU AFIKIRIE KITU KAMA HICHO?

Ndugu yangu, kuhusu wind energy, yes ni eneo, lakini efficiency ya blades design na angle zinaleta tofauti i.e aerodynamics za blades (that is efficiency). Mfano, gari mbili za Ferrari zaweza kuwa na ingine sawa, na kila kitu, ila kwa mfano lile dude la mbele liwe-fofauti, yaani angle ya bumper lile la mbele......the smallest degree change, makes a great difference in speed. Hiyo ni efficiency ya aerodynamics. Je Tanzania kuna wind-tunnels ya kupima vitu kama hivi? Kuna softwares za kupima vitu kama hivi?

At no point nimeonyesha kuwa na ujinga wa ku-disturb eco-system ya Serengeti, so sijui wazo la hoteli umetoa wapi. Kama unaweza kuona kuna tatizo kuweka kiwanda cha chumvi.....kwani uone kwamba mimi nafikiria wazo zuri kuweka hotel sehemu hiyo hiyo? Think man. Dont make an argument for the sake of arguing.

Kuhusu energy, be it renewable or non-renewable, sina haja ya kufuata link hiyo. Najua nachoongelea. Hapa kila mwezi kuna lectures/presenations si chini ya 3 za energy proffessionals wana-discuss haya mambo. Not only nimepitia hii area, na nadeal nayo kila siku, ila pia nakutana na proffesionals ambao ni gurus katika area zao. Nina monthly subscription ya haya mambo, kinachonipita ni labda uvivu tu wa kusoma. Na nitatafuta article moja kuna kijana alikuja bongo kufanya thesis or something, na jinsi alivyo-conclude kwenye nchi kama Tanzania. Unajua, sometimes, tusiongee kama tunajua nchi yetu kuliko wengine. Kuna wazungu wanaijua nchi yako kuliko wewe na utajiri wake. Na hizo ndoto za Nuclear ndio kujichora.

Yaani BMaryam ameingiwa na sera za JKN kwa sana, anaweza kuongea na propaganda, kama sifa za waTanzania. Ila when it comes to doing, ndio mambo ya kuchemsha. Tufanye mambo simple, ndo tufikirie makubwa.

As for Nyumbu, sina cha kusifia (yes, nimeongelea Engineering za kuiba, ndizo wamefanya Wachina/Wahindi, sasa sisi tumefanya nini na Nyumbu??). Tunakufa na mbu kila siku, je lab zetu zinafanya nini? We unafikiri wazungu wangekuwa hawajapata solution? Tena ukute solution wanayo, ila sisi tunakufa ovyo miaka nenda rudi....unashindwa kuua mbu unataka Nuclear? Uzalendo naojisifia ni kwamba, Tanzania is a peacefull country, beautiful, we talk a lot with little substance and big smile. I am partially proud of that and embarrased at times!!

Nzokanhyilu:

Naomba nikusahihishe kwanza handler ninayotumia hapa ni BIN MARYAM (SON OF MARY(AM)).

Pamoja na kutumia handler yangu vibaya nitajaribu kujibu kwa kuuliza swali mafupi tu.

1./ Hivi wanaotupa misaada ya 40% wangesema nini kama pesa tulizotumia kujenga BOT twin towers tungetumia katika kununua KINU cha nyuki?

2./ Nchi zinazotoa misaada kwa Tanzania kama Denmark na Holland ni wazuri sana kwa katika mambo ya Wind-Mills kwanini wasiamue kutoa misaada ya technologia ya enegy ambayo ingesaidia sana maendeleo yetu?

3./ Wewe ni mtaalamu wa haya mambo kama unavyodai (I give you the benefit of the doubt). Kama Tanzania ingeacha na matumizi yasio na priority, je ungeshindwa kuwa baba wa nuclear age Tanzania?
 
Bila kuondoa taadhima, Nzokanhyilu

Kwa wanaong’ang’ania na wasionga’ang’ania is just a matter of Intellectual faculties. Kutesti zali ndio haswa ilikuwa ni azimio langu.

Hii ni moja ya hizo faculty zako ambazo ni kutoa mzozo(kutofautiana mawazo ya bin marya na wanga’ang’aniaji) maoni, hukumu, na kupimana-pimana. Hakuna mabaya na haya lakini hakuna haja ya ku-politicize.

Kuhusu maryam kupiga makelele ndio faculty yake kwenye huu mdahalo sijui huko kwingine lakini hapa ameweza kuonyesha mantiki- amechangia, ameonyesha mapungufu pamoja na mlolongo wa mawazo, uchanganuo na hoja.

Unawezekana una undai na haya lakini ukumbuke kutesti zali sio kufanya zali.

Nafikiri ukiangalia hapo juu utaona umeweka data na huko nyuma huyu maryam ameweka vidata au vi link sasa hayo mahesabu umsaidie. Utusaidie na sisi wang’ang’aniaji. Tunaodai uwezekano upo-na kuafiki kwa upeo.

Vilevile naona bado tu umenga’ang’ania nakueleza visivyo. Una maaana serengeti ni sehemu ya attraction peke yake? Nafikiri wewe huyo huyo unataka ujenge hoteli kubwa tuu katikati ya serengeti. Eti watu waje kuona wanyama, basi vinyesi vyote vya kuendesha hoteli vitaishia kwa wanyama.

Kuenda kuvuna chumvi hakuhitaji magari moshi wala nini, au?

Uholanzi iko kwenye tambarare yenye upepo, Iko chini ya bahari. Upepo wa kutoka kaskazini magharibi ni mfano mzuri-hii inamaana wana chanzo kikuu cha kuwezekana kwa hii ‘Wind-energy’ siyo technology au efficiency ambayo inafanya wind energy ni eneo mbadala.
In Tanzania 'a plateau makes up the greater part of the country'. Hiyo Wind-energy itakuwaje basi?
Kwenye 'Nyuki'Tanzania napo tuna chanzo…Uranium, and what not…why not ‘think’ nuclear power?

Yakuendesha magari na nini nafikiri upo uwezekano wa kujadili, upo. Tujadili hili, tulifikirie hili, nalo ni ‘NYUKI’ (Asante bin maryam)

Fuata linki hizo ufungue upeo (visonary glands) jaribu hapa kwanza…www.howstuffworks.com/nuclear-power.htm

Hii ndio mindset inatakikana kubadilika haswa ikija kwenye mijadala ya namna hii. Sasa hao wazungu/wadosi ni wa wapi? Kwani, ni nani hajafanya hivyo?(kupelekewa injini na kushindwa kutengeneza gari) sio ndio nyumbu hizo sasa iwe vipi? Technology advance zimetokana na mengi tu haswa baada ya vita kuu ya pili. Wizi huo (reverse technology) uliwaendeleza nchi nyingi. Nimesema wizi huo na mrejeo wa hao Wazungu/Wadosi. Kwa sisi kuletewa ni vizuri tatizo tumetumia vipi hii advantage kuendeleza (reverse technology) injini hizo?

Next time waambie tuliletewa injini na tumetengeneza nyumbu ‘ki-utani.’ Ungeonyesha uzalendo kidogo.

Cha muhimu katika mjadala huu ni ‘Think nuclear power’ ‘NYUKI’ tu.

Mchango wako una umuhimu, mahususi. asante. Tuendelee

Source zingine:Answers.com

Atanaye:

Fundi Mchundo anasema Tanzania ina watu wazuri tu waliosoma hayo na mambo na Nzokanhyilu anaseme anayafanya kazi katika mambo hayo. Hivyo suala la kumpata mtanzania mwenye technical know-how halipo (BABA WA NYUKI TANZANIA).

Suala linalosumbua ni la budget. Na hili litatuliwa kwa kupanga priorities zetu vizuri. Mtaalamu Nzokanhyilu anaonyesha kuwa ujenzi wa BOT ungetosha KINU KIMOJA.

Hivyo tatizo kubwa hapa sio pesa au wataalamu bali wala-nchi.
 
Nzokanhyilu:

Naomba nikusahihishe kwanza handler ninayotumia hapa ni BIN MARYAM (SON OF MARY(AM)).

Pamoja na kutumia handler yangu vibaya nitajaribu kujibu kwa kuuliza swali mafupi tu.

1./ Hivi wanaotupa misaada ya 40% wangesema nini kama pesa tulizotumia kujenga BOT twin towers tungetumia katika kununua KINU cha nyuki?

2./ Nchi zinazotoa misaada kwa Tanzania kama Denmark na Holland ni wazuri sana kwa katika mambo ya Wind-Mills kwanini wasiamue kutoa misaada ya technologia ya enegy ambayo ingesaidia sana maendeleo yetu?

3./ Wewe ni mtaalamu wa haya mambo kama unavyodai (I give you the benefit of the doubt). Kama Tanzania ingeacha na matumizi yasio na priority, je ungeshindwa kuwa baba wa nuclear age Tanzania?

Nisamehe kutumia jina lako vibaya. Ni usingizi na kukosea kidogo.
1./ Wangetucheka, wangetuzuia na kutupa sanctions. Vitu hivi hutangazi. unafanya kisiri, unashitukiza ukikaribia kumaliza. Au dili na warusi au wachina. Au wape madini wamarekani moja kwa moja, waambie wajenge hiyo Nuclear Plant.

2./ Priority yao sio wakufundishe technology. Priority ya wazungu ni kukufanya wewe uwategemee (soma Economic Hitman labda itakusaidia kuelewa). Ndio maana waChina na waHindi wanawasumbua vichwa, maana hawahitaji msaada wao. Pia, wanafunzi wetu wanapata scholarship za 'arts' nyingi....lakini engineering chache. Kuna watu wanasomea kilimo nje ya nchi, lakini bado tuko nyuma katika kilimo. Mzungu hakusaidii, jisaidie mwenyewe (read UKRAINE).

3./ Hapana, siwezi kuwa hivyo, siko involved na nyuki, ila kama naona opportunity hiyo ipo TZ, then najipachika sehemu huku for atleast 5 yrs (hii ni field iliyo na siri, na lazima upigwe checks kibao. wakati nasoma degree, pass yangu ya bongo wali-kataa kunichukua kama intern kwenye plant ya Nuclear, ila kuna washikaji waingereza waliingia kiulaini, maana they needed people). Ila naamini kuna waTanzania wengine lazima wako katika field hiyo, pia tuna Physicist wazuri tu around the world. Kuna mwalimu wa kibongo alinifundisha Physics, yuko Australia, mtu kama huyo si kawaida. Kama tuna mbongo NASA, basi sehemu zingine wapo tu, better equipped.

Ila ukija katika fani zingine za non/renewable sources, hizo naweza contribute moja kwa moja (na nina imani zaidi na hizi kwa Tanzania, taking into account our competence as peoples). Mimi nimespecialise katika sector moja, ila kutokana na foundation, ni rahisi kuingia sector yoyote (then give a year to feel specialised in that sector).

(Ukitaka kujua zaidi ni-PM).
 
Mkuu Atanaye,
Kwanza hii thread imewekwa kwenye Siasa....na huwezi kuongelea maendeleo bila politics, we vipi? Wewe unataka uongelee umeme (power) lakini hutaki kutaja Richmond? We vipi?

All protocol observed

Kwa kweli nilikuwa mgeni...inawezwa kuhamishwa kokote mradi mdahalo upo.

Mie vipi?:eek: NYUKI tu hapa. Umesema your reference to richmond was a joke. Nimekubali. ku politicize was just a reference to your characterization. Kama sikosei ulikuwa ukimweleza Fundi Mchundo. Hii ilikuwa by the way!.

I am a member of the Institute of Energy;
Institute of Energy
Sasa, sihitaji kubishana na kuhangaika na data hapa, if you can not answer the simplest of my questions........na soma unahitaji ufanye nini ili uwe member.
I remain unassuming. Kwa kweli sikutaka tuhangaishane kwa data kwa sababu tu nilivyoona toka huko juu, Unazo. Tumegee

Nijibu, kwa njia yoyote ile unavyoweza;

a) Tanzania kuna kiasi gani cha coal/oil/gas? (kumbuka makampuni hayaji Tanzania kubahatisha, wanajua wamefuata nini).
b) Kwanini tunashindwa kutibu malaria, ambayo inaua zaidi ya ukimwi (lakini tunataka Nuclear)? Investment yake itakuwa cheap sana in comparison to Nuclear. A healthier nation is a smarter nation.
c) kwanini Tanzania hatuwezi kutumia maji yamezunguka nchi nzima (tumwagilie kama wa-Israel wenye man-made lakes), lakini tunakimbilia Nuclear?
d)kwanini Mombasa port more efficient than dar?
e)kwanini wasomi wetu wa Ukraine tunawanyanyasa na visa?

Ukiweza kunijibu haya maswali convincingly(sana sana la 'a'), I will spend as long as it takes to prove to you that Nuclear is not yet the way forward. I will even go further, nitakuomba data fulani kuhusu ardhi ya Tanzania (sehemu unayotaka kiwanda/and deposit ya waste ikae), nitaichukua kama personal project, whether it takes 3 months or 6, nitatumia muda wangu wa free nikuandikie report nikitumia technology ya kisasa......hiyo report nitafanya bure (so long you supply the info i need).

Until then, sina muda wa kubishana na watu wanaongea politically (lead by the heart) and not scientifically (lead by the brain) on this issue. Mambo ya kuwa na vision sijui nini......YES, wote tuna ndoto......tatizo ni kuzifikia bila misingi.

Kama unajua kuhusu Uholanzi kuwa ukanda wa upepo, kwanini hujui 'wind-tunnel' ni nini? google basi....labda nimetoa kwenye vi-link.

Kwa haya mengine kama ulivyosema. Tutaendela. Sasa hivi nafikiri wapi kwa kupata 'NYUKI'(wanzuki):mad: Nafikiri.

Hapo juu hujasema chochote

Basi tuendelee na mdahalo, hujaona tu nilichokisema
 
Atanaye:

Fundi Mchundo anasema Tanzania ina watu wazuri tu waliosoma hayo na mambo na Nzokanhyilu anaseme anayafanya kazi katika mambo hayo. Hivyo suala la kumpata mtanzania mwenye technical know-how halipo (BABA WA NYUKI TANZANIA).

Suala linalosumbua ni la budget. Na hili litatuliwa kwa kupanga priorities zetu vizuri. Mtaalamu Nzokanhyilu anaonyesha kuwa ujenzi wa BOT ungetosha KINU KIMOJA.

Hivyo tatizo kubwa hapa sio pesa au wataalamu bali wala-nchi.

Na ndio haswa chanzo changu 'Intellectual faculties' Na nilinena huko mchango wake mahususi hapa.

Azimio langu ndio hilo la kutesti zali. Na kama kipaumbele naelewa, naelewa tulivyo najua fika hili ni jambo la kufikiria sasa na sio la kulifanya, kwa priority zilizokuwepo. I am stuck with the mind-set thing! Nafikiri kwanza ni kutoa uwoga uliokuwepo, hata mimi nilikuwa mwoga ....
"I came across this and(jaw-dropping) I thought I could share my thoughts. 'I don't know the coordinates, but I am sure one of the axis is evil!'
Hapo tu inadhihirisha woga niliokuwa nao(nikiwa hypothetical kwamba inawezekana)
Can we manage such an endeavor?... dukuduku langu la uwoga, majibu mengi na yote ni kuwa Tunafikiria makubwa hatuyawezi. Basi Wananchi kwanini tusifikiri Nuclear Power?

Tanzania think nuclear power na sio thinks nuclear power

Nawasilisha
 
How about recycling water used in Kidatu, Nyumba ya Mungu and other HEP plants for more production of electricity? Also, in areas semi-arid areas like Same and Dodoma where they have decent altitude and dry, windy conditions, wouldn't windmills be the preferred solution? How about Solar?

We can't have good monitoring on minerals and other natural resources that are being smuggled out of the country...how can we trust folks with Uranium and Plutonium? It's about time we go Green!!!
 
Anayeuliza mtaji uko wapi! ulipatikana jumatatu Australia Stock Exchange.

Mining explorer Mantra Resources Ltd with principal operations in Dodoma, on Monday demonstrated a continuing interest in uranium stocks on the Australian Stock Exchange, making its market debut at a 27.5 per cent premium to its offer price of 20 cents.

But after listing at 25.5 cents a share, the stock continued to rise and after several hours it was trading 12 cents or 60 per cent higher at 32 cents.

Capital thus raised would consolidate its operations in Tanzania where its principal operations are based, with direct and joint venture operations in a portfolio of uranium exploration tenements.

Its Mkuju River Project is in southern Tanzania, 470km southwest of Dar es Salaam, covering 3350 sq km prospective of uranium.
 
hivi vyote haviwezi kutegemea solar wala ethanol. uranium iko tele tu dodoma wala hatu-import kunaubaya gani tukiikodolea macho!

Eddy, ethanol, uranium vyote ni vyanzo vya energy. Ethanol pamoja na kuweza kutumika kuzalisha umeme inaweza kutumika kama fuel mbadala ya kuendesha engines kama magari. Hiyo technology mnayoing'ang'ania si ngeni na katika miaka ya kabla ya Azimio la Arusha ilitegemewa kuwa ingetatua matatizo yote ya nishati ya dunia. Lakini baada ya ajali za three-mile nachernobyl watu walianza kuiangalia upya. hapo ndipo nchi nyingi za ulaya (Sweden etc) zikaanza kupanga mikakati ya kujitoa na kuanza kutumia vyanzo mbadala na kuongeza efficiency katika matumizi ya nishati. Iligundulika kuwa kwa kuongeza efficiency kunaweza kupunguza haja ya kuongeza uzalishaji wa nishati. Hivyo majengo, magari,n.k. yakabanwa sana na standards za matumizi ya nishati. Wakati nyuklia inaanza kutatuliwa swala la disposal ya spent fuel iliaminiwa kuwa litatuliwa kirahisi. Kwa bahati mbaya mpaka sasa hivi utatuzi wa kudumu haujapatikana na ni nchi chache zilizokubali kuhifadhi haya mabaki. Kama uko makini utasikia malumbano yanayotokea wakati haya mabaki yanasafirishwa kutoka nchi moja hadi nyingine. Tatizo lingine lilojitokeza ni urahisi(kuliko wa kuvuna nishati) wa kutengeza bomu kutokana na hayo mabaki. Wasiwasi ni pale wasio na nia njema watakapoweza kuyapata na kuyatumia kulipua wenzio. Katika miaka ya hivi karibuni, kuongezeka kwa bei ya mafuta na gesi ambayo sehemu kubwa inatoka urusi na nchi za kiarabu, kuengezeka kwa dalili za global warming ndiko kulikofanya baadhi ya nchi zimeanza kuangalia upya nyuklia kama chanzo cha nishati. Hizi nchi ni zile ambazo haziwezi kukidhi mahitaji yao ya nishati kwa kutumia vyanzo mbadala ya mafuta, gesi na makaa ya mawe. Hutasikia nchi tajiri kwa nishati kama Norway ikizungumzia nyuklia. Ni wafaransa, wamarekani n.k. Lakini uoga juu ya athari zake bado uko palepale.

Sisi kama nchi ambayo ipo kwenye tropics tumebarikiwa kuwa na vyanzo mbadala vingi vya nishati vitakozoweza kukidhi mahitaji yetu ya nishati. Tuna upepo kama mtaalam alivyoainisha vyema, tuna jua ambalo bei ya mafuta inavyozidi kuongezeka nalo linazidi kuwa economical, bahari na mazao ambayo yanaweza si tu kutumika kuzalisha umeme, yanaweza kutoa fuel mbadala ya mafuta (Eddy, ndiyo hiyo ethanol). Nchi za ulaya na baadhi ya majimbo ya marekani(k.m. California) yameanza programu ya kujitoa kwenye matumizi ya mafuta (oil, gas) na kutumia kinachojulikana kama bio-fuels badala yake. Hizi bio-fuel zimeishaanza kuuzwa kwa wateja. Nchi kama cuba na yenyewe imeanzisha mpango mahususi kuzalisha nishati kutokana na zao lao la sukari. Brazil nao wanaelekeza nguvu zao zaidi kwenye bio kuliko nyuklia. hizi nchi zote zina teknolojia na kwa Brazil wana kinu tayari lakini wanaelekeza nguvu kwenye vyanzo mbadala. Sio wajinga hawa. Ni kupanga priorities vyema. Kwa kuwekeza kwenye bio unapanua wigo la watakaofaidika haswa wakulima wako,unaondoa utegemezi wa kuagiza fuel kutoka nje, na unachoiceya aina ya nishati utakayoitoa, dizel au umeme! Vile vile ni nishati safi, haichafui mazingira badala yake mazao haya ndiyo yanahitajika kupunguza carbon dioxide. sasa kwa nini sisi hatumo humo? Ni mind-set ya mtu mweusi kupenda bling. Kutaka kujivunia kuwa una kinu badala ya kusema kuwa umewawezesha wapogoro kujikwamua kwenye umasikini! Hata kama hicho kinu kukafanya kazi mwaka mmoja na kuzimwa kutokana na kukosa matengenezo! Si wapakistani wametutambua kuwa nasisi tumo?

Bin Maryam, moja ya matatizo yetu ni kupenda big projects. Kwa nchi kama ya kwetu, kungojea siku ambapo tutaweza kuviunganisha vijiji vyote kwenye grid ni kutokuwa makini. Tuangalie kila sehemu na potential zake. Watu wa Mbinga na maporomoko yao wapelekewe vyanzo vitakavyoweza kutumia hayo maporomoko kuzalisha nishati itakayowasaidia katika kilimo chao, watu wa Singida na Dodoma wapelekewe utaalamu wa kutumia jua na upepo uliojaa bwelele, wale wa Morogoro ambao wanalima miwa wapelekewe vyanzo vinavyoweza kutumia baggase n.k. Baadaye tutakapoweza kuwalink na grid wote wataweza kuchangia kwa kuuza surplus na kupunguza utegemezi wa chanzo kimoja. Miradi kama big dams (Stiegler n.k), nyuklia hatuviwezi kwa sasa hivi. Tuelekeze nguvu zetu kule tunakoweza na wengi wa wananchi wetu kufaidika. Kwa kuwasaidia wasukuma wa shinyanga kutumia bio gas kutokana na mifugo yao kunaweza kupunguza vifo vya bibi vizee wanaouawa kutokana nakuwa na macho mekundu mengi yanayosababishwa na kupuliza moto wa kuni! Hiki ndicho tunachodai wengine. Tuwe realistic, tuache kpenda mijisifa isiyokuwa na maana.

Mtaalamu Nzokanhyilu amedokeza kuhusu mistaken priorities zetu akitumia mfano wa lake Natron na uvunaji wa chumvi ya magadi utakaoathiri uhai wa flamingoes. Yuko sahihi sana , huu ni mfano wa jinsi tulivyo myopic. Baya zaidi, mradi huu uko kwenye jimbo la Mheshimiwa Slaa. Tunajivunia kuwa tunataka watalii milioni moja watembelee Ngorongoro bila kuangalia athari zake kwa eko-system. Tunajenga mihoteli ya kifahari mbugani na jirani zetu wakituonya kuhusu athari walizozipata tunasema wanatuonea gele. Tunajenga mahoteli kwenye coral reefs ( Sea Cliff, White Sand etc) na kukataa katakata maoni ya wataalam. Wotetunaona yanayotokea kwenye pwani ya Dar es Salaam. Ni hizi delusions of grandeur zilizotufikisha hapa. Sisi na Waafrika wengine.
 
Anayeuliza mtaji uko wapi! ulipatikana jumatatu Australia Stock Exchange.

Mining explorer Mantra Resources Ltd with principal operations in Dodoma, on Monday demonstrated a continuing interest in uranium stocks on the Australian Stock Exchange, making its market debut at a 27.5 per cent premium to its offer price of 20 cents.

But after listing at 25.5 cents a share, the stock continued to rise and after several hours it was trading 12 cents or 60 per cent higher at 32 cents.

Capital thus raised would consolidate its operations in Tanzania where its principal operations are based, with direct and joint venture operations in a portfolio of uranium exploration tenements.

Its Mkuju River Project is in southern Tanzania, 470km southwest of Dar es Salaam, covering 3350 sq km prospective of uranium.

Eddy, hawa wanataka kuchimba na siyo kuwekeza kwenye kinu etc. Hii uranium watakayoichimba ni kama dhahabu na mineral nyingine wanazozichimba na sisi tunabakiwa na mashimo tuu! Hakuna mtaji hapa!
 
Nchi zinazotoa misaada kwa Tanzania kama Denmark na Holland ni wazuri sana kwa katika mambo ya Wind-Mills kwanini wasiamue kutoa misaada ya technologia ya enegy ambayo ingesaidia sana maendeleo yetu?

Hawatoi kama hatujaomba!
 
Inawezekana kabisa. Mimi sioni hofu ya nini. Nishati inayotolewa na makaa ya mawe ina tatizo kubwa la 'pollution'. Maji nayo, pamoja na kwamba yanatoa umeme wenye gharama ya chini sana hayaji tunapoyahitaji (mvua).

Nishati ya jua bado ni ghali sana. Kuna sehemu za Tanzania ambazo zina upepo wa kutosha kuweza kutumia 'windmills' kutoa umeme lakini umeme huo bado utakuwa ni kidogo sana kulinganisha na mahitaji.

'Nuclear power' ni ghali kuanzisha lakini matumizi yake kwa muda mrefu ni nafuu na haiathiri mazingira (clean).

Bado kuna tatizo la kuhifadhi 'nuclear waste' inayotokana na kuzalisha nishati. Lakini kwa ujumla, ukipima faida na hasara za nishati ya 'nuclear' naamini faida ni kubwa zaidi.

Unafuu wa gharama ya nishati unaipa nchi 'competitive edge' inapokuwa kwenye ushindani wa kiuchumi wa utandawazi. Tuking'ang'ania vya zamani, ambavyo havina uhakika wowote, tutabaki wafanyakazi wa mataifa mengine.
 
Tatizo sio sisi tunaong'ang'ania vya zamani. Hii teknoloji mnayoibebea bango si ya leo. Imeanza kutumiwa toka fifties. Nyinyi wenzetu ndio mnakuwa single tracked. Mnakataa kabisa kuangalia alternatives ambazo zinajitokeza na kuanza kupewa umbele katika nchi za wenzetu mkikazania hii ambayo mnaona itatuweka kwenye chati. Hizi tunazozingumzia ndiyo wenzetu wanawekeza ilikuondoka kuwa tegemezi kwenye nyanja hii. Teknoloji hiyo ya nyuklia itatuweka kuwa tegemezi tukitegemea good-will ya wakubwa ili tuweze kuendelea nayo. Mimi sioni huo uhuru mnaodai utapatikana vipi kwa kutegemea chanzo ambayo ili tuianzishe itatubidi kukopa kwa wenye nazo, kukubali annual inspections n.k. Cutting edge resarch ni kwenye alternative energy sources na sio kama mnavyodhani kwenye hiyo nyuklia. Tusiwe kama North Korea, wana mabomu ya nyuklia lakini wanashindwa kuwalisha watu wao.
 
Back
Top Bottom