Urais wa Samia; Tumkunje angali mbichi

Urais wa Samia; Tumkunje angali mbichi

Rais ni Taasisi na Kibongo bongo na kwa Sheria zilizopo unaweza kumkunja wewe?

By the way hata panya ukim-corner akawa hana cha kufanya / kukimbilia usishangae badala ya kukimbia akaku-attack.

Kwahio hata huyu Mama akiwa pressurized sana usishangae akabadilika na kuwa worse kuliko unavyomuona sasa hivi (its just survival instinct)...
 
Ni fikra potofu kuwa unaweza kujenga uchumi huku ukiwa na sheria za hovyo zinazompa nguvu mtu mmoja kuamua lolote, siku yoyote, mahali popote, dhidi ya chochote.

Nani ataenda kuwekeza mahali ambapo mtu mmoja anaweza kutamka kuwa kuanzia leo wawekezaji wote wa nje fungeni miradi yenu kama hamtaki kufanya ninachotaka, na ikawa, na kusiwepo na yeyote wa kufanya chochote kwa namna yoyote.

Nilikuwa namheshimu sana Mama Samia, na hakika nilijenga imani kubwa kwake, kama walivyo Watanzania wengi, lakini kwa sasa naona tunahitajika kuwa makini naye kuliko kumwamini moja kwa moja.

Kuna watu Dunia hii, huwa wanaweza kufanya mazuri mengi lakini nyuma yake wakiwa na dhamira mbaya/chafu. Hawa watu ndiyo huitwa wanafiki. Na Mungu, hata yale mema waliyoyafanya huyanyima baraka. Lakini wapo pia wanaoweza kutenda mabaya wakiwa na dhamira na njema, Mungu huyatakasa yale matendo yao waliyoyatenda vibaya kwa sababu ya ile dhamira yao njema.

Samia, tayari ametenda mazuri kadhaa. Lakini msimamo wake juu ya kutotaka kuwa na mfumo bora wa kiutawala (katiba bora), ni kwa bahati mbaya ndani ya dhamira njema au yale aliyoyafanya mema yana nia ya kuficha dhamira mbaya?

Marehemu Magufuli aliwatesa na kuwaonea sana Watanzania. Tusikubali tena, awepo mwingine wa kutotendea vile au hata kukaribia kututendea hivyo. Hakikisho la hiyo, ni kupata katiba bora mpya.
 
Vipo viashiria kwa mbali vinaonyesha kuwa rais Samia ameanza kukizoea kiti (Hili ni jambo zuri), na pia ameanza kukipenda kiti (hili siyo jambo baya) ila ameanza kutamani kukilinda kiti kwa gharama yoyote (hili ni tatizo)

Tatizo ninaloliona ni kuwa hii dhana ya ya tatu ya kutamani kukilinda kiti kwa gharama yoyote ndiyo mwanzo wa yeye kuanza
We acha ujinga wewe! marais wote waliopita hawakukamilisha mchakato huo na hamkuhoji, iweje leo mama mumshinikize??? au kwa vile amewalealea hapo mwanzo sasa mnataka kudai kila mnachofikiria sio? acheni ujinga, fanyeni shughuli za maendeleo
 
Na nchi inahitaji usalama, afya, kuheshimiana, ajira, biashara, uchumi, miundombinu, uwajibikaji.

Hivi vitu ni zaidi ya katiba mpya

Kuna hoja muhimu unataka kuijenga lakini unapoteza mantiki. Huwezi kutenganisha maendeleo na katiba. Kama vile usivyoweza kutenganisha maendeleo na siasa.

Vyote hivyo ulivyotaja haviwezi kutafutwa nje ya katiba makini. Nchi huendeshwa kwa sheria na mifumo sahihi iliyo katika mzingo wa katiba makini ambayo ndiyo sheria mama.

Matumizi sahihi ya rasilimali za taifa huongozwa na kudhibitiwa na mfumo mzima wa sheria, taratibu, na taasisi zilizowekwa kikatiba. Bila hivyo ni vurugu. Viongozi wanaweza kufanya chochote kwa utashi wao tu bila kuhojiwa na kuishia kuharibu vipaumbele vya kitaifa na kuliletea taifa hasara kubwa.

Hivyo, Ili hoja yako iwe sawa, kwamba katiba mpya si muhimu sana wakati huu basi ni vyema uthibitishe kwamba Katiba iliyopo si mbaya; inatuwezesha kujiletea maendeleo kama tunavyotaka.
 
Kuna hoja muhimu unataka kuijenga lakini unapoteza mantiki. Huwezi kutenganisha maendeleo na katiba. Kama vile usivyoweza kutenganisha maendeleo na siasa.

Vyote hivyo ulivyotaja haviwezi kutafutwa nje ya katiba makini. Nchi huendeshwa kwa sheria na mifumo sahihi iliyo katika mzingo wa katiba makini ambayo ndiyo sheria mama.

Matumizi sahihi ya rasilimali za taifa huongozwa na kudhibitiwa na mfumo mzima wa sheria, taratibu, na taasisi zilizowekwa kikatiba. Bila hivyo ni vurugu. Viongozi wanaweza kufanya chochote kwa utashi wao tu bila kuhojiwa na kuishia kuharibu vipaumbele vya kitaifa na kuliletea taifa hasara kubwa.

Hivyo, Ili hoja yako iwe sawa, kwamba katiba mpya si muhimu sana wakati huu basi ni vyema uthibitishe kwamba Katiba iliyopo si mbaya; inatuwezesha kujiletea maendeleo kama tunavyotaka.
Mimi nimesema wapi katiba siyo muhimu ?

Punguza bangi.
 
Vipo viashiria kwa mbali vinaonyesha kuwa rais Samia ameanza kukizoea kiti (Hili ni jambo zuri), na pia ameanza kukipenda kiti (hili siyo jambo baya) ila ameanza kutamani kukilinda kiti kwa gharama yoyote (hili ni tatizo)

Tatizo ninaloliona ni kuwa hii dhana ya ya tatu ya kutamani kukilinda kiti kwa gharama yoyote ndiyo mwanzo wa yeye kuanza kupiga danadana hitajio la msingi la wananchi juu ya namna wanavyotaka nchi yao iongozwe, yaani hitajio la katiba mpya. Hii ni ishara mbaya kabisa ya kiuongozi, kwa sababu inaonyesha dhahiri kuwa na yeye hana tofauti na watangulizi wake ambao Ukweli wanaujua kuwa katiba hii siyo miafaka katika mazingira ya sasa ya kisiasa na kiuchumi, lakini waliendelea kuikumbatia tu kwa sababu uwepo wa katiba mpya unaweza kutoa HAKI nchini ambazo zinaweza kupelekea wao kushindwa chaguzi na wakakosa means za kulazimisha ushindi wao binafsi na chama chao cha CCM.

1. Kauli ya rais hakosei
Samia alitoa kauli hii, wengi tunaweza kuichukulia juujuu, lakini hii kauli inamaana kubwa mbaya sana, ina maana kuwa yeye anaweza kufanya lolote katika nchi na litakuwa sahihi tu, asihojiwe!. Ipo haja ya kumkatalia kwa nguvu rais pindi tukiona anakwenda chaka, tumueleze wazi kuwa kwenye suala kadha wa kadha hauko sahihi, mfano ni katika suala hili la kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ya wazi nchi mzima kinyume cha sheria.

2. Kupiga danadana katiba mpya
Kauli ya Samia kuwa suala la katiba mpya tumpe muda ajenge uchumi kwanza, ni kauli iliyopakwa mafuta kumaanisha kuwa licha ya hilo suala la katiba mpya kuwa ni la msingi kwetu sisi wananchi lakini kwake yeye kama rais siyo la kipaumbele, na huenda anamaanisha kuwa halitaki ila tu anatumia "tafsida" ili kumpaka chura lipsitiki. Hapa binafsi nina maswali yafuatayo kwa Samua mwenyewe.

a) Kama anajua kuwa uchumi ni kipaumbele kuliko Katiba mpya, kwa nini yeye binafsi alishiriki kikamilifu kwenye mambo ya katiba mpya mwaka 2013 kwa kuomba nafasi ya kuwa Makamu mwenyekiti wa bunge la katiba?, Kwa nini asingejiweka pembeni na masuala ya katiba mpya wakati huo na badala yake kushauri serikali ijikite katika yjenga uchumi?

b) Yeye sasa hivi ni mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi, na Chama kiliweka suala la katiba mpya kwenye ilani yake ya mwaka 2015, Kama Samia anadhani Uchumi hauwezi kujengwa sambamba na katiba mpya, kwa nini alizunguuka nchi nzima nwaka 2015 kuinadi Ilani hiyo yenye kuelezea kuwa uchumi utajengwa na katiba mpya itapatikana?

3. Rai yangu kwa rais Samia, Kumbuka kuwa mchakato wa katiba mpya ndiyo ulioinua nyota yako na ndiyo utakaoizima
Kabla ya mchakato wa katiba mpya 2013-2014 hakuna aliyekuwa akimjua Samia kama mwanasiasa wa kiwango cha Kitaifa, Ila uongozi aliouonyesha mwaka huo katika bunge ka katiba ndiyo uliompa nafasi ya kutambulika kitaifa na hata kwenye system kuwa huyu anafaa. Sasa ni ajabu sana kwa mtu ambaye alishiriki kwenye jambo muhimu kama hilo kuanza kuleta excuse ya kuliahirisha. Yaani kwenye hili la suala la Katiba mpya kitu ambacho rais Samia anakifanya ni sawa na mwanamke anayesaka mtoto halafu baada ya kupata mimba anataka kuitoa!. Hoja ya katiba mpya ndiyo mimba, na katiba ndiyo mtoto mwenyewe!. Tunataka Samia akamilishe kazi aliyowahi kushiriki kuifanya, kazi iliyoibua nyota yake ya kiuongozi nchini, yaani kuwapatia wananchi katiba nzuri na bora

4. Rai kwenu Wazalendo wa nchi hii
Ndugu zangu, tusikubali nchi hii kuwa ya kidikteta, tunapoona chembechembe za udikteta ikiwa ni hata kauli ya kuteleza ya kiongozi tusikae kimya, maana tukikaa kimya wataanza kuamini katika invincibility kitu ambacho ni illusion na mdogomdogo wataanza kujenga tabia za udikteta. Kwa hiyo tumkunje rais Samia angali mbichi kabla hajanogewa sana na mamlaka makubwa anayopewa na katiba hii. Tukimuacha akakomaa katika ulevi wa madaraka utokanao na katiba hii atatuzingua sana huko mbeleni maana wahenga walisema, Power corrupts absolute power corrupts absolutely.

5. Mwisho kabisa hoja ya katiba mpya haiwezi kufa mpaka katiba mpya ipatikane
Na hili suala wadau tumeshalijadili sana kuwa.

1. Katiba mpya ni takwa la kisheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2012, tunataka rais atekeleze sheria.

2. Katiba ya sasa ya Muungano na ya Serikali ya Mapindizi ya Zanzibar vinapingana, kwa mfano kwenye muundo wa serikali ya SMZ, Masuala ya mahakama ya rufani etc. Hizi katiba mbili haziko in sync. Sasa hatuwezi katika nchi kuwa na katiba inayopingana na katiba nyingine, huo ni uendawazimu

3. Katiba mpya imewahi kuwemo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM, Sasa haiwezekani chama kilekile kilichowahi kunadi ilani, kitumie ahadi hiyo kupata kura halafu baada ya hapo kikatae ahadi yake ya kwenye ilani yake kwa hoja kuwa ahadi yake ya mwanzo ilikuwa inachelewesha kujenga uchumi, kwa hiyo eti sasa tujenge uchumi kwanza huo ni ulaghai wa wazi mbele ya wananchi, tunataka CCM iwe na soni!.

4. Katiba mpya iliyo bora zaidi ndiyo itakayolinda Haki zetu, uhuru wetu binafsi, itasimika fairness katika nchi, na itatulinda dhidi ya uwezekano wa kupata kiongozi dikteta akatuvuruga!.
Na bado..tulia iingie vzurii...ulipokuwa unafurahia kifo cha jpm..ulizan alieingia ni mboe sio..kalagha bahooo...missile of the toilet.
 
Mimi nimesema wapi katiba siyo muhimu ?

Punguza bangi.

Kwanza tuheshimiane. Lugha za “bangi” haziko katika ulimwengu wangu. Nimekuandikia vizuri tu. Umedai kuwa masuala ya maendeleo (umeorodhesha) NI ZAIDI ya “katiba mpya”.

Nilichokuambia ni kuwa, kwanza, huwezi kutenganisha masuala ya maendeleo na “katiba makini”. Nikashauri kuwa ukithibitisha kuwa katiba iliyopo inakidhi maendeleo basi hoja yako itakuwa ok.

Sikusema kuwa umesema katiba si muhimu. Umeongea kuhusu “katiba mpya…”

Btw huwa sishiriki mijadala ya kusemeana ovyo. If you’re not happy with my views just ignore me. Narudia tena, tuheshimiane.
 
Kwanza tuheshimiane. Lugha za “bangi” haziko katika ulimwengu wangu. Nimekuandikia vizuri tu. Umedai kuwa masuala ya maendeleo (umeorodhesha) NI ZAIDI ya “katiba mpya”.

Nilichokuambia ni kuwa, kwanza, huwezi kutenganisha masuala ya maendeleo na “katiba makini”. Nikashauri kuwa ukithibitisha kuwa katiba iliyopo inakidhi maendeleo basi hoja yako itakuwa ok.

Sikusema kuwa umesema katiba si muhimu. Umeongea kuhusu “katiba mpya…”

Btw huwa sishiriki mijadala ya kusemeana ovyo. If you’re not happy with my views just ignore me. Narudia tena, tuheshimiane.
Ni wapi huko katiba unayoita makini imeleta maendeleo ?
 
Samia anatwambia anazuia siasa ili kukuza uchumi, hatuambii kipindi cha Nyerere na Mwinyi ambapo siasa za upinzani zilikuwa hakuna uchumi ulikuwa unakua kwa asilimia ngapi? Halafu alinganishe na Kipindi cha Mkapa na Kikwete ambapo kulikuwa na uhuru wa kisiasa kwa vyama vya siasa nchini kufanya siasa, Uchumi ulikuwa unakua kwa asilimia ngapi? — Ukiondoa doa la ufisadi, Kiufupi mafanikio ya ukuaji wa uchumi ya Mkapa na Kikwete combined ni ya kupigiwa mfano kwa watawala wajao, Sisi tunataka Katiba mpya ili kupunguza ufisadi wa kimadaraka na ufisadi wa mali na rasilmali za umma!, ili ukuaji wa uchumi ulrte tafsiri kwenye maendeleo ya taifa!
 
Back
Top Bottom