Urais unamfaa January Makamba kwa sasa

Mnasaidiana kutafuta wateja wa Tanesco Dubai eeh!
Mchukuwe akawe mume wa mama yako ili awaongoze kwenu.
Shida yako umekalili ukisikia wawekezaji unawaza ufisadi. Ukiwakalilisha ujinga wajinga wanakuwa wajinga zaidi maana hawajui kureason pia ni wavivu wa kufanya utafiti, uchumi wa China na nchi za magharibi unakuwa kwa kasi kutokana na wawekezaji (Private sector), inshu ungejikita ni namna gani mikataba ikawa wazi pamoja na faida kwa nchi yetu ningekuelewa.
 
Huyo anayeteua watu kutoka kwenu wa dini moja humuoni?
Kwani hawana uwezo? Au ni chuki zako binafsi. Mm mwenyewe ni mkristo ila naona ni fresh tu kama mtu anauwezo akipata bahati ya kuteuliwa ni fresh tu.
 
January Makamba kwa mtazamo wangu namuona ni mtu ambaye yupo smart sana kichwani, ana busara, mtulivu, si mpenda sifa bali ni mchapa kazi, si mtu wa media sana na hakurupuki kataka maamuzi yake bali ni mtu wa kujiridhisha Kwanza hivyo anafaa sana. Huyu anawajua matajiri vizuri.

Antony Mutaka anafaaa sana kuwa waziri mkuu wake mana ana UTU, mchapakazi, mbunifu, katika utendaji wake na speech zake huwa anajikita namna ya kuwakwamua watu wa kipato cha chini, ni mtu anayejitoa sana na pia hutoa maamuzi si kwa kukurupuka bali kwa kujiridhisha. Huyu anawajua watu wa hali ya chini vizuri.

Mawaziri ambao watatakiwa wawateue ili utendaji wa kazi uwe vizuri ni Paul Makonda, Bashe, Kalemani, Nape, prof Mbalawa, Lukuvi, Biteko, Dr. Bashiru, Prof Asssad, Zitto Kabwe, James Mbatia, Jussa, Fatma Karume, Jafo, Aweso, Kyombo, Ummy Mwalimu, Uttoh, Mafuru, Mchechu Prof. Lipumba na prof Kabudi.

Muunganiko mzuri wa watu masikini na matajiri ndio utaleta tija kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu. Iwapo patakuwa na ubaguzi au kuonewa kwa kundi mojawapo nchi yetu itakuwa bado tupo kwenye safari ndefu ya mafanikio makubwa ya kiuchumi.
nakuona katika ubora wa pumba zako khaaa ety makamba huyu huyu anayekata umeme kila sku au👹👺
 
January Makamba kwa mtazamo wangu namuona ni mtu ambaye yupo smart sana kichwani, ana busara, mtulivu, si mpenda sifa bali ni mchapa kazi, si mtu wa media sana na hakurupuki kataka maamuzi yake bali ni mtu wa kujiridhisha Kwanza hivyo anafaa sana. Huyu anawajua matajiri vizuri.

Antony Mutaka anafaaa sana kuwa waziri mkuu wake mana ana UTU, mchapakazi, mbunifu, katika utendaji wake na speech zake huwa anajikita namna ya kuwakwamua watu wa kipato cha chini, ni mtu anayejitoa sana na pia hutoa maamuzi si kwa kukurupuka bali kwa kujiridhisha. Huyu anawajua watu wa hali ya chini vizuri.

Mawaziri ambao watatakiwa wawateue ili utendaji wa kazi uwe vizuri ni Paul Makonda, Bashe, Kalemani, Nape, prof Mbalawa, Lukuvi, Biteko, Dr. Bashiru, Prof Asssad, Zitto Kabwe, James Mbatia, Jussa, Fatma Karume, Jafo, Aweso, Kyombo, Ummy Mwalimu, Uttoh, Mafuru, Mchechu Prof. Lipumba na prof Kabudi.

Muunganiko mzuri wa watu masikini na matajiri ndio utaleta tija kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu. Iwapo patakuwa na ubaguzi au kuonewa kwa kundi mojawapo nchi yetu itakuwa bado tupo kwenye safari ndefu ya mafanikio makubwa ya kiuchumi.
 
Wana JF kiukweli mimi sio Makamba sina urafiki nae wala simpigii kampeini mana uchaguzi bado upo mbali sana na mama anaupiga mwingi tu hivyo tufanye kazi kwa bidii tu, Mimi sio mtu wa siasa kivile ila natoa mtazamo wangu pamoja na wa vijana walio wengi wasomi kwa nature ya raisi wanayemuhitaji kiukweli huyu jamaa wanamkubali sana he is very smart. Tatizo la wabongo mnapenda watu waongo, wasiofuata utawala wa sheria, wapenda sifa, miungu watu, muitwe wanyonge(wajinga) ndio muhisi huyo ndiye raisi.
Wewe ni January, unamtumiaga hadi dada yako kutapeli watu.
January ni tapeli
 
Mwandishi wa hii Makala ni mkamba mwenyewe!
Kwa ufupi hii familia ya makamba kuanzia baba yao sio watu wa kuamini, kwa ufupi hawana ethics za utawala kabisa!
 
Mwandishi wa hii Makala ni mkamba mwenyewe!
Kwa ufupi hii familia ya makamba kuanzia baba yao sio watu wa kuamini, kwa ufupi hawana ethics za utawala kabisa!
Si kweli brother! Mm ni mtu wa kawaida sana si mwanasiasa ni mtu wa kawaida na ni mkulima mpambanaji.
 
Huu Uzi najua haukuandikwa na January, lkn utakua umeandikwa na mpishi au mfanyakazi wa ndani wa January.
Hata hivyo kwa waliopo Sasa sioni mwingine zaidi ya huyu homeboy.
 
Mawaziri ambao watatakiwa wawateue ili utendaji wa kazi uwe vizuri ni Paul Makonda,Kalemani, Nape, Biteko, Dr. Bashiru, Zitto Kabwe, James Mbatia, Jafo, Ummy Mwalimu, prof Kabudi.

HAWA LABDA UENYEKITI WA KIJIJI HUKO KONGWA NDANINDANI
 
Kujadili mtu (individual) kwamba ndiye anayefaa kuwa Rais maana yake ni kupuuza uhuru wa Watanzania kuchagua Rais wao.

Kuna ujinga ulioenea kuwa Rais anawekwa na “system”; kwamba huwezi kuachia wananchi wachague Rais; eti watakosea! That’s pure BS! Hata kukosea ni haki ya kidemokrasia ya wananchi. Muhimu ni mfumo uwawezeshe kusahihisha makosa yao kwa wakati muafaka. Ndio nchi za maana zilivyo.

Kwanza hiyo “system makini” kwenye nchi iliyojaa mazuzu kwenye taasisi/vyombo vya dola unaipataje? Halafu ya nini? Ije kuteua Rais atayekuwa “mungu”? Yaani tunapenda sana utumwa sisi (subservience)? Kuwa chini ya udikteta wa vikundi maslahi vya chama tawala?

Uchaguzi huru na wa haki unawapa wananchi uwezo wa kuchagua na kuwajibisha viongozi wao. Rais hatakiwi kuwa na absolute power. Hayo ni mambo ya banana republics. Akifanya ndivyo sivyo kuna hatua za kibunge za kumuondoa. Zipo na za kisheria vile vile.

Ni aina ya ushirikina na uzuzu kujadili “individuals” na “mysterious systems” kama mikakati muhimu ya kisiasa nchini. Ni kama zile “kamati za ufundi” za klabu za mpira.
 
hatutaki mtu mwizi ,naona unataka kuongozwa na mtu kilaza labda mpatie familia yako aiongoze wewe mtoa mada

 
WASIFU

January Yusuph Makamba, amezaliwa mwaka 1974 tarehe 28 mwezi januari, katika mkoa wa Siginda akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wanne.

Ni mwanasiasa nguli nchini Tanzania katika Chama tawala cha Mapinduzi CCM, amekuwa na kulelewa katika misingi ya siasa za CCM, baba yake amekuwa Katibu Mkuu katika chama hicho. ELIMU na KAZI Amesoma katika shule ya msingi Handeni , na sekondayi amesoma katika shule ya Galanos, kisha elimu ya kidato cha tano ameipata katika shule ya Forest Hill ya Morogoro.

Amesoma katika chuo cha Quincy College kilichopo Marekani, kabla ya kwenda kuchukua Shahada ya Uzamili ya masuala ya usuluhishi katika chuo cha George Mason mwaka 2004.

Alipohitimu elimu yake alirejeea nyumbani na kuanza kufanya kazi katika Wizara ya Mambo ya nje kama ofisa utumishi wa mambo ya nje wakati huo msatafu Jakaya Kikwete akiwa ndiye Waziri katika Wizara hiyo. Mwaka 2005 alikuwa nmstari wa mbele katika kumpigia kampeni Kikwete katika uchaguzi Mkuu wa urais, aliyeibuka na ushindi wa asilimia 80.

Alichaguliwa kuwa msaidizi binafsi wa rais, nafasi aliyoitumikia kwa miaka mitano. SIASA Mwaka 2010 aligombea nafasi ya Ubunge katika uchaguzi Mkuu jimbo la nyumbani kwao Bumbuli, alipita bila kupingwa, amehudumu toka 2010 hadi sasa. Amekuwa pia mjumbe wa kamati ya Nishati na Madini ya Bunge la kumi. Mwaka 2011 alichukua nafasi ya Bernad Membe ndani ya CCM akawa Katibu wa masuala ya Siasa na uhusiano wa Mataifa, alihudumu hadi mwaka 2012.

Alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya Taifa NEC. Mwaka 2012 aliteuliwa tena kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia. Januari ni mwepesi katika masuala ya jamii, mwaka 2014 alikubali wito aliotumiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, wa kushiriki katika tamasha la kueilimisha jamii juu ya ugonjwa wa Fistula ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wagonjwa wa Fistula, aliweza kuchangia kiasi cha Milioni Moja kuwasaidia wagonjwa hao.

Mwaka 2015 alitangaza nia ya kugombea urais, lakini suala hili alianza kuliongelea tangu mwaka 2014 na anatajwa kuwa mgombea wa kwanza kutangaza nia yake ya kugombea. Katika Kampeni za Urais wa mwaka 2015, Makamba alizindua kitabu kilichoandikwa na Fr. Karugendo, kilichokuwa na maswali 40 aliyoulizwa , jina la kitabu lilikuwa ni "Mazungumzo na Januari Makamba. Mchakato wa kura za maoni wa CCM ulimteua Hayati Magufuli kuwa mgombea atakaye gombea nafasi ya Urais, na hapo Makamba ilimpasa kurejea Jimboni mwake alipochukua fomu tena kutetea kiti chake cha uwakilishi.

Aliteuliwa kuwa Waziri wa Muungano na Mazingira mwakanafasi aliyohudumu hadi mwaka 2020. Akiwa Waziri alifanikiwa kutokomeza matumizi yamifiku ya olastiki nchini kote. Kwasasa kiongozi huyu ni Mbunge katika jimbo hili hilo la Bumbuli, na anatajwa kuwa kiongizi mwenye weledi mkubwa katika kutatua masuala mbali mbali.

Tarehe 12, septemba 2021, katika uongozi wa awamu ya sits chini ya Rais Samia, Makamba anarejea tena katika Baraza la Mawaziri kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati akichukua nafasi ya Dr. Medard Kelemani.
 
Back
Top Bottom