Urais ni kuwa msingi mbovu katika msingi wa maendeleo Kama watangulizi wake wote, JPM si msingi sahihi

Whitesmith

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
386
517
Ni muhimu sana tukaimarisha biashara kati yetu sisi waafrika, ni vyema tukayafikia masoko yetu kwanza, kuunganisha watu wetu kufanya biashara,ni mara nyingi tunapozungumzia masoko ya nje basi watu wengi wahamisha fikra zao kulenga masoko ya Ulaya, Marekani, nk hii si fikra sahihi sana, kuna masoko makubwa yenye uhitaji wa bidhaa zetu, masoko yenye ushindani mdogo km DRC, Uganda, Burundi, Kenya, nk. Sasa haya masoko tunayafikiaje? Kuna Reli (TAZARA),Anga(ATCL), majini. Tumeona juhudi kubwa ya Rais kuyafufua mashirika mengi ya Umma. Tunamuomba muheshimiwa JPM haya anayoyafanya mazuri kama dira na mwelekeo wetu km nchi ayajenge haya katika MISINGI isiyo bomoka ili yabaki kuwa mambo ya msingi katika MSINGI wa maendeleo yetu. Tumeona mambo ya msingi katika misingi ya maendeleo yalivyochezewa nakuharibiwa mfano; ATCL, Ushirika, Viwanda, Elimu, rasilimali madini,Reli, nk. Haya yote yalibomoka kwa sababu msingi wake ulikuwa ni mtu( Mwl JK Nyerere). Kwa kweli mashirika mengi ya umma halihujumiwa na wasomi...Sasa kama haya anayofanya JPM msingi wake ni yeye mwenyewe hakika YATABOMOKA. Sasa ni muombe muheshimiwa utusaidie kuimarisha sheria zitakazo simamia haya, pili Sisi Wakristo hasa mi mkatoliki tumefundishwa Mungu yupo kila mahali, pamoja na kuwa kila mahali Mungu anatufundisha utawala wa Kitaasisi yaani kuna Mungu, Yesu na kuna Roho Mtakatifu na kuna malaika. Hivyo basi JPM huwezi kuwa kila mahali tuimarishie Taasisi ili ziwe Msingi wakujenga unayoyafanya sasa ili hata kama ukiondoka YASIBOMOKE.

MISINGI WATU(MARAIS) MAENDELEO:
Hili limekuwa chanzo cha Watanzania wengi kusema tumekukumba JK au BWM au Mwinyi au Nyerere. Hii kauli ni kiashiria kwamba kila Rais anayeingia madaraka anakuwa ndo msingi katika msingi wa jambo flani katika maendeleo. Hili sijui wanafanya makusudi au bahati mbaya. Tuongelee hali ya sasa ya Kisiasa, wanasiasa wengi utawasiki "enzi za Kikwete mambo hayakuwa hivi" hii maana yake ni kwamba msingi wa demokrasia za awamu ya nne msingi wake ulikuwa "Kikwete mwenyewe" hapakuwa na hakuweka misingi yoyote kuhakikisha mfumo wa demokrasia unalindwa na Sheria na Katiba za nchi kwa kujua hivyo alisema "naindoka lakini MTANIKUMBUKA"
Nyerere: "kwa katiba hii mkimpata Rais dikteta mmekwisha"
Misingi ya maendeleo ikiendelea kuwa huruma ya Marais basi hakika hatuwezi kufika mbali.

Hitimisho:
Kama JPM anataka tumkumbuke atuachie katiba na sheria mbovu, na taasisi legelege, kwasababu ajaye anaweza akapiga chini yote yanayofanyika sasa akaja na plan B: Rais ajaye anaweza sema kipao mbele cha siyo ATCL au Reli(Road Transpot ikawa ndo kipaombele). Anayoyafanya sasa hivyi ni ujenzi wa ukuta kwenye msingi wa mchanga akiondoka yeye basi yanaweza yakabomoka. Ivyi imarisha taasisi na utawala wa sheri huu ni msingi sahihi wa maendeleo endelevu
 
Kipaumbele chake ni kuua upinzani na kubakiza wapinzani uchwara kama cheyo na mrema.
 
Back
Top Bottom