Mkuu wa mkoa Morogoro, shule ya msingi Juhudi ni bomu linalosubiri tu kulipuka

Tsyamatsy

Senior Member
Sep 9, 2023
109
155
Mkuu, nakileta kwako kilio Cha sisi wazazi WALALAHOI tunaosomesha watoto katika shule ya Msingi JUHUDI, kata ya Lukobe.

Mheshimiwa, sina uhakika kama Una taarifa zozote kwamba ndani ya kama kilomita 10 kutoka ofisini kwako ktk kata ya Lukobe Kuna shule ya watu maskini KABISA KABISAA TENA MASKINI WAKUTUPWA!! HAWA NI WALALA HOI KABISA ktk nchi hii ambao Mheshimiwa Rais wao Mama Samia anawatambua na ANAWATHAMINI kabisa na kawajengea shule iwe jirani yao ili watoto wao waelimike, na kwa jinsi Mama anavyowathamini hao walalahoi akakuteua wewe Mheshimiwa kuwa mlezi wa hao masikini wasio na UWEZO wa kusomesha watoto wao ktk shule za hadhi ya juu. Lakini sijui kama na wewe hao unaowasimamia chini yako sijui kama WALISHAKUELEZA ni nini kinachoendelea ktk shule ya Msingi JUHUDI!

Na kama WALISHAKUELEZA, basi walikudanganya Hali halisi ya hapo. Na kama unayo taarifa basi Wahenga walinene " Tusiandikie mate na wino upo" funga safari dakika yoyote usomapo waraka huu nenda mwenyewe kajionee, tuache masikhara kwenye uhai wa watoto wetu. No research no Comment!

Waswahili tunasema "Jihadhari kabla ya Hatari" Mheshimiwa kwani YALIYOTOKEA HANANG tena majuzi tu, Ina maana hatujajifunza kitu tu? Au ni mwendo ule ule tu, yaani tunasubiria majanga yatokee ndio Mnajifanya mnasikitika na kutoa pole!

Mkuu, shule ya JUHUDI ni HATARI KABISA KWA AFYA ZA WATOTO WETU! Mazingira ni Hatarishi Kwa watoto, magogo, michanga,tope, mawe na matakataka yanayoletwa na Mvua yamejaa Uwanja wa shule. Imekuwa sio shule kwani mkondo wa maji unapita katikati ya shule na imekuwa mikondo zaidi ya mmoja. Maji yanaingia madarasani, vyoo vimezingirwa na tope na mchanga, sijui watoto wanajisaidiaje. Maji yamechimba baadhi ya majengo na Msingi kubomoka.

Inasemekana Viongozi kadhaa walishafika hapo shuleni na Hali halisi wamejionea, lakini hakuna wanachokifanya.

Kwa yaliyotokea HANANG Liwe ni somo Kwa sisi binadamu; kwanini iwe ni somo? sababu kabla ya Hilo janga hakuna MTanzania ambae aliamini kuwa mlima unaweza KUMUNG'UNYUKA wote na kuleta maafa.
Mkuu pia Kuna suala la KIPINDUPINDU.

Hayo maji yanayopita hapo ndani ya shule yanakotoka yanapita katika nyumba za watu ambao wengine wanatumia fursa hii ya Mvua kutiririsha maji taka ya vyoo kuingia miferejini na hatimae yanapita hapo shuleni na watoto hao wadogo wanachezea.

Hili suala naona tunaWATESA sana walimu kwani tunawapa kazi za ziada kudhibiti watoto wasicheze kwenye matope, hivi kweli hao walimu wataweza kweli kuandaa masomo, kufundisha na Sasa kulinda AFYA za watoto it's not fair!

Hii naifananisha na mahafa ya Hanang Kwa kuwa iwapo kutatokea KIPINDUPINDU itakuwa ni HATARI sana, kwani tusiseme haiwezekani, kwani magonjwa yanasababishwaje? Shule Ina mamia ya watoto tena hapa ni wadogo wa darasa la 5 kurudi chini.

Na kama Manispaa Ina Bwana AFYA basi Kwa hii Hali halisi ya JUHUDI primary inabidi ajitathmini!
Wanakauli za kebehi eti kama hapakufai HAMISHA mwanao, sisi walalahoi uwezo wetu ndio hapo hapo ambapo Mama Samia anapathamini.

Mkuu, nakuomba fika mwenyewe hapo shuleni ujionene mwenyewe usitume mtu.
Na iyo shule kama ingelikuwa ya mtu binafsi Kwa mazingira halisi ya uchafu uliopo pale basi mmiliki angelikuwa muda huu yupo Magereza.

Hii shule ni ya Walalahoi ORIGINAL maana kama mtu una uwezo japo kidogo HUWEZI kumwacha mwanao ktk mazingira Hatarishi kivile.

Hivi unafikiri umaskini ni sifa au Ulemavu?Tufanye kazi kwa bidii watoto waende shule bora..wewe umepeleka mwana "Bora shule" na unaona ni Sifa kujiita maskini wa kutupwa Shenzi kabisa
 
Rubbish, nilipoona umeanza kusifia sijui mama kawajengea badala ya serikali na ni kodi zetu, nikajua huna akili.
 
Hivi unafikiri umaskini ni sifa au Ulemavu?Tufanye kazi kwa bidii watoto waende shule bora..wewe umepeleka mwana "Bora shule" na unaona ni Sifa kujiita maskini wa kutupwa Shenzi kabisa
Don't argue with a fool, otherwise people may not notice the difference!

Sent from my Infinix X6512 using JamiiForums mobile app
 
Malima mchapa kazi, limefika.

Kama Mluguru analilia shule badala ya ngoma na vigodoro, nchi imesomga mbele.

Wakoloni waliandaa IQ analysis ya makabila yote nchi nzima, na mkoa wa morogoro walipata the lowest score Tanganyika nzima.

Wakati huo mkoloni alikuwa anatafuta watu wa kufanya nao kazi za kuitawala Tanganyika.

Siongelei makabila yaliyopata the highest, sitaki migogoro na watu
 
wajinga nyie mnaturudisha nyuma haswa
Mjinga ni wewe, pilipili Iko Shamba unawashwa na nini? Ujinga wako nikujulishe maana hujui unalopoka tu, ujinga wako ni kwamba soma hapo juu kichwa Cha waraka huu, ni Kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro. Je, wewe ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro? Au unajiona kama upo very special!
Hii Jamii Forums sio sehemu ya matusi Wala kukashifiana, huo ni utoto, childish! Kama ni Matusi ebu tukana Tusi JIPYA ambalo halijawahi kutukanwa hapa duniani, ndio tukuone wa maana, yote Matusi ni ya zamani tumeyasikia sana. Utoto ukizidi unashindwa hata kuelewa Jamii Forums ni Kwa ajili ya nini! Hili ni jukwaa ambalo Malengo yake ni Makubwa, ni Kuelimisha, pia kurahisisha kupeleka taarifa Kwa wahusika kuhusu mambo
mbalimbali kwani Jukwaa hili members wengine ndio hao hao Viongozi Kwa iyo wanapata taarifa mapema na kutafuta suluhisho, mfano mmoja tu japo ipo mingi ni wa Dr Dorothy Gwajima aliwahi kujibu yaliyokuwa yanamhuhusu kupitia humu humu JF. Sasa wewe usituletee utoto wako kwenye mambo ya maana. We can't argue with a fool otherwise people may not notice the difference!
Sio Kila kitu unashobokea tu! Uwe na Busara ya kufikiri, kwani ukikaa kimya utayeyuka!

Kajifunze kiswahili kwanza wewe kilaza
 
Mkuu, nakileta kwako kilio Cha sisi wazazi WALALAHOI tunaosomesha watoto katika shule ya Msingi JUHUDI, kata ya Lukobe.

Mheshimiwa, sina uhakika kama Una taarifa zozote kwamba ndani ya kama kilomita 10 kutoka ofisini kwako ktk kata ya Lukobe Kuna shule ya watu maskini KABISA KABISAA TENA MASKINI WAKUTUPWA!! HAWA NI WALALA HOI KABISA ktk nchi hii ambao Mheshimiwa Rais wao Mama Samia anawatambua na ANAWATHAMINI kabisa na kawajengea shule iwe jirani yao ili watoto wao waelimike, na kwa jinsi Mama anavyowathamini hao walalahoi akakuteua wewe Mheshimiwa kuwa mlezi wa hao masikini wasio na UWEZO wa kusomesha watoto wao ktk shule za hadhi ya juu. Lakini sijui kama na wewe hao unaowasimamia chini yako sijui kama WALISHAKUELEZA ni nini kinachoendelea ktk shule ya Msingi JUHUDI!

Na kama WALISHAKUELEZA, basi walikudanganya Hali halisi ya hapo. Na kama unayo taarifa basi Wahenga walinene " Tusiandikie mate na wino upo" funga safari dakika yoyote usomapo waraka huu nenda mwenyewe kajionee, tuache masikhara kwenye uhai wa watoto wetu. No research no Comment!

Waswahili tunasema "Jihadhari kabla ya Hatari" Mheshimiwa kwani YALIYOTOKEA HANANG tena majuzi tu, Ina maana hatujajifunza kitu tu? Au ni mwendo ule ule tu, yaani tunasubiria majanga yatokee ndio Mnajifanya mnasikitika na kutoa pole!

Mkuu, shule ya JUHUDI ni HATARI KABISA KWA AFYA ZA WATOTO WETU! Mazingira ni Hatarishi Kwa watoto, magogo, michanga,tope, mawe na matakataka yanayoletwa na Mvua yamejaa Uwanja wa shule. Imekuwa sio shule kwani mkondo wa maji unapita katikati ya shule na imekuwa mikondo zaidi ya mmoja. Maji yanaingia madarasani, vyoo vimezingirwa na tope na mchanga, sijui watoto wanajisaidiaje. Maji yamechimba baadhi ya majengo na Msingi kubomoka.

Inasemekana Viongozi kadhaa walishafika hapo shuleni na Hali halisi wamejionea, lakini hakuna wanachokifanya.

Kwa yaliyotokea HANANG Liwe ni somo Kwa sisi binadamu; kwanini iwe ni somo? sababu kabla ya Hilo janga hakuna MTanzania ambae aliamini kuwa mlima unaweza KUMUNG'UNYUKA wote na kuleta maafa.
Mkuu pia Kuna suala la KIPINDUPINDU.

Hayo maji yanayopita hapo ndani ya shule yanakotoka yanapita katika nyumba za watu ambao wengine wanatumia fursa hii ya Mvua kutiririsha maji taka ya vyoo kuingia miferejini na hatimae yanapita hapo shuleni na watoto hao wadogo wanachezea.

Hili suala naona tunaWATESA sana walimu kwani tunawapa kazi za ziada kudhibiti watoto wasicheze kwenye matope, hivi kweli hao walimu wataweza kweli kuandaa masomo, kufundisha na Sasa kulinda AFYA za watoto it's not fair!

Hii naifananisha na mahafa ya Hanang Kwa kuwa iwapo kutatokea KIPINDUPINDU itakuwa ni HATARI sana, kwani tusiseme haiwezekani, kwani magonjwa yanasababishwaje? Shule Ina mamia ya watoto tena hapa ni wadogo wa darasa la 5 kurudi chini.

Na kama Manispaa Ina Bwana AFYA basi Kwa hii Hali halisi ya JUHUDI primary inabidi ajitathmini!
Wanakauli za kebehi eti kama hapakufai HAMISHA mwanao, sisi walalahoi uwezo wetu ndio hapo hapo ambapo Mama Samia anapathamini.

Mkuu, nakuomba fika mwenyewe hapo shuleni ujionene mwenyewe usitume mtu.
Na iyo shule kama ingelikuwa ya mtu binafsi Kwa mazingira halisi ya uchafu uliopo pale basi mmiliki angelikuwa muda huu yupo Magereza.

Hii shule ni ya Walalahoi ORIGINAL maana kama mtu una uwezo japo kidogo HUWEZI kumwacha mwanao ktk mazingira Hatarishi kivile.

View attachment 2879403
Acha kutanua likitambi hilo jinyime peleka mtoto English Medium

Jinga kabisa
 
Back
Top Bottom