Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Wadau,
Kwa uzoefu wangu wa uongozi katika idara mbalimbali zikiwemo za serikali na za binafsi, nimekuwa najikuta ninakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinanikosesha usingizi na wakati mwingine zinanifanya nifanye kazi hadi weekend au nifanye kazi hadi usiku bila malipo. Mara nyingi nimekuwa nikikwazwa sana na utitiri wa matatizo yanayokuwepo kwenye idara yangu ambayo kila nikiyaandikia proposal kwa ajili ya utatuzi hayapatiwi ufumbuzi. Ni kutokana na changamoto hizo nimejikuta kila nikipewa nafasi naishikilia kwa muda halafu naanza kutafuta mahali pa kutokea haraka sana ili niachane na cheo hicho nilichopewa.
Lakini kinachonishangaza ni nafasi ya Urais, ambayo mtu akishaingia tu basi hatamani tena kutoka, wengine wanabadili hadi katiba ili aongoze milele. Sasa najiuliza kitu, hivi huko hakuna majukumu kama yale yaliyopo kwenye ngazi za chini? Hivi ukiwa Rais huoni matatizo ya unaowangoza kama ambavyo tunaona tukiwa kwenye hizi nafasi za chini? Au hukumbani na changamoto zenye kukatisha tamaa kama hawa waliopo huku chini.
Kwa mfano Kikwete kasakamwa na watu wa kila aina si magazeti si watu gani, huko mbeya wakamrushia na mawe, ikulu wakamdanganya na kumdhalilisha, mara akaingizwa kwenye kufungua hotel ambayo in two days ilivunjwa na lawama kibao juu ya kushuka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha. Kutokana na haya yote hakupaswa aone kwamba hii ni kazi iliyomuelemea na hivyo aamue kuachana nayo? Lakini nashangaa anarudi kwa kasi ya ajabu ... huku akina Yahya wakiwatishia kifo kwa watakaompinga!
Ndiposa najiuliza hivi Urais ni kazi ngumu au ni rahisi tu ambayo hata mimi naiweza?