Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Wana JF,
Itakuwa vizuri zaidi tukajikita katika kujadili mchakato wa katiba.Tujadili maudhui ya katiba mpya ili tupate katiba bora kabisa ili tufike kwenye demokrasia ya kweli na tujenge Tanzania tuitakayo miaka 50 ijayo kuanzia sasa
Kwa wanachadema,tujadili namna bora ya kutunga sera mbadala na tufikirie zaidi kujiimarisha kama timu ili ifikapo 2015 tuingie kwenye uchaguzi mkuu tukiwa hatuna mgogoro wala makundi.Tukiimarishe chama chetu,tunayo fursa ya kuendelea kusaidiana na viongozi wetu wa ngazi zote na tuweke miundombinu itakayotupatia viongozi bora watakaotupeleka 2015.Wakati wenzetu wanagawanyika basi tutumie fursa hii kujiimarisha ila kwa tahadhari ya hali ya juu ili tusije tukaingia kwenye mtego wa kutegemea udhaifu wao tu
Tuweke mikakati mizito,tuzibe mianya yote na udhaifu uliokuwepo uchaguzi uliopita.Tunayo dhamira moja,naamini chama chetu kitatoa mgombea bora 2015 bado.Kitu cha msingi tuepuke ubinafsi tualenge kwenye maslahi mapana ya chama na taifa letu kwa ujumla.Uchaguzi wowote au uteuzi ndani ya chama chetu ni lazima tuuweke kwenye mizani ya 2015,ni uchaguzi wa Transitional team.
Ni wakati muafaka kwa wanachama na viongozi kupima aina ya kauli tunazotoa vinywani mwetu,sio muda wa kutoa reckless statements.Tuwekeze na tuimarishe kitengo chetu cha research.Ni muda wa uwajibikaji zaidi na kila mmoja awe evaluated kupitia results zinazoonekana
Kuna mgombea/wagombea wa chama tawala wanajitahidi kujitenga na udhaifu wa serikali iliyopo ili kujenga aura ya messiah ajaye.Watanzania tusidanganyike.Wanajitahidi kujifanya wanaguswa na matatizo ya vijana ili kuteka kundi la vijana ambao ndio mtaji mkubwa wa vyama na wagombea urais 2015.Tuitumie taasisi ya BAVICHA katika hili na kitengo cha research.Tusiingie kwenye mtego wa majungu kama wenzetu.Pia katibu mkuu na secretariat wanajituma tuwaongezee nguvu
Tujipange kikamilifu kwani uchaguzi ujao utakuwa mgumu sana,naamini CHADEMA itaweka historia.Tupanue mtandao,tuimarishe safu ya uongozi na kuhakikisha umoja na mshikamano ndani ya chama,tufanye tafiti za kutosha tuandae ilani ambayo itakuwa the best na itakayo sustain transition kwa kuzingatia waathirika wakubwa na walengwa wakundi kubwa la vijana katika aspect zote
Ben,
Mkuu chadema isipochukua dola 2015 nahisi unaweza kuingia msituni.ila nimeona unatumia Masters yako ya International relations vizuri katika propaganda na kutetea chama chako.Hata hivyo usitegemee chadema kushinda 2015.ila shwari tu naona mmejipanga kwa juzi kumteua mnyika kwenye hicho kitengo cha propaganda ndani na nje ya nchi.hii ni changamoto kwa nape na January makamba sasa.punguza siasa za ki-radical maanke kila ukiongelea demokrasia huwa nainua eyebrows kwa jinsi ninavyokufahamu.ee mungu iepushe tanzania na umwagaji damu uchaguzi mkuu ujao
Inaonekana mnaanza kujiandaa kama vile mmejua lowassa atakuwa mgombea ndani ya CCM.Hakuna chama chenye hatimiliki ya vijana.