Mbio za urais 2015 zimeanza ndani ya CHADEMA, harakati hizi zinamtaja Mb. Zitto Kabwe, Mb. F.A. mbowe Na MRUSHA BENDERA YA CHADEMA 2015, na mb. Tundu Lisu. Mi nampa chapuo
1. Tundu Lisu
2. Dr. W. Slaa
Sababu kuu 3 kwao
1. Wameonesha mapambano ya wazi na uwezo mkubwa wa kujenga na kusimamia hoja za msingi kwa maendeleo ya Tz. Pia katika hilo hawajayumbishwa na tume mbambali kama ile ya madini aloingia Zitto na kufungwa mdomo.
2. Hawajaonesha tamaa ilopitiliza ya mali na utajiri haramu katika kundi la masikini hohehahe wa tz. Hakuna ushahidi wa wao kujilimbikizia mali na maisha ya kujirusha bila kujali wavujajasho.
3. Watakwepa mishale ya ya ukanda na ukabila Kama ulivyo kwa mbowe, wamejipambanua katika kusimamia kanuni na heshma kwa taaluma zao.
GREAT THINKERS TUNAWASAIDIA CHADEMA ILIKUPATA MGOMBEA URAIS AMBAE ELECTABILITY YALE NI KUBWA, NA ANAEWEZA KUTOA USHINDAN KWA CCM AMBAYO KWA VYOVYOTE LAZIMA ISHINDE UCHAGUZI UJAO HATA IKIWAHI NDANI YA KATIBA MPYA?
1. Tundu Lisu
2. Dr. W. Slaa
Sababu kuu 3 kwao
1. Wameonesha mapambano ya wazi na uwezo mkubwa wa kujenga na kusimamia hoja za msingi kwa maendeleo ya Tz. Pia katika hilo hawajayumbishwa na tume mbambali kama ile ya madini aloingia Zitto na kufungwa mdomo.
2. Hawajaonesha tamaa ilopitiliza ya mali na utajiri haramu katika kundi la masikini hohehahe wa tz. Hakuna ushahidi wa wao kujilimbikizia mali na maisha ya kujirusha bila kujali wavujajasho.
3. Watakwepa mishale ya ya ukanda na ukabila Kama ulivyo kwa mbowe, wamejipambanua katika kusimamia kanuni na heshma kwa taaluma zao.
GREAT THINKERS TUNAWASAIDIA CHADEMA ILIKUPATA MGOMBEA URAIS AMBAE ELECTABILITY YALE NI KUBWA, NA ANAEWEZA KUTOA USHINDAN KWA CCM AMBAYO KWA VYOVYOTE LAZIMA ISHINDE UCHAGUZI UJAO HATA IKIWAHI NDANI YA KATIBA MPYA?
FUKUTO la Urais mwaka 2015 ndani ya vyama vya siasa linazidi kupamba moto, huku majina ya makada wanaowania nafasi hiyo kupitia chama kikuu cha upinzani nchini Chadema, yakianza kuanikwa.
Ikiwa imebaki takribani miaka mitatu kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka 2015, makada mbalimbali ndani ya vyama, wameanza kupigana vikumbo kila mmoja kujaribu kujipanga ili achaguliwe kupeperusha bendera ya chama chake kwenye uchaguzi huo. Ndani ya chama tawala CCM, taarifa zinadai kuwa baadhi ya wanasiasa wameanza kuunda mitandao huku wengine wakilaumiwa kuanza ‘kucheza rafu' kwa kumwaga mamilioni ya fedha kwa lengo la kutekeleza mkakati huo.
Tayari hatua hiyo imelaumiwa na baadhi ya makada ndani ya chama hicho kikongwe nchini huku wengine wakionya kuwa mbio za Urais mwaka 2015, zinatishia kuisambaratisha CCM.Wakati heka heka hizo zikiendelea ndani ya CCM, habari kutoka ndani ya Chadema, zimetaja baadhi ya majina ya makada wa chama hicho, wanaopewa nafasi kubwa kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Chadema, zimewataja watu hao kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chadema ambaye pia aligombea urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi uliopita, Dk Willibroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.
Ingawa Zitto tayari ameweka wazi kuwa hatagombea kutokana na umri wake kuwa chini ya ule unaotambuliwa kikatiba kwa nafasi hiyo, bado ana matumaini kwamba kipengele hicho kinaweza kubadilishwa ndani ya katiba mpya.
Kwa mujibu wa katiba ya sasa, mtu anayewania Urais wa Jamhuri ya Muungano lazima awe na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea. Mwaka 2015 Zitto atakuwa hajafikisha umri huo na ‘atanusurika' endapo tu katiba mpya itapunguza umri huo. Chanzo chetu kimeeleza kuwa picha halisi ya atakayewania nafasi ya urais kupitia chama hicho itadhihirika baada ya kukamilika kwa chaguzi za ngazi zote ndani ya chama hicho baadaye mwaka huu.
Mazingira mengine ambayo yanaweza kuathiri ama kuamua juu ya mgombea urais wa chama hichona kujiunga kwa wanachama wapya husasan kama baadhi ya vigogo watajiengua CCM na kuamua kujiunga na chama hicho.
Hofu ya makada wa CCM kutimkia Chadema inatokana na kundi kubwa la wanasiasa ndani ya chama hicho kutaka nafasi hiyo, hali itakayowafanya wengine kwenda vyama vingine kujaribu bahati zao.
Kutokana na idadi kubwa ya wanaCCM wanaotaka nafasi hiyo, baadhi ya watu wanadaiwa kuunda mitandao yenye malengo ya kuchafuana
CCM katika kikao chake cha Halmashuari Kuu (NEC) kilichoketi mjini Dodoma Novemba mwaka jana, kilikiri kuwa mvutano mkubwa wa makundi uliopo ndani ya chama hicho, chanzo chake ni Urais wa mwaka 2015.
Kwa upande wa Chadema, ingawa bado hakuna vita ya wazi wazi kama ilivyo ndani ya CCM, wanachama wake wameaanza kuzungumzia na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi huo.
Dk Slaa ambaye aligombea katika uchaguzi uliopita na kuibuka mshindi wa pili baada ya kupata asilimia 26 ya kura zote zilizopigwa, ndiye anayeonekana kupewa nafasi kubwa. Mwanasiasa huyo anaonekana kuwa bado anafaa kuwania tena nafasi hiyo kutokana na rekodi nzuri kwenye uchaguzi uliopita.
Katika uchaguzi huo, Dk Slaa alionesha kuyaelewa vyema matatizo ya Watanzania na kujaribu kueleza nini kifanyike kuondokana nayo, hali iliyowafanya wananchi wengi kuwa na imani naye.
Mbowe (50) ambaye aliwania kiti cha urais mwaka 2005 na kushika nafasi ya tatu, anatajwa kuwa anaweza kuwania tena nafasi kutokana na rekodi yake safi ya kukiimarisha chama hicho kunzia tangu kikiwa kichanga hadi kukiwezesha kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.
Wanachama wengine wa chama hicho wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ni pamojan na John Shibuda ambaye mwaka juzi alichukua fomu za kuomba kuwania urais kupitia chama CCM, lakini baadaye alijitoa na kumuunga mkono mgombea wa chama hicho, Rais Kikwete.
Wengine ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
Hata hivyo Lema ambaye ametajwa kuwa mbunge bora kwenye moja ya mitandao ya kijamii nchini, aliliambia Mwananchi Jumapili juwa hana nia ya kuwania urais kupitia chama hicho mwaka 2015.
Alisema pamoja na kupata kura nyingi za watu waliomuunga mkono kwenye mtandao huo, alisema hatarajii kugombea nafasi hiyo ya urais ila akasisitiza kuwa ataweka nguvu zaidi kwenye ubunge.
"Nashukuru kwa kupata kura hizo, lakini sitarajii kuwania nafasi hiyo… Atakayeteuliwa na chama changu nitamuunga mkono," alisema.
Source: Mwananchi 08/01/2012