Anawaza urais wenzake 2najenga CHADEMA kwanzaliwalo na liwe zitto lazima agombee urais na makam wa rais lazima atokee kigoma - kafulila
Jadili hoja..,ukishindwa kaa kimya.
SAFARI ya CHADEMA kuelekea 2015 na ndoto za kuingia ikulu zinazidi kupaa kwa Chama hiki kikuu cha Upinzani Bungeni.
HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe ya kutangaza nia yake ya kutaka kugombea urais mwaka 2015 na sakata la tuhuma za rushwa bungeni, vimekifanya chama hicho kigawanyike makundi makubwa matatu yanayovutana.ambapo kila kundi lina msimamo wake, hali iliyosababisha kuzuka kwa mvutano wenye mkanganyiko mkubwa na kuibua sintofahamu miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama chake.
Miongoni mwa waandamizi ,Watatu waliojitokeza waziwazi kumkemea huku kwa visingizio tofauti wakiwemo mwasisi wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei; Mwenyekiti wa Taifa wa sasa, Freeman Aikaeli Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Peter Slaa.
Hata hivyo ZITTO alipuuza makemeo hayo na alichukua hatua ya mbele zaidi kwa kusisitiza kauli yake hiyo katika Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kusema kuwa anaitaka nafasi hiyo na anaimudu, na pia ana uwezo mkubwa wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama huku akitamba kwamba ni MWADILIFU na MZALENDO.
Ikiwa kashi kashi hiyo inaendelea kwenye Chama, Karibuni ZITTO ametajwa kuhusika katika sakata la RUSHWA katika TANESCO, ambapo kashfa ya tuhuma hizo za rushwa ziliibuka baada kauli yake ya kuwatetea maofisa waandamizi wanne wa Shirika la Umeme.
Kuhusika kwa Zitto kumeibua mtafaruku ndani ya Chadema. Viongozi, wanachama na wafuasi wa chama hicho wenye msimamo mkali wa ukabila na ukanda wanapinga kwa kelele nyingi uwezekano wowote wa mbunge huyo kugombea urais wakitoa sababu tofauti (ambazo kabla ya hili la rushwa, sababu nyingi hazikuwa za msingi).
Jumatano iliyopita, Zitto aliwashutumu baadhi ya wabunge kutoka nje na ndani ya Chadema akidai wanatumika kumpakazia tuhuma za rushwa kutokana na sababu za kisiasa. Alisema wengine hususan wapinzani wenzake wanaitaka nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC). Pili, alisema wapo wanaofanya hivyo wakilenga kumchafua hasa baada ya kutangaza kutaka kugombea urais mwaka 2015.
Kuibuka kwa makundi hayo kumeelezwa na vyanzo hivyo vya habari kuwa kumegawanyika kimikoa. Wengi wanaomuunga mkono wanatoka mikoa ya Kigoma, Geita, Kagera, Tabora, Rukwa na Katavi na baadhi ya mikoa iliyopo kusini.
Lakini wanaompinga wakidai amechafuka kwa tuhuma za ufisadi na hivyo hawezi tena kuwa mgombea sahihi wa kiti hicho wanatoka zaidi katika mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Mara ambayo ipo kaskazini mwa Tanzania.
Hata hivyo, sehemu kubwa ya mikoa iliyobaki haijaingia katika mvutano huo wa kisiasa, lakini imeelezwa kwamba baadhi ya wabunge wa Chadema nao wanampiga vita kwa siri na vya wazi, lakini wapo baadhi ambao wapo upande wake na wanamuunga mkono katika harakati zake hizo kuelekea urais.
Miongoni mwa wabunge wanaotiliwa wasiwasi kuwa inawezekana ni mmoja kati ya wale waliogusiwa na Zitto lakini bila ya kutajwa majina yao kwamba wanainyemelea nafasi ya Uenyekiti wa POAC ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu
Hali ya vita ya Urais ni JINAMIZI zito ambalo linaelekea kuimaliza CHADEMA moja kwa moja, kwani wapo baadhi ya viongozi ambao wanaamini katika wao tu na si mwingine na ambao wamejitengenezea wigo na ngome imara ya kujilinda ili kuhakikisha nafasi hiyo inabki kwao na kutumia mbinu mbalimbali hasa kwa kuwachafua wenzao ili wao wabaki pekee katika kinyang'anyiro hicho. Shibuda alijaribu japo kwa UTANI tu na alijadiliwa zaidi ya mara 5 katika vikao vya maadili kwa kitendo chake hicho cha kusema anataka urais akiwa chama hiko.
Unatumia nguvu kubwa bila sababu huku ukitokwa mapovu kutetea upumbavu wako! Sikushangai kwani najua wazi hizo ndio tabia za wapenda majungu na fitina kama wewe.Ilazimishe akili yako kufikiri nje ya box ulilomo..,kama hatoamua kushirikisha ubongo wako ipasavyo katika unayoyasema na kuyaamua daima utaishia kuburuzwa.
Jadili hoja..,ukishindwa kaa kimya.
Jadili hoja..,ukishindwa kaa kimya.
i like this. hakyanani CDM tumekomaa kimawazo. jamaa anajaribu kupenyeza jungu, lakini kagonga mwamba. duh!!TandaleOne kajipange upya, hili jungu lako limebuma. mambo yetu CDM tutayamalize wenyewe wala usiwashwewashwe kutubunia uozo hapa. KAJIPANGE KIVINGINE MKUU, OVYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!!!Sema tujadili majungu, maana hakuna hoja hapa!
Jadili hoja..,ukishindwa kaa kimya.