Urais 2015, Rushwa vyaitesa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Urais 2015, Rushwa vyaitesa CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, Aug 7, 2012.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  SAFARI ya CHADEMA kuelekea 2015 na ndoto za kuingia ikulu zinazidi kupaa kwa Chama hiki kikuu cha Upinzani Bungeni.

  HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Zitto Zuberi Kabwe ya kutangaza nia yake ya kutaka kugombea urais mwaka 2015 na sakata la tuhuma za rushwa bungeni, vimekifanya chama hicho kigawanyike makundi makubwa matatu yanayovutana.ambapo kila kundi lina msimamo wake, hali iliyosababisha kuzuka kwa mvutano wenye mkanganyiko mkubwa na kuibua sintofahamu miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama chake.


  Miongoni mwa waandamizi ,Watatu waliojitokeza waziwazi kumkemea huku kwa visingizio tofauti wakiwemo mwasisi wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei; Mwenyekiti wa Taifa wa sasa, Freeman Aikaeli Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Peter Slaa.

  Hata hivyo ZITTO alipuuza makemeo hayo na alichukua hatua ya mbele zaidi kwa kusisitiza kauli yake hiyo katika Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa kusema kuwa anaitaka nafasi hiyo na anaimudu, na pia ana uwezo mkubwa wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama huku akitamba kwamba ni MWADILIFU na MZALENDO.

  Ikiwa kashi kashi hiyo inaendelea kwenye Chama, Karibuni ZITTO ametajwa kuhusika katika sakata la RUSHWA katika TANESCO, ambapo kashfa ya tuhuma hizo za rushwa ziliibuka baada kauli yake ya kuwatetea maofisa waandamizi wanne wa Shirika la Umeme.

  Kuhusika kwa Zitto kumeibua mtafaruku ndani ya Chadema. Viongozi, wanachama na wafuasi wa chama hicho wenye msimamo mkali wa ukabila na ukanda wanapinga kwa kelele nyingi uwezekano wowote wa mbunge huyo kugombea urais wakitoa sababu tofauti (ambazo kabla ya hili la rushwa, sababu nyingi hazikuwa za msingi).

  Jumatano iliyopita, Zitto aliwashutumu baadhi ya wabunge kutoka nje na ndani ya Chadema akidai wanatumika kumpakazia tuhuma za rushwa kutokana na sababu za kisiasa. Alisema wengine hususan wapinzani wenzake wanaitaka nafasi ya Uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC). Pili, alisema wapo wanaofanya hivyo wakilenga kumchafua hasa baada ya kutangaza kutaka kugombea urais mwaka 2015.

  Kuibuka kwa makundi hayo kumeelezwa na vyanzo hivyo vya habari kuwa kumegawanyika kimikoa. Wengi wanaomuunga mkono wanatoka mikoa ya Kigoma, Geita, Kagera, Tabora, Rukwa na Katavi na baadhi ya mikoa iliyopo kusini.

  Lakini wanaompinga wakidai amechafuka kwa tuhuma za ufisadi na hivyo hawezi tena kuwa mgombea sahihi wa kiti hicho wanatoka zaidi katika mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Mara ambayo ipo kaskazini mwa Tanzania.

  Hata hivyo, sehemu kubwa ya mikoa iliyobaki haijaingia katika mvutano huo wa kisiasa, lakini imeelezwa kwamba baadhi ya wabunge wa Chadema nao wanampiga vita kwa siri na vya wazi, lakini wapo baadhi ambao wapo upande wake na wanamuunga mkono katika harakati zake hizo kuelekea urais.

  Miongoni mwa wabunge wanaotiliwa wasiwasi kuwa inawezekana ni mmoja kati ya wale waliogusiwa na Zitto lakini bila ya kutajwa majina yao kwamba wanainyemelea nafasi ya Uenyekiti wa POAC ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu

  Hali ya vita ya Urais ni JINAMIZI zito ambalo linaelekea kuimaliza CHADEMA moja kwa moja, kwani wapo baadhi ya viongozi ambao wanaamini katika wao tu na si mwingine na ambao wamejitengenezea wigo na ngome imara ya kujilinda ili kuhakikisha nafasi hiyo inabki kwao na kutumia mbinu mbalimbali hasa kwa kuwachafua wenzao ili wao wabaki pekee katika kinyang'anyiro hicho. Shibuda alijaribu japo kwa UTANI tu na alijadiliwa zaidi ya mara 5 katika vikao vya maadili kwa kitendo chake hicho cha kusema anataka urais akiwa chama hiko.
   
 2. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Msalimie bosi wako...umemcopy ritz na rejao vipi upo kundi gani wewe?
   
 3. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Jadili hoja..,ukishindwa kaa kimya.
   
 4. O

  Ongeauchoke Senior Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mawazo ya watu wa Mabwe pande
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Hivi vijarida vya udaku na waandishi makanjanja ni bomu kabisa
   
 6. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Hivi kuwa mwenyekiti wa kamati ya POAC kuna uhusiano gani na urais? Ningekuwa mimi ni mshauri wa Zitto kutokana na madudu yanayoibuliwa na CAG kuhusiana na mashirika anayopaswa kuyasimamia kwa niaba ya bunge ningejiuzulu kwani madudu ni mengi sana.
   
 7. makusanya

  makusanya JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Foolish
   
 8. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Sema tujadili majungu, maana hakuna hoja hapa!
   
 9. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Nalitazama jambo hili kwa jicho kali lenye utafakari wa kutosha, yawezekana kabisa uwepo wa kundi hilo linalompinga zitto ni ishara ya ukomavu katika siasa za kidemokrasia, lakini nachelea kusema kuwa njia zinazotumika zaweza kuwa ni za kimafia na zisizo za kidemokrasia kabisa.
   
 10. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,176
  Likes Received: 1,257
  Trophy Points: 280
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu mbona majibu yapo wazi na yameisha tolewa.. Ebu soma haya kwa mamkini halafu tafakari....

  Kwa CHADEMA, siku zote suala la urais linategemea na kufuata mahitaji mapana ya Watanzania, kamwe haliwezi kuamriwa kwa kufuata matakwa, utashi au uchu wa watu/mtu binafsi. Na katika kufikia hatma ya mahitaji/ maslahi mapana ya wananchi, chama hiki siku zote huamua kwa kufuata na kuzingatia katiba, kanuni na taratibu zake, si vinginevyo.

  Ni uwezo na umakini wa kuzingatia mahitaji ya chama na maslahi mapana ya umma katika kuamua masuala mazito kwa mstakabali wa taifa, huku kikifuata katiba yake, kanuni na taratibu, ndiyo umekipambanua CHADEMA kuendelea kuwa chama makini, kinachoaminiwa kwa dhati na Watanzania, na kiupekee kuwa kinastahili kupewa ridhaa ya kuongoza nchi hii.

  Mahitaji ya chama na ya Watanzania ndiyo yaliyotumika kupata wagombea urais wa CHADEMA katika chaguzi kuu mbili, mwaka 2005 na 2010. kwa kuzingatia mtazamo huo, mara zote hizo mbili, wagombea waliombwa, wala hawakuongozwa na uchu au tamaa ya madaraka.

  Hali itakuwa hivyo hivyo wakati ukiwadia wa kumpata mgombea urais wa mwaka 2015, kamwe utashi, uchu au maslahi binafsi ya mtu hayawezi kupata/kupewa nafasi ndani ya CHADEMA.

  Kwa CHADEMA, urais si cheo, ni dhamana ya utumishi kwa umma, suala ambalo linazingatia masuala muhimu, ambayo ni mahitaji ya wananchi (nchi) na kisha sifa za mtu husika kuwa kiongozi wa nafasi hiyo.
   
 12. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Ilazimishe akili yako kufikiri nje ya box ulilomo..,kama hatoamua kushirikisha ubongo wako ipasavyo katika unayoyasema na kuyaamua daima utaishia kuburuzwa.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  TandaleOneTandaleOne Hii tittle ya Dissertation yako mpelee Nape aipitie kabla hujaileta kwa External halafuu hii Tittle Magamba wengi wameshaitumia sana Sugua kichwa uje na Nyingine kama
  1: Lema anashirikiana na Mashoga japo hii imeshatumiwa na Ritz
  2: Chadema ni Wezi wa Mali za Umma
  3: Dr Slaa ameoa
  4: Mtoto wa Mbowe Anasoma shule za kisasa badala ya shule za kata
  5: Chadema wachochea Vita Malawi
  6: Chadema inasambaza Ebola
   
 14. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sijaona Hoja, that is why?
   
 15. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #15
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,075
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Mkuu tandale umewashika pabaya tegemea kejeli na matusi pro chadema si wajuzi wa kwenda hoja kwa hoja... Ukiwazidi hoja wataleta fitna za upewe ban
   
 16. A

  AUDITOR OF MAFISADI Member

  #16
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  umbeea au,tunajua mshahara wako aliyekutuma,1000/-
   
 17. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #17
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Una kazi!
   
 18. r

  rwazi JF-Expert Member

  #18
  Aug 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu kama hawa ndo wanalalaga kwenye milango ya watu wakisikilizia ili wapate chakuongeaMbona hujasema namna makundi yanavytesa magamba yenu
  .
   
 19. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #19
  Aug 7, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Masikini weee! Ungependa itokee hivi, lakini huna uwezo huo. Hamia kwanza CDM uende ukawavuruge humo humo.
   
 20. t

  thatha JF-Expert Member

  #20
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  kwa chama makini,huu ni wakati muafaka wa kuanza kuandaa mgombea wa urais
   
Loading...