Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

wewe acha kudanganya uma chadema ni chama makini hawakurupuki hakuna mpasuko wowote 2015 nchi lazima ichukuliwe na chadema

Cdm waache kujidanganya, kiukweli umaarufu ilionao leo umechangiwa kwa kiasi kikubwa sana na ugombeaji urais wa Dr Slaa 2010, na bado wapenda mabadiliko tunaimani naye sana. Mpango wotote wa kumuondoa kwa hila kwa kuamini kuwa sasa chama ni maarufu kuliko Slaa kitabadili upepo wa wapenda mabadiliko kwa kasi ya ajabu na historia itawahukumu maana kosa hilo litasababisha ccm watawale kwa muda mrefu sana ujao kabla ya wananchi kupata chama mbadala cha kukiamini, tutambue kuwa ushindi wa chama chochote unategemea wapiga kura wasiofungamana na vyama kuliko wanachama.
 
Hii dhana sijui imetoka wapi mtu yeyote humu JF hakiwa Against Chadema basi katumwa na CCM, labda nikuulize wewe kwenye mshahara wa Dr Slaa wa milioni 7 kwa mwezi anakutakia kiasi gani?

inaonekana unamzimia sana Nape; maana huishi kumtaja sisi wengine hamtujui zaidi ya kumsoma kwenye magazeti

Chama
Gongo la mboto DSM

Hapa sion hoja ya kujibu ngoja nisepe niende majukwaa mengine

hii mitambo inayofyatuliwa kwa Nnauye Jr Lumumba zero:poa
 
Last edited by a moderator:
Pasco said:
Hivi nyinyi wapenzi wa Chadema, bado hamjajua ZZK ndio mtaji wenu pekee wa ushindi 2015?...ZZK anakubalika sana kutokana na kuendesha "strategic politics" kwa urafiki wake na January Makamba, atazivuna kura zote za vijana wa CCM!, kwa urafiki wake na Jussa, atazivuna kura zote za CUF kule visiwani. Kwa usomi wake, atazivuna kura zote za vijana/wasomi na wataka badiliko ya kweli with clear goals na right strategies!.

Sasa Pasco, kweli unaamini kwa dhati kutoka rohoni kuwa hiyo picha unayoijenga ndio lengo na dhamira ya Chadema...yaani kushinda Uraisi kwa namna yoyote ile hata ikibidi kuwasaliti mamilioni ya wapenzi wao. Kwa lugha nyingine ni kuwa bila ZZK, Chadema haifiki popote pale kwani inahitaji baraka za CCM (January) na CUF (Jusa) ili iweze kukamata dola. Pasco, you are better than this!

Kuna watu mnaiunderestimate hii tsunami ya Chadema, sijui ni kwa makusudi, hila au kutojua. Leo hii niko tayari ku"bet" na yeyote yule anayeamini kuwa ikitokea ZZK akatemwa Chadema, basi huu moto wa Chadema basi...Please Pasco, this is a movement now, you are either in it and agree to swim with the current or out and be swept and left by the wayside. This is no NCCR or CUF...time will tell!
 
Zitto na ujana. Ujana pekee siyo sifa maana naona Zitto kila wakati ni kuomba wazee waondoke. Sifa muhimu ni ukamilifu wa akili.

Hiyo akili ya Zitto nikifikiria inanipa taabu maana anaonekana kama wale wanaoamini wamefanikiwa kuliko mtu yoyote nchi hii. Nadhani baada ya haya yanayotupata na huyu aliyeko ikulu, sasa tuwatake wote wanaotaka urais wapime afya zao za akili.

BTW mbona nasikia 'kijana' huyu siyo raia wa TZ. Nasikia ni mkongoman. Zitto kabila gani? maana ukichokoa lazima uchokolewe!
 
Hii dhana sijui imetoka wapi mtu yeyote humu JF hakiwa Against Chadema basi katumwa na CCM, labda nikuulize wewe kwenye mshahara wa Dr Slaa wa milioni 7 kwa mwezi anakukatia kiasi gani?

wanaweweseka, wameshikwa pabaya.

Kwa taarifa yake mimi sina chama, nitasimama kwenye ukweli daima.
Cdm ni wanafik wakubwa, zito kwao ni kama toilet pepa, wanamtumia pale wanapomuhitaji, akitaka kutumia haki yake ya kikatiba mnamzuia na kumuita msaliti.

Ubaguzi wenu ndo unawamaliza.
 
inaonekana unamzimia sana Nape; maana huishi kumtaja sisi wengine hamtujui zaidi ya kumsoma kwenye magazeti

Chama
Gongo la mboto DSM

mkuu chama mimi huyo nape sijawai kumuona hata kwa sura, wewe sikufaham wala Ritz wala memba yeyote wa jf.
Sasa nashangaa anahangaika kutuo shutuma za kitoto badala ya kujibu hoja.
 
kwa kweli namsihi aangalie maneno ya busara ya wazee wanayompa na siyo kuropoka na kiongoz mzur anateuliwa na watu na siyo kusimama majukwaani na kujitangaza ovyo ovyo kwani jamni ikulu kuna nini

mwl.alisema ukiona mtu analilia ikulu huyo mwogope kama ukoma
 
mkuu chama mimi huyo nape sijawai kumuona hata kwa sura, wewe sikufaham wala Ritz wala memba yeyote wa jf.
Sasa nashangaa anahangaika kutuo shutuma za kitoto badala ya kujibu hoja.

ndugu yangu si ulale au ndio unatafuta overtime kutoka kwa mwenezi?
 
Zito anajidanganya sana,aache kuropoka,anakuwa kama hajaenda shule!,subiri muda ufike utangaze nia yako,sasa hivi jenga chama kwanza.

Mkuu, kuna wimbo mmoja wa zamani kidogo ambao huanza na maneno yafuatayo "wamekula ya mbuzi, wameota mapembe". Nadhani ni msanii Ndanda Kossovo.
Usemi huu kwa sasa unamlenga Mhe. Zitto.

Anajiona amekwisha komaa sana kiasi cha kushika dola. Binafsi namwona bado sana. Kwa bahati mbaya ni mtu wa kujisikia sana na kutaka kusikilizwa sana.
Hii ni mbaya kwa kiongozi anayependa kuwa rais wa nchi.
 
Ritz said:
Hii dhana sijui imetoka wapi mtu yeyote humu JF hakiwa Against Chadema basi katumwa na CCM, labda nikuulize wewe kwenye mshahara wa Dr Slaa wa milioni 7 kwa mwezi anakukatia kiasi gani?
Na hii dhana sijui imetoka wapi mtu yeyote humu JF hakiwa Against CCM basi ni Chadema, labda nikuulize wewe kwenye wizi wa mabilioni ya EPA, Richmond, Kagoda...ulikatiwa kiasi gani?
 
Zitto is genuine and always speaks his mind, he can make a very good candidate. I'm in support of Pasco.
 
acha nami swali kama anavyoulizaga "Liwalo na Liwe"..Huyu Zitto huyu ni nani huyu Zitto? Isijekuwa tunamkuza wenyewe kumbe kijana mwenyewe anahangaishwa na identity crisis
 
Mzee mtei anatushangaza kajuaje kama mbowe na slaa wanautaka urais.na mbona hakuwakemea kama anavyomkemea ZZK au kwa sababu Mbowe na Slaa wanatoka kanda moja na yeye Kaskazini?
 
Mkuu unachanganya hoja yko n nn hapa
Mkubwa,

Hoja yangu ni kwamba, Mtei , a founding elder wa chama, anapoenda kwenye media kumshambulia Naibu Katibu Mkuu wa chama kwa kosa la ku declare presidential ambitions, huko sio kupasua chama? Mtei hakutakiwa kumshambulia Zitto hadharani, kama ambavyo Zitto nae hakutakiwa kumjibu hadharani, wote ni reckless amateurs.

Lakini cha muhimu zaidi - kikubwa kuliko Mtei na Zitto - ni kwamba CHADEMA wanakosea wanaposema "Chama bado hakijatoa utaratibu..." Katiba ya CHADEMA haijaeleza utaratibu? Kwa nini Mtei aseme Zitto asubiri chama kitangaze utaratibu? Asubiri chama kitangaze Katiba ya chama? That's incredibly ridiculous.

Mwasisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA Edwin Mtei amemuonya mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuacha kutangaza mambo ya Urais sasa kwani anasababisha mpasuko ndani ya CDM na badala yake ajikite kukijenga chama mpaka muda utakapofika ili chama kitoe utaratibu.

 
mkuu chama mimi huyo nape sijawai kumuona hata kwa sura, wewe sikufaham wala Ritz wala memba yeyote wa jf.
Sasa nashangaa anahangaika kutuo shutuma za kitoto badala ya kujibu hoja.

Wakipita pale Togo kuchukua posho kazi yao ni kulalama tu ! Hawa si wageni kwetu tumewazoea; ukiwaeleza ukweli tu wanapokimbilia ni Nape na Lumumba hawana jingine

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kaskzini in da white house ndo tatizo.
Vijana wengi wamesahau huyu huyu Zito wanayemtukana na kusema kahongwa ndiye aliyewavutia kuingia chadema na ndiye alowapa mwanga wabunge wengi vijana na amewakomaza kisiasa.
Kweli fanya jema usepe zako usingoje shukrani!

Salute

www.oric.co.tz, skype: alfred.kohi, 0784800989
 
Sasa Pasco, kweli unaamini kwa dhati kutoka rohoni kuwa hiyo picha unayoijenga ndio lengo na dhamira ya Chadema...yaani kushinda Uraisi kwa namna yoyote ile hata ikibidi kuwasaliti mamilioni ya wapenzi wao. Kwa lugha nyingine ni kuwa bila ZZK, Chadema haifiki popote pale kwani inahitaji baraka za CCM (January) na CUF (Jusa) ili iweze kukamata dola. Pasco, you are better than this!

Kuna watu mnaiunderestimate hii tsunami ya Chadema, sijui ni kwa makusudi, hila au kutojua. Leo hii niko tayari ku"bet" na yeyote yule anayeamini kuwa ikitokea ZZK akatemwa Chadema, basi huu moto wa Chadema basi...Please Pasco, this is a movement now, you are either in it and agree to swim with the current or out and be swept and left by the wayside. This is no NCCR or CUF...time will tell!
Mkuu Mag3, kwanza tukubaliane yafuatayo...
  1. Chama ni wanachama wenye lengo moja na nia moja, hivyo chama sio jina, jengo au mtu!. Chadema sio ZZK, Mbowe au Slaa, its more than that!. Kuna manazi wa Chadema, kwao Chadema ni "watu" na hao watu kwao ndio lazima wawe wao, kama sio wao basi hakuna wengine!, hakuna chama!.
  2. Chama cha kidemokrasia ni kile kinachofuata misingi ya demokrasia vs misingi ya kidictator, Chadema ni chama cha kidemokrasia na kinahubiri demokrasia, kinawajibika ku practice hiyo demokrasia kuanzia ndani ya chama ndipo kije kwenye nchi, "practice what you preach"!.
  3. ZZK ametangaza nia ya kugombea kwa mujibu wa haki zake za kidemokrasia kama mwanachama mwingine yoyote, hajavunja sheria yoyote!, hajakiuka kanuni yoyote!, wala taratibu zozote za chama!. Unless unieleze sheria, taratibu na kanuni za kutangaza nia Chadema zikoje?.
  4. Pamoja na umaarufu wote wa Chadema, Chadema kama chama, kilipaswa kuongozwa na viongozi wakuu 4. viongozi wakuu 4. Mwenyekiti, M/Mwenyekiti, Katibu Mkuu na N/Katibu Mkuu!. Ila kiukweli Chadema inaongozwa na viongozi wawili tuu, and infact kiukweli inaongozwa na kiongozi mmoja tuu!, huyu mwingine ni follower tuu hawezi kumbishia lolote kiongozi wake as a result, Chadema kinaendesha "politics of confrontation" as if kinataka kuchukua nchi kwa mapinduzi na sio kupitia ballot box!.
  5. Nilipo andika "Chadema haijajipanga", nilisema "Chadema Peke yake haiwezi"!. Kiongozi mkuu wa Chadema ni kama mjeshi, yeye anaamuru mashambulizi tuu, ni confrontations tuu badala ya co-oparation!, Ndio maana maandamano na mikutano ya hadhara na misuso ni mtaji mkubwa kwenye M4C.
  6. Uchaguzi wa 2015 ni vita kubwa kati ya waliopo CCM ambao wajajipanga kuwa ving'ang'anizi, na Chadema wanaotaka kuwapokonya. Ili Chadema ishinde vita hii, si lazima itumie jeshi lake kwa kulisongesha mbele kushambulia adui kwa mikutano na maandamano tuu, linahitaji sio tuu kamanda muamrishaji "shambulia!, shambulia!", bali linahitaji kama strategist, na "tactician" atakayetumia tactics kushambulia na sio kuwaswaga tuu wanajeshi wake!. ZZK ndie strategist na tactician, waliopo wana wa swaga tuu kushambulia!.
  7. Ili Chadema ishinde vita hiyo, inahitaji, ushirikiano na umoja ambao ni nguvu!, Ili Chadema ishinde, inazihitaji kura za CCM, za CUF za NCCR Magauzi and the like. Viongozi waliopo wanashadadia zaidi "confrontation" kushambulia tuu, ili kumuangamiza adui CCM badala ya kumbadili mawazo na kumu integrate huyo adui ili umtumie for your own good use!, ambapo ni ZZK pekee ndiye mwenye "spirit ya umoja ni nguvu"!, anaweza kuzivuna kura za CCM, CUF na za Chadema zenyewe kwa kuihesabu CCMna CUF kama washindani na sio maadui!. Hii "compromising" position ya ZZK ndio inamfanya aonekane "msaliti" kitu ambacho sii kweli!.
  8. Katiba iliyopo ina mapungufu kwa kutoweka "quoter" system ya ushindi, hivyo chama kinaweza kuuchukua ushindi wa kutawala Tanzania bila hata ya kura moja kutoka Zanzibar, hivyo kuitawala Zanzibar kimabavu!. Chadema wajiandae kwa katiba mpya itaweka kipengele ili chama kishinde kihalali, lazima ushindi huo ujumuishe angalau theluth moja ya kura za visiwani!. Bila ushirikiano na CUF, sio jinsi yoyote mgombea wa Chadema asiyetaka ushirikiano, atakavyoweza kuvuna theluthi moja ya kura za Zanzibar zaidi ya ZZK!.
  9. Ili ushindi wa 2015 upatikane kwa Chadema, "lazima" (nasisitiza) "LAZIMA" (with no posibility ya any option), Chadema iendeshe siasa za "ukweli" "the politics of truth"!, kwa kukukubali ukweli kuwa CCM ipo, na kuna vitu CCM imefanya ambavyo vinaonekana wazi with naked eyes, na kueleza Chadema wao wakija, watafanya nini tofauti, na sio kulaumu na kushutumu tuu mwanzo mwisho!. ZZK is the only one mwenye kuliweza hili kutokana na kuendesha siasa za ukweli kwa kutumia "Nguvu za Hoja" vs "Hoja za Nguvu"!.
  10. Chadema kama chama, kinapaswa kionyeshe ukomavu wa demokrasia ndani ya chama kwa ku encourage all hopefuls wa nafasi zote kuanzia serikali za mitaa, udiwani, ubunge hadi urais, kujitokeza kwa vingi ili sio tuu kuwapima, bali pia kuwa groom and get the best out of them!. Nia ya ZZK needs support ana uungwaji mkono na Mbowe na Dr. Slaa na kuencourage wengine wengi wajitokeze, badala ya hatua hii ya muasisi kumyooshea ZZK accusing finger, ila pia ZZK anahitaji busara japo kidogo tuu asijibishane na wazee wake!.

Pasco.
 
Back
Top Bottom